Helikopta ya CCM yapotea kwa kukosa ramani; yarudi salama

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, helikopta inayotumiwa na CCM katika kampeni za Igunga imeripotiwa kupotea ikiwa angani wakati ikijaribu kutafuta vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Dk Dalaly Kafumu.Taarifa za kupotea kwa helikopta hiyo zilianza kuzagaa jana majira ya saa tano asubuhi mjini Igunga na baadaye zilithibitishwa na mmoja wa maofisa wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa walipotea mara kadhaa baada ya mtu wanayemtegemea kuwaongoza njia kupoteza ramani akiwa angani.

“Unajua tumemchukua mtu ambaye anaifahamu vizuri Igunga ili aweze kuielekeza helikopta mahala pa kwenda, lakini kwa bahati mbaya mtu huyo alipokuwa angani alishindwa kwa sababu ya kupoteza ramani,” alisema ofisa huyo.
Helikopta ya CCM ambayo iliwasili juzi asubuhi na kuanza kutumika katika kampeni, inadaiwa kutumia mmoja wa wenyeji wa wilayani hapo katika ziara yake kutokana na kutokuwapo kwa maandalizi ya ramani inayojulikana kama GPRS.

“Hatuna ramani ya kumwogoza rubani, hivyo tunafanya kazi hii kwa kutumia wenyeji wanaoifahamu vizuri Igunga, kama unavyojua huko angani wakati mwingine ni vigumu kutambua eneo na hili ni tatizo kwetu," alisema ofisa huyo.Helikopta hiyo ya CCM ilirejea mjini Igunga jana majira ya saa tisa alasiri na haikufahamika iwapo kurejea huko mapema kulitokana na matatizo hayo yaliyoelezwa.

Source: Mwananchi
 
Yaani CCM ni mufilisi kabisa, nilishasema lakini before......... Yaani huu ni ujuha, Viongozi waCCM wanatembea na misimu mikubwa mikubwa ya gharama ambayo definetely ina GPS wanapotea njia? Coordinates za vijiji vyote hivyo vya Igunga ziko kwenye mtandao. Lakini pia kama CCM wanatamba kila siku humu kwamba wanafanya kampeni nyumba kwa nyumba kwa nini basi kila mpiga kampeni wao asiende na simu yake eneo linakotakiwa kutua hiyo helkopta akarekodi coordinates wakamtumia Nchemba???? Ina matter of just one hour Vijiji vyote vitakuwa vimejulikana coordinates zake.

Hii imemuumbua Dr. Kafumu kwamba si lolote si chochote, hiyo elimu inamsaidia ni sasa kama anapanda helikopta inayoendeshwa kama baskeli "eti wanaongozwa na mtu anayeijua Igunga, pambaaaaaaaaffffffffff!!!!!!!!!!" Sasa hiyo midigrii yote ya nini kama anashindwa kuelewa hata mambo madogo kabisa kama haya!!!!!!!

Ukienda kwenye hiyo ramani hapa chini ukaizoom, you can get almost all mapped coordinates of that area.

28lrkwp.png
 
ina reflect jinsi utendaji ulivyo CCM na serikali yake!!!

Yaani hili ndiyo jibu sahihi kabsaaaaaa, helikopta kuchelewa kufika kisa kukosa vibali wakati walijua watatumia helikopta zaidi ya mwezi umepita sasa!!!!!!
 
Hii ni aibu, inadhihirisha kuwa Tanzania hatuna wasomi. Hiyo ina reflect utendaji wa serikali ulivyo wa kubahatisha.
 
This is very new to me but also a sad story yaani hawa jamaa kila kitu ni kuunga unga kweli yaweza kufanya kazi ?
 
Mambo ya kuiga hayo! Ccm hakuna kamanda wa anga. Watapotea sana wakati cdm wana pasua anga!
 
Hii ni aibu, inadhihirisha kuwa Tanzania hatuna wasomi. Hiyo ina reflect utendaji wa serikali ulivyo wa kubahatisha.

Hapana mkuu, Tanzania kuna wasomi, kwanini helkopta ya chadema isipotee? Ni wao tu CCM wakurupukaji, wanaiga bila kujua jambo linafanywaje.
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, helikopta inayotumiwa na CCM katika kampeni za Igunga imeripotiwa kupotea ikiwa angani wakati ikijaribu kutafuta vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Dk Dalaly Kafumu.Taarifa za kupotea kwa helikopta hiyo zilianza kuzagaa jana majira ya saa tano asubuhi mjini Igunga na baadaye zilithibitishwa na mmoja wa maofisa wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa walipotea mara kadhaa baada ya mtu wanayemtegemea kuwaongoza njia kupoteza ramani akiwa angani.

“Unajua tumemchukua mtu ambaye anaifahamu vizuri Igunga ili aweze kuielekeza helikopta mahala pa kwenda, lakini kwa bahati mbaya mtu huyo alipokuwa angani alishindwa kwa sababu ya kupoteza ramani,” alisema ofisa huyo.
Helikopta ya CCM ambayo iliwasili juzi asubuhi na kuanza kutumika katika kampeni, inadaiwa kutumia mmoja wa wenyeji wa wilayani hapo katika ziara yake kutokana na kutokuwapo kwa maandalizi ya ramani inayojulikana kama GPRS.

“Hatuna ramani ya kumwogoza rubani, hivyo tunafanya kazi hii kwa kutumia wenyeji wanaoifahamu vizuri Igunga, kama unavyojua huko angani wakati mwingine ni vigumu kutambua eneo na hili ni tatizo kwetu," alisema ofisa huyo.Helikopta hiyo ya CCM ilirejea mjini Igunga jana majira ya saa tisa alasiri na haikufahamika iwapo kurejea huko mapema kulitokana na matatizo hayo yaliyoelezwa.

Source: Mwananchi
Haya mambo ya ajabu sana. yaani rubani wa chopa anaelekezwa na navigator kana kwamba yuko kwenye mbio za magari! Mi nilidhani ndege za aina yote zina vifaa vya kumsaidia rubani kujua yuko wapi ili ajue anapaswa kuelekea wapi. sasa kama anategemea mtu mwingine kumwelekeza, ni vipi atadhibiti usalama wa abiria wake, ambalo ni jukumu lake la msingi?
 
Back
Top Bottom