Uchaguzi 2020 Hekima na Busara za John Madale Shibuda: Kongamano la maombi na maridhiano ya amani leo Mjini Dodoma

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
12,078
12,756
Kongamano la Maombi,Dua Na MARIDHIANO ya Amani Kuelekea Uchaguzi Wa Oktoba 2020.

Hakika Alichokihubiri Mzee John Magalle Shibuda Akiwakilisha Vyama 19 vya siasa nchini,kitabaki kuwa Ni MANENO YA DHAHABU Leo,Kesho na Milele. Shibuda Anabaki Ni Alama Ya Kutukumbusha kuwa TAIFA Hili litabaki hata baada ya UCHAGUZI ujao na zile za miaka Ijayo.

Ulimi FASWAHA wa Shibuda, Ukihanikiza Sauti Tamu Yenye Utajiri Wa Kujipenyeza Mioyoni mwa wamsikilizao,ilitukumbusha kuwa SIASA Ni njia na lengo la kutufikisha kupata WAWAKILISHI wetu Uongozini ambao WATATENDA kwa niaba yetu,WATATENDA Kwa Kodi Zetu Ili kuileta nchi pamoja na kutupeleka kule Tutakako kwa FAIDA yetu na vizazi vyetu vijavyo bila kubaguliwa KIDINI, KIKABILA, KIRANGI, KIKANDA na FAMILIA WATOKAZO.

Msikilize Mzee Shibuda Akisema kuwa Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa;huwezi kuyatatua Matatizo kwa kujitia kuwa HAYAPO.

Shibuda aliendelea kusema ya kwamba;
<
WANASIASA Waache kuwa CHANZO Cha kumwaga petroli katika Moto.

< Huwezi Kuweka Miiba Nje Ya Nyumba Na Njiani Kwako Ukategemea Utakwenda na Kurudi Kwa Amani.

< WANASIASA Waangalie Wasijikwae Mwili Badala ya kidole.

< Japo kuwa Siasa Ni kupigana Vijembe ila Waangalie WASIACHE kutumia lugha za Staha zenye Kurindimisha AMANI TELE.

< TAMISEMI iache ilichokifanya katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa.

< MaDC na maRC Waache Kujipendekeza Kwa Mpendwa Rais Wetu Magufuli na kuacha Ukweli unaojulikana.

< Werevu hutembea na Hoja zenye HEKIMA NA BUSARA.

< Amemsifu Rais kwa mapambano dhidi ya CORONA na KUKUKUMBUSHA kuwa,UKIPENDA KUSIFIWA VYAKO VIZURI BASI UWE NA HULKA YA KUSIFU VIZURI VYA WENZAKO.

< WANASIASA mkashindanishe utamu wa HOJA na Nyinyi Serikali mkae mkijua kuwa WANASIASA NA SIASA Ina VIONJO VYAKE kwani mwalimu HAWEZI kuvijua VIONJO vya DAKTARI.

< Vyama Vingi vilianzishwa na CCM kwa hiyo Mmakonde Asiogope kinyago chake.

< TAMISEMI isisahau kuyafanyia kazi YALIYOJIRI KATIKA KAMATI ZA MARIDHIANO YA KISIASA NA KIDINI.

< Rais Wetu Anapenda Ukweli na Hapendi Maneno Ya KUFUBAZA Kwani SI DAWA YA UKIMWI.

John Magalle Shibuda alimalizia kwa KUKUKUMBUSHA kuwa UNAFIKI hula THAWABU,na Uchaguzi Ni KAA LA MOTO,twendeni kwenye Uchaguzi tukitanguliza AMANI, HAKI, UPENDO, MARIDHIANO, MSHIKAMANO NA UMOJA WETU kwa Maana Mwalimu Nyerere HATUKO NAYE KIMWILI ila bado anaishi kwa MANENO NA VITENDO VYAKE tunduizi kwa FAIDA Pana ya nchi hii zaidi ya FAIDA za vyama na LEGACIES ZA KISIASA za watu wachache.

Mwenyezi Mungu Ambariki mzee wetu John Magalle Shibuda aaamin aaaamin.

Na Pia ninamuomba Mwenyezi Mungu Ayaweke Maneno Haya yaliyo DHAHABU kutoka kinywani mwa Shibuda, Tuyasome na Tuyaelewe Sisi Tuliopo Sasa, na Ukifika muda huko mbeleni wayasome Wanangu na Wanetu Walio Wadogo pale Watakapokuwa VIJANA wakubwa Kama Sisi,aaaamin aaaamin.

Tanzania Kwanza,
Maridhiano Kwanza,
Amani Na Haki Kwanza,
Siempre Siempre TZ,
Hasta la Victoria TZ.

Jumbe Brown
Kijana Muuza Al Kasus
Tandale Kwa Mtogole.
24/8/2020
 
Lini kutafanyika kongamano la haki? Maana ya amani a.k.a kufanya watu makondoo tumeshayaona sana. Kwa sababu mpaka sasa kuna idadi ya kupika ya wapiga kura 29m+, lengo la yote haya ni kutoa matokeo ya kupika.

Hiyo amani ni kuzuga watu. Amani hupatikani kwa kutenda haki tu. Hilo kongamano la amani ni kichaka cha kulia fedha za umma, na kufunika hujuma iliyopangwa kufanyika kwenye uchaguzi huu.
 
Lini kutafanyika kongamano la haki? Maana ya amani a.k.a kufanya watu makondoo tumeshayaona sana. Kwa sababu mpaka sasa kuna idadi ya kupika ya wapiga kura 29m+, lengo la yote haya ni kutoa matokeo ya kupika...

Mkuu Tindo Kama Umemsikiliza vyema John Madale Shibuda Ameongelea AMANI NA HAKI....

Kama nilivyotanabahisha ya kwamba alichokisema na nilichokiandika Kitabaki kuwa Ni Cha kutekelezwa na asiye sikia LEO na kutenda Basi yatakuja kutendwa na WANETU watakapokuwa WAKUBWA Kwani UKWELI HAUFI...
 
Nimemsikiliza Shibuda!

Ameongea kutoegemea kokote lamini maudhui yake yalikua kuwaasa wenye makali(Serikali) kuacha kunyanyasa wasio na makali(Vyama vya upinzani) na Alisema sio kila neno ni uchochezi na kama ni uchochezi basi hata ccm hufanya uchochezi mwingi sana...akatolea mfano wa wimbo wa John Komba.."...wapinzani! Tuwashike,tuwakatekate tuwachinje"...

Ukitafsiri hii kisheria ni uchochezi lkn ni lugha ya siasa na hivyo hakuna haja ya kuwaonea wanaotumia maneno mengine ya vijembe na lugha ya siasa. Lakini pia alisisitiza HAKI ili kupata amani.

NB; Umeandika kwa kunyofoa baadhi ya maneno labda kwa lengo la kuonyesha alikua anawaambia Wapinzani.
 
Nimemsikiliza Shibuda!

Ameongea kutoegemea kokote lamini maudhui yake yalikua kuwaasa wenye makali(Serikali) kuacha kunyanyasa wasio na makali(Vyama vya upinzani) na Alisema sio kila neno ni uchochezi na kama ni uchochezi basi hata ccm hufanya uchochezi mwingi sana...akatolea mfano wa wimbo wa John Komba.."
Hakika Mkuu Ametambaa Vyema kuwaasa WANASIASA wote.

Mkuu Sijanyofoa Kuwananga wapinzani as Sikunukuu kila alilolisema na Kama watu wanataka KUMSIKIA watafute ALICHONENA kwa UPANA wake.

Ahsante Mkuu Wangu
 
Hana tofauti na Benson Bana, ni njaa tu akipata atanyamaza kama Bana.
Mkuu Wangu Daaah Mbona Umekuwa JUDGEMENTAL badala ya kujikita katika Kile kilichotoka kinywani mwake?!!!

Hiyo mizani Bora ya kuwapima WATU unayo mikononi mwako?!!😁😁😁

Amani Mkuu Wangu.
 
Yule shibuda wa pingamiz lililobuma au mwingine halafu andika jina lake vizuri sio madale in magale madale mnaijua wanalumumba na diamond yule wa mitama
 
Kaongea vizuri, ila hili la kusema Multiparty democracy limeletwa na CCM ni siasa ya kip.mbavu. .. kwa wakati wote ...
 
Lini kutafanyika kongamano la haki? Maana ya amani a.k.a kufanya watu makondoo tumeshayaona sana. Kwa sababu mpaka sasa kuna idadi ya kupika ya wapiga kura 29m+, lengo la yote haya ni kutoa matokeo ya kupika..
Umenena vema ndugu
 
Mkuu Tindo Kama Umemsikiliza vyema John Madale Shibuda Ameongelea AMANI NA HAKI...

Tumesharuka hatua ya kufumbafumba, huku kufumba fumba ndio kunatufanya haki isipatikane. Alipaswa kusema kuwa chaguzi zote za marudio zilinajisiwa, na uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo haki iliporwa kabisa.

Asitake kuchanganya maneno mengi wakati tatizo liko wazi kuwa Magufuli ndio tatizo. Na kwa aina ya tabia za Magufuli ili aweze kubadilika, anapaswa kuambiwa ukweli bila kufichwa fichwa. Sasa kama idadi ya wapiga kura ni ya kupika, anaonengea mafumbo ili iwe nini?
 
Back
Top Bottom