Hela wanazotuhumiwa kupewa kina TID zilitolewa na nani na kutoka fungu gani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,883
1.Hiyo milioni mbili inayotajwa kuwa TID kapewa imetolewa na nani?

2.Kama kweli baadhi ya walionekana kwenye vyombo vya habari watakuwa wamepewa hela, itakuwa wamepewa jumla ya shilingi ngapi?

3.Inawezekana mtu akatoa hela hizo zote kutoka mfukuoni mwake?

4.Kama kuna kikundi au taasisi ndio imehusika kutoa hizo fedha,watatoa tu hela zao hivi hivi bila kuwa na maslahi?

5.Kama kuna maslahi,yatakuwa ni maslahi gani?

6.Kwasababu zoezi hili lilikuwa likiratibiwa na serikali,inawezekana kuna mkono wa serikali?

7.Kama kuna mkono wa serikali,ni afisa gani kahusika na amezitoa katika fungu gani?

8.Kama hizi "clip" ni fake,kuna yoyote miongoni mwa wanaotajwa amejitokeza kukana yanayosemwa?

9.Mama Sepetu na Steve Nyerere kuna yoyote kati yao amejitokeza kuzikana hizo clip mpaka sasa?

10.Kama hizi clip ni za kweli, Mama Sepetu na Steve Nyerere hawatashili kuhojiwa na vyombo husika?

11.Swala hili likipita pasipo wahusika kuhojiwa au likaishi tu kimya kimya,itakuwa ni hivi hivi tu?

12.Wote wanaotajwa kama kweli wanasingiziwa, ina maana wote mpaka muda huu wameshindwa kutumia hata mitandao ya kijamii kukanusha /kutolea ufafanuzi?

Kama kina TID walipewa/hawakupewa hizo hela basi tunaomba kina TID na hao wenzake wajitokeze hadharani wakanushe au wakiri kupewa hizo fedha lakini wakikiri watuambie walipewa na nani.

Mwisho kama ni taasisi ya serikali ikihusika bila shaka taratibu zilifuata hivyo tutaomba kuona document za malipo hayo.

Ukiona giza linazidi,ujue ndio kunakaribia kukucha.
 
Bado na ile kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoa huo!!!!

Kiongozi wake anaonekana kila mara katika vyombo vya habari kumtetea mtu huyu kuliko anavyoonekana akihubiri katika Nyumba ya ibada ya dini yake!

Kiongozi wa kamati hiyo anaonekana akikatiza maofisi ya umma kuliko anavyokatiza katika maeneo ya viunga vya watu wa imani yake.......unaweza kudhani kuwa naye ni mtumishi wa umma na unaweza kukosea ukamuomba akupeleke au akuelekeze ofisi fulani,maana kila siku ukienda unamkuta katika ofisi hiyo ya umma.

Anatumia muda mwingi kukaa katika ofisi hiyo ya umma kuliko muda anaotumia kuhubiri

[HASHTAG]#2000000[/HASHTAG]

Tunamuhoji huyu kiongozi wa dini,kulikoni?
 
1.Hiyo milioni mbili inayotajwa kuwa TID kapewa imetolewa na nani?

2.Kama kweli baadhi ya waliojitokeza mbele ya vyombo vya habari siku ile watakuwa wamepewa hela,itakuwa wamepewa jumla ya shilingi ngapi?

3.Inawezekana mtu akatoa hela hizo zote kutoka mfukuoni mwake?

4.Kama kuna kikundi au taasisi ndio imehusika kutoa hizo fedha,watatoa tu hela zao hivi hivi bila kuwa na maslahi?

5.Kama kuna maslahi,yatakuwa ni maslahi gani?

6.Kwasababu zoezi hili lilikuwa likiratibiwa na serikali,inawezekana kuna mkono wa serikali?

7.Kama kuna mkono wa serikali,ni afisa gani kahusika na amezitoa katika fungu gani?

Kama ni kweli kina TID walipewa hizo hela basi tunaomba kina TID na hao wenzake wajitokeze hadharani wakanushe au wakiri kupewa hizo fedha lakini watuambie walipewa na nani.

Mwisho kama ni taasisi ya serikali ikihusika bila shaka taratibu zilifuata hivyo tutaomba kuona document za malipo hayo.

Ukiona giza linazidi,ujue ndio kunakaribia kukucha.
Unaonaje kama wangeanza kina Msukuma na kina Bulaya kwanza kujisafisha?
 
Aliyerusha ile audio alidhani anamsaidia Makonda na kumbe anamharibia zaidi. Mengi yamejuliana kama,

1.Makonda anatumia madaraka yake vibaya kwa maslahi binafsi kwa kisingizio cha vita ya dawa za kulevya.tuhuma kuwa anahonga wasanii ali waseme anachotaka ni uthibitisho kuwa hii vita ni usanii mtupu.
2. Makonda anatumia vyombo vya dola vibaya kwa maslahi binafsi.Uthibitisho ni pale alipodaiwa kumpiga stop Steve asiende kumuona Wema.

3.Mkuu wa nchi hajui nia ovu ya makonda hasa anapompa support hadi kuonekana bunge ndio kimbilio la kutatua uonevu wa Makonda.
4.Makonda anatumia madaraka yake kuwapata warembo awatakao.Tuhuma za kumpagishia nyumba masogange na wakati huohuo kumtongoza Wema ni uthibitisho tosha.

Yapo mengi yaliyoibuliwa na hiyo clip na huenda ikamfungua Mkuu ili amfahamu vyema kijana anayemwamini sana.
 
Namba 4!!!!!

Imenisikitisha sana!!!!
 
Tutafika ila ni kwa mbinde,

Nchi na uongozi badala y kufanya mambo ya msingi wanatafuta coverage kwenye media kila siku,

Viongozi wasio na maadili wapiga dili lakini kila kukicha wanajitia watetezi wa wanyonge,

Viongozi waliojaa kiburi na vitisho kwa wananchi ambao hata hawana uhakika wa mlo,

Viongozi wa nchi kuanzia juu mpaka chini MATAPELI tu
 
Back
Top Bottom