Hekima ya kupambana na paka (nyau): nashauri itumike zaidi

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
181
261
Habarini,

Kuna hekima ya Kiafrika ya namna ya kumdhibiti paka na kumpiga akiwa kakosea, awe ni paka wako au wa jirani.

Wazee wa Kiafrika wanashauri kuwa ukifanikiwa kumdhibiti paka ndani ya chumba na mkononi una kiboko mujarabu kwa ajili ya kumpa kichapo na mlango na madirisha yamefungwa ipasavyo, wanashauri kabla hujaanza kumpiga hakikisha unaweka uwazi kidogo au nafasi ya kupenya na kukimbia akizidiwa na kichapo. Usipofanya hivyo akizidiwa na kichapo na kuanza kuona dalili za kifo atakugeukia kwa mbinu zozote na nguvu zake zote na hakika hatokuacha salama, atakumaliza au wewe ndio utatafuta pakutokea ujiponye.

Bana sana ila hakikisha unaweka mianya usizibe kila mwanya

Asante
 
Kama ni mwanaume wa mjini lazima uweke upenyo ila kwa anayekula dona kwa samaki wa mchuzi.

👉🏾 Nina mfano halisi.
 
Isije kuwa wewe hata panya pekee anakutoa mbio🏃🐀🐀😂
HAPANA, kwanza panya ananiogopa, alafu nikufundishe kitu, kwanza nyau anamuogopa binadamu as God say "...wakatawale ... , na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Sasa kwa hofu ipi labda, yaani umepewa mamlaka alafu mwanamme unakuja kulia hapa 😥!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom