EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, helikopta inayotumiwa na CCM katika kampeni za Igunga imeripotiwa kupotea ikiwa angani wakati ikijaribu kutafuta vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Dk Dalaly Kafumu.Taarifa za kupotea kwa helikopta hiyo zilianza kuzagaa jana majira ya saa tano asubuhi mjini Igunga na baadaye zilithibitishwa na mmoja wa maofisa wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa walipotea mara kadhaa baada ya mtu wanayemtegemea kuwaongoza njia kupoteza ramani akiwa angani.
Unajua tumemchukua mtu ambaye anaifahamu vizuri Igunga ili aweze kuielekeza helikopta mahala pa kwenda, lakini kwa bahati mbaya mtu huyo alipokuwa angani alishindwa kwa sababu ya kupoteza ramani, alisema ofisa huyo.
Helikopta ya CCM ambayo iliwasili juzi asubuhi na kuanza kutumika katika kampeni, inadaiwa kutumia mmoja wa wenyeji wa wilayani hapo katika ziara yake kutokana na kutokuwapo kwa maandalizi ya ramani inayojulikana kama GPRS.
Hatuna ramani ya kumwogoza rubani, hivyo tunafanya kazi hii kwa kutumia wenyeji wanaoifahamu vizuri Igunga, kama unavyojua huko angani wakati mwingine ni vigumu kutambua eneo na hili ni tatizo kwetu," alisema ofisa huyo.Helikopta hiyo ya CCM ilirejea mjini Igunga jana majira ya saa tisa alasiri na haikufahamika iwapo kurejea huko mapema kulitokana na matatizo hayo yaliyoelezwa.
Source: Mwananchi