hivi kweli jeshi letu la polisi limeshindwa kuweka vijana wake maeneo muhimu ya jiji badala ya kuendelea kuichosha hii helikopta yake ambayo hata asiye na uelewa mkubwa wa vyombo vya anga anajua imeshazeeka? Si afadhali waepushe disaster kwa kununua mafuta kwa ajili ya pikipiki na gari zao badala ya huu utani wanaouendeleza!! Mtu yeyote atembelee eneo la Ubungo Stand ya mabasi madogo, na maeneo ya jirani kuanzia saa moja jioni,atashuhudia jinsi wezi wababe na wasioogopa chochote wanvyosumbua raia, lakini hakuna hata polisi mmoja!!? Tafadhali mkuu Kova, jaribu kuangalia suala hili, mambo mengine mnafanya utani mtupu!!