Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,991
- 144,322
Kumekwa na hii tabia ya viongozi wa nchi hii kuwaandalia wabunge futari jambo ambalo naamini linafanyika kwa gharama za serikali huku Serikali hii ikikemea matumizi mabaya ya fedha za Umma.
Japo mini si muislamu, najiuliza kuna thawabu yoyote wanapata hawa viongozi kwa kutumia fedha ya umma kuandalia wabunge futari?
Kama ni thawabu au sijui ndio suna,si wangeipata iwapo wangetoa fedha kutoka mifukoni mwao na si kwa kutumia hela ya serikali ?
Tukirudi kwenye mada, idadi ya wabunge ni mita tatu ni tisini na kitu kama sikosei. Sasa gharama ya kuwaandalia chakula watu wote hawa tena wenye hadhi ya ubunge itapungua malaki kadhaa au hata kufika milioni na ushee?
Kwanini Raisi asione umuhimu wa kutoa fedha kama hizi kusaidia ununuzi wa madawati kwa watoto wa kitanzania wanaosoma katika mazingira magumu(wanakalia mawe au magogo huku wamejaa vumbi)
Au ni kwanini hiyo futari isiandaliwe kwa watoto yatima na badala yake wanaandaliwa watu wenye uwezo mkubwa na wanaolipwa vizuri tu?
Halafu hii futari haiwezi kutafsiriwa kama ni takrima kwa chombo kinachopaswa kuisimamia serikali?
Na kama serikali haina dini, vipi kutumia fedha za serikali kugharamia mambo ya kidini yawe ya kikiristo au kiisilamu?
Nawaza sana