Helcopter ya Gwajima hii hapa

davidm

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
393
127
Ni miezi kadha sasa tangu ulipozuka uvumi wa Mchungaji Kiongozi na Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kununua Helcopter. Kanisa la hilo limeitambulisha rasmi picha ya helcopter hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook. Kwa mujibu wa Mch. Gwajima, Helcopter hiyo aina ya Robinson 44 itatumika kuhubiri injili katika mikoa mbalimbali nchini.

Pamoja na Hayo, Mchungaji huyo amesema kuwa kama kila kitu kitakwenda sawa; Helcopter itazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda. Tayari usajili wa Chopper hiyo umekamilika na kupewa nambari za usajili 5H-OLY.

.
attachment.php
attachment.php

Pamoja na uwepo wa Helcopter hiyo; Mchungaji Gwajima pia amesema anatarajia mwakani kupokea ndege nyingine tatu; na tayari amepata kibali cha kujenga uwanja wa ndege ujenzi ambao utaanza mwishoni mwa mwaka huu.
 
Attachments

  • IMG_20141015_113637.jpg
    IMG_20141015_113637.jpg
    367.8 KB · Views: 17,134
  • IMG_20141015_113511.jpg
    IMG_20141015_113511.jpg
    339.3 KB · Views: 13,286
Kwahiyo unataka sisi tufanyeje?, Toka toka toka pepo toka. hahahahaaaaa mapepo humuandama mlokole popote alipo ndiyo sababu kila anapo omba anayafukuza toka toka tokaaaaaaaaa
 
Ni miezi kadha sasa tangu ulipozuka uvumi wa Mchungaji Kiongozi na Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kununua Helcopter. Kanisa la hilo limeitambulisha rasmi picha ya helcopter hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook. Kwa mujibu wa Mch. Gwajima, Helcopter hiyo aina ya Robinson 44 itatumika kuhubiri injili katika mikoa mbalimbali nchini.

Pamoja na Hayo, Mchungaji huyo amesema kuwa kama kila kitu kitakwenda sawa; Helcopter itazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda. Tayari usajili wa Chopper hiyo umekamilika na kupewa nambari za usajili 5H-OLY.
. View attachment 194036View attachment 194037

Pamoja na uwepo wa Helcopter hiyo; Mchungaji Gwajima pia amesema anatarajia mwakani kupokea ndege nyingine tatu; na tayari amepata kibali cha kujenga uwanja wa ndege ujenzi ambao utaanza mwishoni mwa mwaka huu.

Hapa Photoshop inahusika,
 
Vizuri,iliandikwa:-siku za mwisho injiri itahubiriwa kila mahali,hata watoto wa kijakazi watamwamini Yesu
 
Hii ndo ya kusafirisha magendo tu. Mtu utanunuaje ndege kabla ya kujenga majengo muhimu? Na mujiulize sana hela ya ndege kapata wapi. Na gharama za kuiendesha zitatoka wapi. Ingekuwa rahisi hata huku tz wanajumuia tungeshachagia zetu.
 
PM aache kazi zake aje azindue chopper tena ya mtu binafsi? ingekuwa hii chopper ni kwa ajili ya kuhudumia jamii kama wagonjwa hapo sawa
 
Back
Top Bottom