Heko Waziri Mpina, matokeo chanya uzuiaji uvuvi haramu tumeyaona

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Katika mawaziri waliofanikiwa kwa kiwango cha juu uwezi kumwacha waziri Kijana Mpina, huyu alipigana sana kuondoa uvuvi haramu, amepiga marufuku kuvua samaki wadogo, samaki kuwekewa sumu. Ni waziri aliyechoma nyavu nyingi sana ambazo zilitumika katika uvuvi haramu. Pamoja na kupata changamoto wabunge wenzie wakimchamba kwa kupima samaki kwa rula, lakini aliyemchagua alimwona bado anafaa akamwacha. Ni waziri ambaye hana mchezo kabisa kwa kufuatilia sheria iliyowekwa.

Wavuvi wengi walimchukiasana kwani waliona anawapotezea kipata, wengi walifilisiwa, lakini sasa hivi tumeshududia sehemu nyingi kuna samaki wakubwa na wengi sana, samaki wameshuka bei. Hata hivyo bei inaweza kushuka zaidi ila wafanyabiahsa wana janja sana kuhakikisha bei haishuki bali kupandai.

Mwanza sasa hivi bei ya samaki ipo chini ukilinganisha na huko nyuma bei yasamaki ilikuwa haishikiki.
 
Mpina bwana!! Kwa hiyo umekuja kujimwambafy humu JF wakati umeleta amasikini kanda ya ziwa na vipimo vya rula kwenye samaki? Unakumbuka ulivyotuma vijana wako bungeni kupima samaki kwenye chungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpina bwana!! Kwa hiyo umekuja kujimwambafy humu JF wakati umeleta amasikini kanda ya ziwa na vipimo vya rula kwenye samaki? Unakumbuka ulivyotuma vijana wako bungeni kupima samaki kwenye chungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umaskini walijiletea wenyewe kwani uvuvi haramu ulisababisha samaki kukosa na kuwa bei ghali muno wakati ni kitoweo cha kawaida tu.
 
Anaweza akawa amefanikiwa kwa hilo lakini gugu maji linalotembea ziwa victoria mbona limemshinda, gugu maji mpaka linazuia kivuko!!
 
Tuambie kafanikisha viwanda vingapi vya samaki? Vijana kiasi gani wamepata ajira? Maisha ya wavuvi yamebadilika kiasi gani? Hayo mengine ni madogo na wenzetu walishayadhibiti zamani sana Sifia vitu vya maana yaani vitu exceptional
 
Anaweza akawa amefanikiwa kwa hilo lakini gugu maji linalotembea ziwa victoria mbona limemshinda, gugu maji mpaka linazuia kivuko!!
gugu amji lipo siku nyingi linaanzia mto Kagera, labda waweke chujio, gugu maji bila kupata fedha za UN hatuliwezi kabisa
 
Tuambie kafanikisha viwanda vingapi vya samaki? Vijana kiasi gani wamepata ajira? Maisha ya wavuvi yamebadilika kiasi gani? Hayo mengine ni madogo na wenzetu walishayadhibiti zamani sana Sifia vitu vya maana vitu exceptional
Viwanda vilivyopo vinapata samaki wa kutosha, na wananchi wanaendelea kufurahi zao hili sio kama zamani watu walikuwa wanakula mapank, ajira zimeoongezeka kiasi kwani mtu alikuwa anabeba samaki kumi na tano kwenye tenga kupeleka kuuza sasa anabeba mmoja tu anatosha,

maisha ya wavuvi yanaendelea vizuri kwani kilo wazouza zimeoneza kipatao, wanapata minofu ya kutoshqa, mafuta ya samaki ya kutosha ambavo zamani ukuweza kupata hayo, wale wa zamani walishindwa kwani samaki wengi walivuliwa kwa sumu na samaki watoto waliuuliwa na vizazi vyao
 
Kazi iliyofanywa na serikali kudhibiti uvuvi haramu ilikuwa na umuhimu mkubwa kama inavyodhihirika sasa hivi.

Nakumbuka wanasiasa wabezaji walitumia nguvu nyingi kukejeli na kuonyesha zoezi halina manufaa yeyote.

Namkumbuka Zitto na wengine ambao kazi Yao ni propaganda za nguvu kuonyesha kitu kinachofanywa na serikali kina mapungufu na hakifai. Walisema zoezi halina manufaa na halitasaidia chochote labda Kenya na Uganda nao washiriki.

Wapiga zumari waliungwa mkono na wafuata upepo hasa wa JF tuliowazoea. Threads za kejeli zilikuwa haziishi hapa.

Baada ya zoezi kumekuwa na manufaa makubwa sana. Wavuvi walikiri hili mapema. Na takwimu za kuthibitisha zipo. Lakini wapiga zumari wakakaa kimya ukweli mchungu ulipodhihiri.

Hii ni mbinu mojawapo ya propaganda inayowateka wasioshirikisha ubongo.
- Aminisha watu kwamba serikali inafanya makosa kwa kutoa taarifa nyingi na mara nyingi kupinga jambo hilo. ---Tangaza sana Kama kuna mapungufu madogo hata kama hayaathiri matokeo chanya ya mpango mzima kwa mapana yake ili kuondoa imani kwa watu
-Aminisha kwamba serikali haijali maslahi ya watu hivyo kujenga na kuchochea hasira

Kiufupi propaganda zote mnazoziona kwenye social media ni well calculated na centrally coordinated.

Kinachofutahisha kikundi kilichojipanga kuteka mass media na social media hakitafanikiwa kuteka akili na mtazamo wa watu wa kawaida. Sababu ni simple, wao wanaguswa na matokeo ya juhudi za serikali, na siyo upotoshaji unaofanyika JF na kwingineko.
 
Mimi nakuunga mkono. Ni Mhe. Waziri aliye na msimamo. Mawaziri wenziwe walimpiga vita lakini akawa na msimamo usiyoyumba. A Hongera sana Mhe. Mpina. Kwenye utawala kuna kupongezwa na kulaumiwa.
 
Mleta mada kumbuka kuwa kuna watu humu jukwaani watakaokushambulia kwa kumsema vizuri Mpina wakisema kwamba ni wa ile kanda maarufu awamu ya tano.

Siku hizi kutokea kanda hiyo ni dhambi ya mauti, hawachelewi kukimbilia katika mawazo ya ukabila na ubaguzi.
 
Mleta mada kumbuka kuwa kuna watu humu jukwaani watakaokushambulia kwa kumsema vizuri Mpina wakisema kwamba ni wa ile kanda maarufu awamu ya tano.

Siku hizi kutokea kanda hiyo ni dhambi ya mauti, hawachelewi kukimbilia katika mawazo ya ukabila na ubaguzi.
wapo wengi lakini watajiju, mimi ni mpenzi wa samaki, huwa naenda pale tegeta kwa ndevu nyumaya kituo, kuna samaki unawakuta bado wana wekundu kabisa kama wamevuliwa leo, ni wakubwa na wanamafuta, ya kutosha, huko nyuma wakaanga samaki walikuwa wanatuuzia samaki wameoza kwa sumu,

sasa hivi ukinunua samaki hata kwa wakaangaji radha unaisikiakabisa, pale tegeta kwa ndevu, yule jamaa kaajiri vijana wengi wa kuchuna samaki ukimaliza kununua na kukatiwa vipande, kuna mtu anasema wavuvi walipoteza ajira, lakini kuna wakina mama wengi wajiajiri wanuza samaki stand na viunga vyote vya dar es salaam
 
Back
Top Bottom