Helanya: Jambazi sugu, mshirikina alombaka Mama yake

Appollo 11

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
205
520
Wasalam wana jamvi, poleni na corona. Corona inaua tuendelee kuchukua hatua tutokomeza Corona.

hakika dunia inastaajabisha sana, Leo napenda kushare nanyi kisa cha Jambazi sugu, alokua mshirikina na alieza badilisha saut yake atakavyo.

hii ilikua mwanzoni mwa miaaka ya 2000, ni mida ya saa sita mchana katika Kijiji cha Mwakizega Kitongoji cha muyobozi, mkoni kigoma. Kitongoji hiki kipo kaskazini mwa mkoa wa kigoma na kinapakana na Kikosi cha Jeshi Bulombora. kitongoji hiki ni maarufu sana kwa uvuvi kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Mida hio nipo madrasa na wenzangu tukijisomea Qur an, ustadh hakuepo ndani ya darasa, Ghafla nikaskia saut za kundi la watu likipita barabarani huku wakisema Helanya mchawi, Helanya mchawi, Helanya mchawi, nikatoka mbio na wenzangu kuelekea kwenye tukio, wakat huo nakimbia nkawa najiuliza aiseee kama helanya ni mchawi basi tumekwisha maana kuna mzee mmoja Alikua akiitwa Helanya na alikua Muuza kahawa maarufu, nkililekea kundi nikiwa mwenye woga, maana uchawi bana usikie tuu.

barabara ilikua kama mita 20 kutokea madrasa nkaliona kundi na kulikua na vijana na watoto wengi wakiwafuata watu wawili walombeba mtu kama mnyama alowindwa (Wale wawindaji wanajua namna gan wanavyombeba mnyama walomwinda) ,. kutazama vizuri nkamwona Afande Kasi na Afande Chambile (R.I.P) Hawa walikua ni Privates wa Jeshi walokua katika kikosi kidogo (Muyobozi Deti) na tulizoea kukiita Ngomeni, walikua na kazi ya kufanya Doria katika Ziwa tanganyika kuwalinda wavuvi dhidi ya maharamia katika ziwa Tanganyika.

nikajumuika kwenye kundi tukieleke ngomeni, wakat huo watu wakawa wengi mno. Kwa pamoja tukaenda mpaka Ngomeni maana kikosi sio kikubwa na pale walikuepo wanajeshi kama wanne mpaka sita tu. Ngome hio ilikua ni nyumba moja na mbele yake kulikua na miembe mikubwa af na barabara ya Kigoma kwenda Sunuka ikikatisha.

Maafande walimueka helanya chini na kuondoa mti walokua wamembebea kisha akabakiwa na kamba nza kwenye mikono na miguu, Aiseee pale ndipo alipoonekana vizur jamaa Mrefu, mweusi kias na mwenye mwili wa wastani. Jamaa alikua na sura ya upole mno kama kondoo jike usingeweze kukubali kama ni Jambazi sugu, muuwaji aliekuwa kashindikana.

Kukamwatwa kwakwe, baada ya kuwa tumekusanyika watu wengi sana na maafande wakiwa wanaandaa zana za kumuadhibu jambazi Sugu,. Stori za kukamwatwa kwake Zikaanza kupenyeza,.

Jamaa aliingia hapo kijijini Kwa mguu yaan (alikua akisafir kwa kutembea) baada ya kufika hapo kijijini aliingia kwenye moja ya hoteli na kuagiza cha na maandani vyenye gharama ya Tsh 50 huku mfukoni akiwa na Tsh 30 tu, aliomba msaada na akawa amepatiwa chai akanywa, lakin Katika wahudumu wa hoteli hiyo kuna mmoja alimshutukia na alipojaribu kumtazama vizur akajua ohhh Ngoma imewaka Jambazi katimba tutegemee Vilio, Muhudum akatoka chaap kwenda kikosini kuwastua wajeda aiseee Helanya akili ikamcheza mapema, (Jamaa alikua na akili mingi ilochanganyika na Utamaduni) akaanza kujikataa nje ya kijiji, kutoka nje ya kijiji kulikua na njia mbili yaa Babara bara na nyingine inapita pembeni ya Ziwa (Tuliita njia ya chini) wajeda wakajigawa wakiwa na SMG mmoja akapita chini mwingine akafuata barabara kuelekea mwakizega ( kuna kimlima), Alofata barabara kuu akiwa kwa chini akamwona Helanya kwa juu kabisa akiwa anaondoka zake mdogo mdogo kama kinyonga, Ghafla katika katika ya Helanya na yule afande akatokea Jama mmoja Anaitwa Yamungu (R.I.P) Huyu alikua ni Mgambo na kulikuwa na wakat huo Wanajeshi walikua wakifanya kazi za doria na wanamgambo, Mjeshi akamshutua Yamungu amsimamishe Helanya.

Yamungu akageuka kumfuata Helanya na kumuita ghafla Helanya anageuka akiwa kashika kisu anataka kumchoma yamunu kisu cha kifua. Mara akatokea Yule Afande alopita Njia ya chini Akampiga Helanya kwenye paji la uso kwa kitako cha Bunduki, Helanya akazima wakambeba na kumleta Ngomeni.

Wakat huo jua lilikua Kali lakin ghafla wingu likatanda mvua ikaanza kunyesha, Taratibu za mawasiliano zikiendelea kufanyika uongozi wa kijiji kuwapa taarifa polisi wamfuate jambazi (Wakati huo mtandao unasumbua sana unatembea hata dk 20 kwenda mahala kwenye mtandao).

Helanya akaachwa akinyeshewa na mvua uwanjani, baada ya muda kidogo wanajeshi wamerud wamevaa Raincoat wanamkuta jamaa ameshasogea karibu na mwembe (Ikumbukwe Helanya akigusa Nyasi anapotea) wakamrudisha katika wananchi wakaingia kazini wakaokota majani yote ya miembe, yaan kwa sekunde 5, hata sisimizi akikatisha umbali wa mita mia ungemuona.

Helanya akawa anadhibiwa aseme akatokea wap na anaenda wapi, na kufanya nn, Jamaa haongei, na waka hateteleki, walipiga sana lakin wapi, kuna Afande mmoja alikua wa Burombola alikuja na smoko akamchoma jamaa sehem ya haja kubwa spoko ikaingia yote akaichomoa lkn jamaa wapi yupo ngangali, kuna raia akachukua jiwe kubwa akampiga kichwani Helanya hashtuki.

Watu ikawa tafrani, Jamaa kashindikana na akitoka ni hatari, nakumbuka nlikua na miaka 7 hiv, lakin nliogopa sana hali ile.

Baadae kidg mvua ikakata alikaja Mzee mmoja na shoka, huyu mzee alikua anaish mwenyew na alikua ni mchoma mishkaki ya mbuzi jina lake nmelisahau, Mzee alikua na ghadhabu sana Alishika shoka akaligeuza akaanza kumgonga Helanya kwenye viwiko na kwenye magoti mara kadhaa kwa kila goti na kiwiko huku akitamka maneno ambayo hakuna alieweza kuyasikia, aiseeeee ghafla Jua likarudi pyeeeeee,.. Ndo kwanza shuguli kama ikaanza upya.

Itaendela..............

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna vitu ukivifikiria unajiona umri ushakutupa mkono yaani mtu miaka ya 2000 mwanzoni,means 2001-2003 alikuwa na miaka 7 halafu leo hii upo naye JF mnabishana naye kuhusu Amfifiro!!😂😂😂ila maisha yanaenda kasi sana,na kila mtu na nyakati zake za kutamba
 
Usipoirudia nakutumia radi🤣
 
Usishangae mkuu kuna watoto wa sekondari humu utakuta unabishana nao bila kujua
Ila kuna vitu ukivifikiria unajiona umri ushakutupa mkono yaani mtu miaka ya 2000 mwanzoni,means 2001-2003 alikuwa na miaka 7 halafu leo hii upo naye JF mnabishana naye kuhusu Amfifiro!!ila maisha yanaenda kasi sana,na kila mtu na nyakati zake za kutamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna vitu ukivifikiria unajiona umri ushakutupa mkono yaani mtu miaka ya 2000 mwanzoni,means 2001-2003 alikuwa na miaka 7 halafu leo hii upo naye JF mnabishana naye kuhusu Amfifiro!!😂😂😂ila maisha yanaenda kasi sana,na kila mtu na nyakati zake za kutamba
Ndio juzi mtu kanipandishia weeee hajui kuna waziri nimemlea na kapitia mikonon mwangu-nikajua umri japo nilitaman kukawasha vibao sema ilikuwa humuhumu jf🤣🤣🤣🤣,watu nyerere kafa tuna miaka sita kazini leo mtu anakubinyia pua
 
Back
Top Bottom