Heko M. M. Mwanakijiji kwa makala (gazeti la Mwanahalisi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heko M. M. Mwanakijiji kwa makala (gazeti la Mwanahalisi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by echonza, Dec 19, 2009.

 1. e

  echonza Senior Member

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa vile sina mahali pengine pa kusemea na kuweza kumpongeza ndugu M. M. Mwanajijiji kwa makala yake aliyoandika kwenye gazeti la Manahalisi la tarehe 9 Desemba 2009 yenye kichwa cha habari "Kikwete amekwishafanya uamuzi mgumu", napenda kutumia fursa hii kumpongeza Mwkjiji kwa kazi ambayo ni muhimu kwa umma katika suala zima la kuwawezesha kifikira (attitude empowerment) kuhusiana na sifa za kiongozi bora. Mwkjj ameweza kuchambua kwa makini juu ya kiongozi bora ni nani, kwamba si yule afanyaye maamuzi magumu bari yule anayefanya maamuzi bora. Vyovyote vile mtu anavyoweza kuita hapa kama anamanisha maamuzi ambayo yako kwa manufaa ya umma ambao ulimuweka madarakani kiongozi husika, basi huo ndiyo uongozi bora aliomaanisa mwkjj.

  Sina shaka pia na maana ya maamuzi magunu yaliyotajwa kwenye kongamano la Mwalimu Nyerere bali pia ulimaanisha maamuzi yale yenye maslahi kwa umma isipokuwa wao walitumia neno gumu badala ya bora kwa maana kwamba, kulingana na hulka na kushuka kwa maadili ya watanzania nchini, kufanya maamuzi bora mtu ataonekana kama vile anafanya maamuzi magumu kwao kuyatekeleza yapo ni maamuzi bora na yenye maslahi kwa umma.

  Kwa kuwa makala ya Mwkjj inaujumbe kwa umma kuhusiana na sifa za kiongozi bora na wajibu wake kwa waliomchangua, napenda kuwaletea baadhi ya sehemu ya makala yake ili tuweze kujikubusha tuliosoma na tusiosoma tuweze kuupata ujumbea aghalabu kwa kifupi na hatimaye tuchagie ili kupanuana mawazo na uelewa wetu juu ya viongozi ambao watanzania wanatakiwa kuwachagua katika uchaguzi mkuu ujao akiwemo Rais wa nchi, nayo ni kama ifuatavyo:

  "Uongozi ni uwezo. Uongozi siyo elimu, uzoefu au umri. Hivi vyote vinaweza kumsaidia kiongozi kuwa kiongozi mzuri. Lakini havimfanyi mtu kuwa kiongozi mzuri au hata kuwa kiongozi.
  Hapa hatuna budi kusema wazi kuwa uongozi ni uwezo. Yaani, mtu ambaye anataka kutuongoza ni lazima awe ni yule mwenye uwezo wa kutufanya tuamini kuwa anaweza, ana maslahi yetu moyoni mwake na yuko tayari kusimamia maamuzi yake na kukubali matokeo ya maamuzi hayo.
  Kiongozi mzuri siyo yule anayetuahidi nini atatufanyia bali yule ambaye yuko tayari kufanya yale ambayo sisi tunayataka kama wananchi.
  Uwezo huu wa kiuongozi unamtofautisha mfuasi na kiongozi. Tangu utoto tumevutiwa na watu ambao wanatuonyesha uwezo wa kutushawishi kukubaliana nao. Kama ilikuwa twende tukacheze mpira au kucheza kombolela, kwenda kucheza “ready” au kwenda kuruka kamba; kutoroka darasani au kwenda kujisomea!
  Wale waliotushawishi utotoni ni hawa tuliwafuata. Wale ambao walikuwa ni washawishi utaona hata baadaye ukubwani wamekuwa ni watu wa ushawishi vile vile na kuongoza wengine (katika mema au mabaya)!

  Uwezo huonyeshwa katika maamuzi. Mojawapo ya maneno ambayo tumeyasikia karibuni ni kuwa tunahitaji viongozi wanaoweza “kufanya maamuzi magumu.”
  Tumeyasikia haya kwa sauti zaidi katika kongamano siku chache zilizopita, ambapo baadhi ya watumishi wakongwe wa nchi yetu walipaza sauti zao wakitaka Rais Kikwete kufanya “maamuzi magumu” na hivyo kuonyesha uongozi. Naomba kutofautiana nao.
  Rais Kikwete hahitaji kufanya maamuzi magumu! Ameshayafanya, yanatosha. Si yeye ndiye aliyemteua Andrew Chenge licha ya Chenge huyohuyo kuandamwa na tuhuma za ufisadi katika suala la rada?
  Ni Kikwete aliyeruhusu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Samwel Sitta, kusulubiwa katika vikao vya chama kiasi cha kutishia utawala wetu wa kikatiba. Ni yeye aliyeliacha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) linunue dege lile bovu na kujiendesha kwa hasara huku akiendelea kulimwagia mabilioni ya fedha za walipa kodi.
  Si yeye na serikali yake waliamua kuwaacha watoto wetu karibu 30 kwenye baridi la Ukraine na kuwalazimisha kuacha masomo ya chuo kikuu kwa kisingizio kuwa “serikali haina pesa” wakati leo hii wanatuma watu karibu sabini kwenda kwenye mkutano huko majuu wakati yeye na wenzake wakicheza kwenye bembea za Cuba? Wanataka Rais Kikwete afanye maamuzi gani magumu?
  Ndugu zangu, uongozi siyo kufanya maamuzi magumu! Uongozi ni kufanya maamuzi bora! Tukitaka kiongozi yeyote ati afanye maamuzi magumu wakati mwingine tunampa ruhusa ya kufanya maamuzi magumu ya nani amridhishe.
  Kama uamuzi ni kati ya kuwakamata wahusika wa Kagoda au kuifunua Meremeta na kuwawajibisha wote wahusika na kiongozi akaamua kutofanya lolote kati ya hayo akiamini kuwa huo ni “uamuzi mgumu” je tutamlaumu?
  Uamuzi bora hutanguliwa na misimamo bora: Mojawapo ya mambo ambayo yanamtofautisha kiongozi bora na bora kiongozi ni misimamo aliyonayo. Vitu ambavyo vinanisumbua sana binafsi ninapoangalia watawala wetu ni kuwa misimamo wanayochukua ni ya kusikitisha. Bila ya mtu kujifunza kuchukua misimamo bora mtu huyo hawezi kuchukua maamuzi bora.
  Kiongozi ni lazima awe na msimamo wa kuchukia rushwa ili aweze kuchukua maamuzi ya kupigana na rushwa; kiongozi ni lazima awe na msimamo wa kukataa uonevu ili achukue maamuzi ya kutokumuonea mtu.

  Misimamo bora hutanguliwa na fikra bora. Hata hivyo, mtu hawezi vile vile kuchukua misimamo bora kama fikra zake na mtiririko wa fikra zake siyo bora. Mtu ambaye hajajifunza kufikiria na kujenga hoja na kuzipima kwa kina atajikuta anachukua misimamo mibovu.
  Kama mtu anaamini kuwa “wazungu wako mbali” na kuwa “wazungu siyo mafisadi” mtu huyo anapoenda kujadiliana na wazungu hawezi kufikiria kuwa wanamuingiza mkenge!
  Hivyo, ili mtu aweze kufikia misimamo bora ni lazima awe na fikra bora ili hatimaye aweze kuchukua maamuzi bora. Nje ya hapo utaona kuwa mtu mwenye fikra za uduni atakuwa na misimamo ya uduni (kama kwenye mikataba) na matokeo yake atachukua maamuzi ya mtu duni.
  Ni kwa sababu hiyo, kama taifa na kama wananchi unapokuja uchaguzi huu mkuu ni lazima tuwapime viongozi wetu siyo kwa kile wanachosema bali kila wanachosimamia na hiki kinaonekana kwenye historia zao.
  Kiongozi anayeibuka sasa hivi na misaada kwenye jimbo lake na ahadi kibao za nini atafanya ni kiongozi wa kuogopwa. Viongozi bora hawaanzi wakati wa uchaguzi. Ni wananchi wenzetu ambao tumekuwa nao wakituonyesha njia na kutushawishi katika mambo kadhaa hata bila ya wao kuwa na maslahi ya uchaguzi au kuchaguliwa. Hawa ndio viongozi ambao hutambulikana kwa fikra zao, misimamo yao na maamuzi yao bora.
  Hawa ndio viongozi ambao ndani ya “hizi kumi na mbili” tunawahitaji ili kuweza kuanza kuushinda ufisadi na kuanza kujenga misingi ya taifa jipya la kisasa. Vinginevyo, tuwe tayari kupokea “bora viongozi”."

  Heko Mwkjj!!!
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hongera nimesoma kweli hapa lazima Tambwe na kundi walie kwa sauti kubwa .
   
 3. e

  echonza Senior Member

  #3
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kilio chao hakitasikika kwa wananchi walio makini maana kitakuwa kimejaa unafiki tupu! Maana ni kundi la wababaishaji tu, ambao maamuzi wayafanyayo hayalengi masilahi ya umma, bali kurudisha gharama zao walizotumia kuhonga wakati wa chaguzi zilizopita.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Dec 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Echonza, hongera kumpongeza Mzee MKJJ. Hiki ni kichwa sijaona mfanowe humu JF. Natamani sauti yake isikike kwa Watanzania wengi zaidi na ikibidi apande jukwaani. Japo MMKJJ ni CCM, naamini ni miongoni mwa wana CCM wachache wenye guts to 'call a spade, a spade' not a big spoon!.

  japo anaendelea
   
 5. e

  echonza Senior Member

  #5
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sure, ni kazi yetu sote kutumia uwezo wetu mdogo tulio nao kuuelimisha umma. Hata hivyo, binafsi siko kupinga u-CCM bali napinga kundi lolote linaloweza kujitokeza iwe kutoka CCM na vyama vingine kutetea wachache kwa gharama za wengi (umma), hasa maskini walipakodi!!!
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  tunahitaji fikra mbadala kama za wakina babu yangu Mwanakijiji na watu wote makini ili taifa letu liende mbele zaidi ya hapa tulipo na pia itakuwa vizuri kama waandishi kama hawa wakija kama 50 hivi Tanzania
   
 7. b

  bigilankana Senior Member

  #7
  Dec 19, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aende bungeni akaungane na Zitto maana sifa yao moja, kujenga hoja na sio kupiga kelele.
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Unamuongelea Zitto wa zamani au wa sasa hivi?
  Nadhani Zitto wa sasahivi amebadilika kidogo!(no offense pls!)
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Labda kama una info tofauti na kigezo cha michango yake hapa JF ,ambapo in my opinion MKJJ is nothing close to be a "mwana CCM" Kwa position aliyonayo,angekuwa mwa CCM asingebother kuwakosoa...Hayo ni maoni yangu binafsi,i might be wrong,maana si kuna CCM wapiganaji?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Sijui niseme nini; nanyenyekezwa na utambuzi wa mchango wangu kidogo katika mapambano haya ya fikra. Natumaini ni cheche kiduchu tu na ni kama tone la maji tu. Fikiria vyote vikiongezeka kwa wingi wake! vyote viwili vyaweza kuwa ni mwanzo wa mlipuko au wa mafuriko makubwa. Ni kama anguko la theluji moja toka angani; mwisho wake ni mwanguko wa theluji usio kifani! Tuko pamoja.
   
 11. L

  Lampart Senior Member

  #11
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Tupatie nambari yake ya kadi ya CCM!!!!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280

  hahaha Pasco.. usiumie sana; kadi wamenikatalia ati nitakuwa pandikizi; kwa hivyo fikra zangu bado ni huru.
   
 13. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #13
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280

  Kweli mkuu, lakini kuna uwezekano amekosea kuzaliwa Tz!
   
 14. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama kuandika ndio kufanya kazi basi warioba angekuwa waziri mkuu bora sana tanzania lakini aliishia kuwa non-productive wakati wake alipokuwa na cheo hicho akawa amebakia kuvuta sigara hakuna chochote alichofanya muda wote..lakini kuandika safi sana

  kama kuongea na kuteka hadhira na kufarahisha watu katika maongezi yako ni ubora wa kazi na maendeleo kwa watu nyerere angekuwa kuwa bora wakati wake lakini aliishia kuchekesha na kuongea illusion zake miaka yake yote na taifa likabaki na msingi mbaya hadi leo

  kama makala za mwkjj JF na kwenye magazeti ni kazi na tija na bora kwa maisha ya watu du mbona ulimwengu, na rafiki zake wangeshasaidia dunia...

  Kiongozi siyo maandishi na malalamiko ni kuwa na kiwanda, kuajiri watu kwa tija na kuingia kwenye production line ili kusaidia taifa kuliko kina ..mwankjj ambao ni watengeneza nadharia bila kujua uhalisia..malalamiko, maoni, blah blah jiulize umeajiri wa Tanzania wangapi wewe kwa elimu yako ili uondoe umaskini kwa watu? huyo ndio kiongozi siyo magazetini wala JF..tukupime!
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  unaweza kufikiria umeandika hekima; je wale walimu wa vyuo vikuu ambao kutwa nzima kazi yao ni kuandika na kujenga nadharia wanazalisha wapi? Je wale walimu wa shule ya msingi wanaotoa mafunzo kwa watoto wetu wana viwanda gani vya kutoa ajira?

  Ungetumia sekunde chache kufikiri ungeona kuwa Mtume Mohammed hakuanzisha kampuni na wala hakuajiri wetu na yeye Yesu Kristu hakutoa ajira!

  Ukiangalia kwa karibu utaona kuwa Plato, Socrates, na wale wataalamu wa kale waliojenga nadharia tunazozitumia leo hii hawakuwa na makampuni zaidi ya kujenga hoja kwa kutumia kalamu zao na uwezo wao wa kufikiria.

  Kama unaamini kuwa watu wote ili watoe michango yao kwa jamii ni lazima watoe ajiri, wamiliki viwanda, n.k basi unageuka kuwa mkanaji wa historia na msaliti wa ukweli wake. Jamii za mataifa zimeundwa na kuboreshwa na michango ya watu mbalimbali kwa kutumia uwezo, nafasi, na vipaji vyao mbalimbali. Wote kama mashine kubwa yenye sehemu mbalimbali hutoa michango yao na kufanikisha jukumu lao.

  Ni kwa sababu hiyo hata wewe una mchango wako unapotukosoa na kuonesha makosa ya hoja zetu na haki yako hiyo si ya kupuuza na ni mchango mkubwa vile vile. Kwa hiyo usidharau nguvu ya kila unachofanya ati kwa vile huna kiwanda au hutoi ajira!
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nadharia ziko tayari tanzania..hatuzihitaji kwa sasa kwenye siasa zetu...tunahitaji watu wanaweza kufanya na matokeo yakaonekana si maandishi, malalamiko blah blah watu wa aina yako wakipewa nchi, tutaishia kuwa na makongamano na warsha zisizo na mwisho kuelezea nadharia zako...watu wanadharia waende zao huko huko vyuoni tutawalipa vizuri e.g. maprofesa, walimu nk..hao ni less 3%

  Mtume Muhammad alianzisha kanuni za uzalishaji mali, viwanda na wakati wa uongozi jamii yake (waislamu) walihimizwa kuzalisha mali na kusimamia uadilifu...siyo nadharia nadharia no practice...get your record right!

  Sikatai hoja zako lakini naona ni zenye kupoteza watu wasijue "real" and serious problem in our politics, wananchi hawataki kushika uchumi wao...na hapa hatuhitaji siasa tunatakiwa kutengeneza waajiri, wenye viwanda wetu kuliko kuongea, kuandika, nadharia blah blah ..nendeni mkafundishe chuo kikuu msubiri mishahara.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Sawa;
  sawa;

  sawa
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Tumaini umenichekesha sana mtu wangu,

  Ulichofanya kwenye post hii na sisi kupata ujumbe ni UMEANDIKA!!

  Ok, lets go back to the point yako,

  But before that, je una viwanda na umeajiri watu kiasi cha kutoa comment kama hiyo?? sio lazima ujibu

  Lets put in this way, unafikiri wana JF hawana kazi zao mpaka wanakuja humu na kunadika maoni yao kwenye vyombo mbalimbali vya habari? au unataka woote tuwe waajiri?? Hivi unafikiri MKJJ hana kazi yake inayompa kula? naona huku haukufikiria maana hiyo insult siyo ya MKJJ peke yake

  Unachomaanisha ni kuwa kisiwe na waandishi, watu wasiandike habari, hata huyo mwajiri anayetaka kuajiri watu asitoe barua za ajira kwani atakuwa anapoteza muda.

  If you care very much what other people think, you will find that you are not one of the ones doing the thinking--- huna cha kufanya kwa nchi hii ndio maana haufikiri

  Tuendelee,

  Pinda anasema hawezi kukamata mafisadi, hawezi, kasema wote , tumesikia, mawaziri , wabunge, rais wako hana cha kufanya juu ya mafisadi.Nakala za MJJ nyingi zinalenga kujenga misingi ambayo hatuna, kuwajibika, uzembe, na kuangalia future. raia wa kawaida unataka tukae kimya tu, hivyo viwanda unavyosema tutatoa kodi, je kodi zitatumika ipasavyo? hivyo viwanda tunataka tupate umeme ili kuwe na uzalishaji , je umeme upo Tanzania?

  Kwa nini haumpi moyo kile ambacho mtanzania mwenzako anakifanya kwa faida ya jamii yetu?

  Lets say MKJJ hajajaaliwa akili kama yako, wewe unayewaza juu sana;

  "I am only one, but still I am one. I cannot do everything, but still I can do something. And because I cannot do everything I will not refuse to do the something that I can do."
  – Hellen Keller

  Natamani MKJJ akujibu hayo maneno ya Hellen Keller!

  wangapi wanaandika nakala, hao wasioandika nakala wameajiri watu? nani ambaye kwako wewe unatmuona wa maana anayetoka kazini CRDB na kurudi anaishia kuangalia game la man. na barca? au anayeikosoa seriali katika uwazi na vithibitisho tunavyoviona?

  Lets move you to another dimension labda utanielewa;

  Unajua division of labour?? unajua binadamu wana uwezo tofauti wa kufanya mambo tofauti? why on earth would you propose everyone should run industry??

  Unataka Juma nature,masanja wote wawe na viwanda, nani atatuchekesha?huo mfano tu.Mimi kama researcher/lecturer, nita instruct wanafunzi, nitafanya utafiti, nitafanya publications! for God sake what is the use of publications? , sitaki kuamini kuwa haujui! yale ni maandishi

  Maandishi yanaleta mawazo mapya, yanafariji, maandishi yanaamsha hisia za mapinduzi, maandishi yanarithisha vizazi vijavyo, historia, maandishi yanaleta mwanga mpya, maandishi yanaonya, yanakosoa, yanabadilisha watu, maandishi yanabaki kama shahidi aliye kimya, silaha ya ajabu inakutazama kila wakati,maandishi yanakumbusha......

  maandishi ndiyo yanayofanya Quran ijulikane vizazi na vizazi tena wewe kwa imani yako mna mpaka Hadith!

  Ukienda kwenye biblia kuna maandiko mengi, moja lina sema 'usiue' hili limeandikwa halibadiliki, ukilala na kuamka lipo pale pale

  Tuna viongozi wazembe na wasiofuata wala kusikia maoni ya watu na hao ndio wamekuroga wewe ujue na kuamini hakuna umuhimu wa kuandika. unataka actions tu without direction and proper foundations

  "Think like a man of action, and act like a man of thought."
  - Henri L. Bergson

  Tunawakosa watu wanao act like a man of thought! hivyo tunataka wafikiri kwanza kabla ya kufanya hili wawaze kama 'man of action' na njia pekee ni kuandika!

  Nadhani umenielewa, tunataka mabadiliko, nataka kubadilishwa , angalia ndugu zetu wanaowachagua mafisadi hali wakijua ni mafisadi, angalia akina EL, RA, Karamagi,Nkono, wanavyopeta na kutandikiwa mazuri mekundu, tatizo ni sisi.MKJJ siyo mara zote anaikosoa serikali wakati mwingine anatuamsha sote, mtu akifufuka leo na kusikia JK alipata ushindi wa asilimia 80 yet tunamwita hafai, atatuangalia na kutucheka na kusema, mbonanyie ndiyo wenye matatizo?? nani wa kutueleza haya

  Usichoke na maandiko na ushauri;

  haya kwa pamoja tumpe moyo mwanakijiji na wengine wote wanaolijenga taifa kwa uwezo na nafasi zao; kuwa

  "So many of our dreams at first seems impossible, then they seem improbable, and then, when we summon the will, they soon become inevitable."- Christopher Reeve.

  Ni kweli yanayoandikwa mengi hayafanyiwi kazi, but we believe one day, someone will put them into actions, and they will all be inevitabe

  msiwakatishe tamaa watu jamani, wakikaa kimya hwana cha kupoteza

  samahani kwa kuandika, naona is the only way to reach you!

  By the way, ondoka JF maana wote humu tunatoa maoni si kwa njia ya simu bali kwa kuandika, nashangaa umejiandikisha na kujipa jina Tumaini!!!
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Alinyimwa ulaji nini? maana anavyowalipua waungwana!!! Siamini kama ni mwana CCM
   
 20. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Ahsante sana Waberoya,huyo hajui kama hata Sir isaac Newton aliandika"In every action there is equal and opposite reaction".watu waliifanyia kazi mpaka leo tunapanda ndege,wakina Archmedes principle waliandika tu,leo tunapanda meli.Ofcoz hakuna kitu kilicho na nguvu kuliko maneno,hata mungu aliumba ulimwengu kwa maneno(hakubeba tofali).Hata vita havipiganwi bila maneno,mwanajeshi hawezi kupigana tu,kama ingekuwa hivyo tungemvamia Amin bila maneno ya Mwalimu.Na ndo maana kuna wanafalsafa mara nyingi hawawi wafalme.
   
Loading...