Heko Magufuli Mpango ulioko jikoni umenifurahisha na umejirekebisha kwa 90% long live JF, awazo yote yamechotwa hapa

Hahaha britanicca we muongo sana. Hapo kipi nyeti. Uchaguzi serikali za mitaa unakuja hilo nalo ni nyeti. Mnajitungia habari mnaziita tetesi. Uandishi wa habari sio taaluma kabisa.
 
Maandishi yako huwa yanakuwa na ukweli kwa asilimia fulani...

Ameruhusu baa saa 24
Amezuia bomoa bomoa nchi nzima
Amezuia kuhamisha wananchi waliojenga kwenye hifadhi.

Kweli ccm mnacheza na akili zetu.
Heri ya Mwaka Mpya kwenu wana jamii forums wote,
Kuna habari Nyeti ambazo zimetoka sehem nyeti na unyeti wake,
Mkulu katika kipindi hiki cha mwaka 2019 kitakuwa kizuri kwa watanzania na wasio watanzania lakini waishio Nchini Tanzania,

Mwaka 2016-2018 umekuwa miaka ya kuangalia mwenendo wako wa uongozi,
nimefurahishwa sana na ulivyobadili gia na kuanza mwelekeo mwingine,

1.Siasa zitaruhusiwa japo haitakuwa moja kwa moja ila itakuwa kama zimeachiwa fulani hivi, hii itakuwa tofauti na miaka ya nyuma hasa kwa wapinzani waliobanwa sana na kufunguliwa kesi mbali mbali kisa mikutano ya hadhara na iasiyo ya hadhara,

2.Kubana matumizi kutapunguzwa kwa asilimia kubwa maana mambo makubwa mengi yaliyogharimu hela ya watanzania wa chini hasa wanyonge na walipa kodi yameisha kwa asilimia zaidi ya 50, yaan vimebaki vichache kama elimu bila malipo itaendelea kugharimu ,na kuhamishia makao makuu Dodoma,

3.Kuachia hela kwenye mzunguko, (money circulation) , hali ya kiuchumi haitakuwa ngumu kama mwaka uliopita hii ni kutokana na ushauri maalumu wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa uchumi wa nchi za ulimwengu wa tatu,

4.Tutaanza kuziona Hotuba makini zilizo pangiliwa na zisizo na vitisho kwa watanzania na wasio watanzania zinazotolewa na mheshimiwa rais,

5.Ubabe utokanao na weledi mdogo wa wateule wa rais dhidi ya wanaowasimamia kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi utapungua maana kuna maelezo maalumu ya kuwa hasa wanaoteuliwa na mkulu kuacha kuchukua maamuzi ya pupa na kuweka watu ndani,

6.Kodi zisizo za lazima kwa watanzania na wafanya biashara wakubwa na wadogo zitaangaliwa upya na zitakuwa na fomula maalumu za kuzijua siyo kukadiria,

7.Wanafunzi wa kunufaika na Mkopo wa Chuo Kikuu na elimu ya juu wataongezeka na kufikia asilimia zaid ya 90 ya wanaoomba,

8.Vyombo vya habari na wamiliki wote wa vyombo hivyo wataheshimiwa na kupewa uhuru

yapo mengi sana



Britanicca
 
Hiyo ni sawa ila kuna muhimu ambazo umesahau nayo
1 mishahara ya watumishi wa umma kupanda
2 ajira mpya zitatangazwa serikalini
Akifanya haya yote 2020 wakati wa kura asfanye kampeni akapumzike zake kura zote zinamhusu.
 
Back
Top Bottom