Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 986
Umuofia wanajukwaa!
Kwanza kabisa nitoe masikitiko yangu makubwa sana kwa chama cha madaktari Tanzania MAT, sikutegemea kuona kua hiki ni taasisi iliyojaa unafki mwingi na kujipendekeza. Haina msaada wowote katika wala katika taaluma ya tiba nchini. Ninashangaa na kushtuka mpaka sasa MAT hawajaweka wazi kua Tanzania tuna wimbi la pili la ugonjwa wa COVID-19 kama ambavyo TLS wamesema bayana na pia baadhi ya viongozi wa dini wamesema.
Hongereni sana chama cha wanasheria Tanganyika TLS kwa kuweka msimamo wenu juu ya hali inayoendelea na kuweka wazi kabisa umma kua tuko katika kipindi kigumu cha Wimbi la pili la ugonjwa wa COVID-19. Mmetimiza wajibu wenu kama alivyotakiwa katika vifungu vya sheria za kuanzishwa kwenu. Hakika ninyi si wanafiki ni wakweli na kweli mnasimsmia haki za watanzania ikiwemo ya kuishi.
Yaani chama cha Madaktari ambacho wataalam wake 24hrs wanashinda na wagonjwa na wanaidhinisha vifo vyao washikwe kigugumizi kusema tatizo nini? Wameamua kuiweka taaluma yao mifukoni na kuamua kufanya siasa?
Hiki chama hakifai, wakitaka kujua ni kwanini hakifai watazame michango ya vyama vya Madaktari toka kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Rwanda na hata mataifa makubwa ya Marekani,Canada,Australia,Uingereza nk. Kivunjwe mara moja hiki chama hakina tija kwa taifa.
Mwisho lakini kwa umuhimu sana, tunawashukuru sana viongozi wetu wa madhehebu baadhi ya dini waliojitokeza wazi wazi kusema kua tunasumbuliwa na tatizo hili la wimbi la pili la homa ya mapafu. Hongereni sana mmeikwepa dhambi ya uongo na hata siku ya hukumu mtalipwa wema wenu.
Ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari, tatizo lipo na linatisha wala hakuna unafki katika hili.

Tamko la Tanganyika Law Society(TLS), Juu ya Wimbi la Pili la Mlipuko wa Ugonjwa wa Korona nchini
TAARIFA KWA UMMA Ndugu Watanzania, TAMKO LA TLS JUU YA KUWEPO KWA WIMBI LA PILI LA UGONJWA WA KORONA NCHINI Mnamo tarehe 13 Februari 2021 Baraza la Uongozi la TLS lilikutana kutekeleza majukumu yake na moja ya ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni umuhimu wa TLS kuitaka Serikali kutoa tamko...
www.jamiiforums.com