Helikopta za zilizokodishwa na CCM kutoka Nairobi, Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Helikopta za zilizokodishwa na CCM kutoka Nairobi, Kenya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MwanaHaki, Sep 29, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  CCM imekodi HELIKOPTA TATU kutoka Nairobi, Kenya, ambazo zinatumika kwenye kampeni ya kutafuta Urais ya JK. Gharama za kukodisha helikopta hizo ni Dola za Kimarekani 5,000 kwa kila saa moja, haijalishi kama helikopta inaruka hewani au imetua hadharani.

  Kwa siku 70 zilizopita, tayari hesabu ni hizi:

  $5,000 X 24 (hours) X ...3 (helicopters) X 70 (days) = $25,200,000!

  Zingegenjwa zahanati ngapi au vituo vingapi vya afya?
  Wangeajiriwa walimu wangapi wa shule sekondari/msingi?
  Zingenunuliwa ambulensi ngapi?
  Yangejengwa madarasa mangapi pamoja na kuyawekea madawati yake?
  Zingejengwa barabara ngapi?
  Wangeajiriwa matabibu wangapi na wauguzi huko vijijini?


  Bado tunahitaji sababu ya kumchagua JK? Bado tuna sababu ya kuirejesha madarakani CCM na wabunge wake?
   
 2. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuhusu uwepo wa hizo helkopta 3 ni kweli hata mimi nimezishuhudia. Jana nilikuwa Kahama, kama kawaida yangu katika pitapita zangu nikaona hizo helikpta 3 ambazo zilitua viwanja vya Buzwagi-Barrick African Gold. Kisha msafara ukaanza kuelekea maeneo ya uwanja wa taifa katika ya mji wa kahama.

  Kilichojiri huko, ilibidi JK akwepe hoja za wabunge wake ili kunusuru mkutano kukumbwa na mchafuko, hii ni baada ya kuona hali inaelekea kuchafuka baada ya Bwana Lembeli mgombea ubunge jimbo la Kahama kupitia CCM kuzomewa mbele ya JK, kwa kile kilichoitwa uongo kuhusu ujenzi wa barabara ya km 4 toka eneo la Phantom kupitia katikati ya mji. Hivi sasa barabara hiyo imejengwa kwa km 1 tu, tena kwa kiwango duni kuliko maelezo jambo ambalo limekuwa kero na gumzo kubwa kwa wananchi wa Kahama. Ikumbukwe pia ujenzi huu umefanyika hivi karibuni na kukamilika wiki ya kuanza kwa kampeni, chini ya kampuni ya Jasco

  Akizungumzia suala hilo JK alisema "......Maelezo yao hayajaniingia akilini, maana hela ilikuwepo ya kukamilisha ujenzi huo na sielewi kwa nini jambo hili lilishindwa kutekelezwa kwa wakati......" Akaendelea "...mkikipa chama changu ridhaa ya kuongoza tena, basi nawaahidi nitalishughulikia hili maana najua ni wapi palipo na mgongano....." Mara kelele za kutokukubali maelezo haya zikavuma.

  Hasira za wadau na wana CCM zilianza mara baada ya JK na watu wake kuchelewa kufika eneo la tukio kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali majira ya saa 9, lakini cha kushangaza aliwasili majira ya saa kumi na mbili jioni hivyo kukuta watu washajaa sumu mithili ya nyoka.

  Yaani ilikuwa patashika nguo kuchanika.
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gawanya hiyo total amount kwa 3 utapata gharama ya helikopta moja ya Chadema. Halafu uliza maswali hayo hayo unayouliza tuone kama wewe ama mkereketwa wa Chadema anaweza kujibu. :becky:
   
 4. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mtizamo hasi! Unajua CHADEMA wanamiliki kupitia mwenzao Ndesa ni tofauti na kukodi. Cheki bei ya helikopta halafu ndio uweze ukafanya milinganisho
   
 5. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ila nadhani kuna utata katika taarifa hizi. Kwa kadiri ya Tanzania Daima, Helikopta zile mbili ni za watu wa CCM walau ndivyo anavyodai Mh Mabere. Soma hapa Marando azilipua helikopta za Kikwete
   
 6. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  This is very serious! na hapo tukishapata kura tunaenda nje kuendelea kulalamika "WE ARE VERY POOR"
  I am fade up, for sure
   
Loading...