Heko Meneja Dawasa - Kawe. Waziri Mbarawa huyu kijana ni mbunifu

petrol

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
596
428
Ni kipindi kifupi umekuwa Meneja wa Dawasa - Kawe lakini umekuwa msikivu mzuri wa changamoto za eneo lako la kazi. Pia umeonyesha ushirikiano wa kuigwa. Wakazi wa Mwenge ni mashuhuda. Ubarikiwe sana pamoja na wenzako katika ofisi ya Dawasa - Kawe.

umebuni mfumo shirikishi siyo tu ofisini mwako bali umepanua wigo kufikia wateja wako. Tija ya mfumo shirikishi na kupeana taarifa imeanza kuonekana.

Mheshimiwa Waziri Mbarawa, sina njia nyingine ya kukufikishia ujumbe kwamba Meneja wako wa Dawasa - Kawe amebuni mfumo wautendaji kazi ambao utaweza kusaidia maeneo mengine nchini katika kukabiliana na changamoto kadhaa katika utoaji wa huduma ya maji katika mijini.
 
Back
Top Bottom