Mikolo Mileki
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 611
- 639
Rubani apigwa jiwe jichoni akiwa angani
*Alishambuliwa kwa kombeo na wavamizi wa mgodi wa Barrick
*Alikuwa akipiga picha za eneo la mgodi kutoka juu
Na Joyce Magoti, Musoma
WATU wasiojulikana wamemjeruhi kwa kumpiga jiwe jichoni kwa kutumia kombeo rubani wa ndege iliyokuwa imekodiwa na mgodi wa Kampuni ya Barrick, North Mara, kwa ajili ya kukagua eneo la mgodi huo na kupiga picha ya eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Mgodi huo, Bw. Emmanuel Nyasigo, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 4 asubuhi wakati ndege hiyo namba ZCHUC ikikagua na kupiga picha eneo la mgodi huo, katika kijiji cha Kewanja ikiwa kimo cha meta 50 kutoka ardhini.
Bw. Nyasigo alisema watu hao wanaodhaniwa kuwa wavamizi katika eneo hilo la mgodi walirusha jiwe kwa kombeo ambalo lilipasua kioo na kumpiga rubani na kumjeruhi jicho la kulia.
Alisema ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam ilikuwa na watu wawili ambao ni rubani, Bw. Charles Wanchira (52) raia wa Kenya na msaidizi wake, Bw. Lioly Ernest, raia wa Afrika Kusini na kuongeza kuwa majeruhi alipata huduma ya kwanza na kisha kupelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi.
Bw. Nyasigo pia aliongeza kuwa yamekuwapo matukio mengi ya uhalifu na kwamba katika kipindi cha mwezi huu, kumekuwa na matukio matatu, ikiwa ni pamoja na tukio la kupigwa kwa mlinzi wa mgodi akiwa lindoni kwa kutumia kombeo na kumjeruhi jicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. David Saibulu, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa watu watatu wamekamatwa.
Kamanda Saibulu aliwataja waliokamatwa, kuwa ni Marwa Nyahiri (40), Ginki Shoma (24) na Nyangi Shongo (22).