Hekima: Kuna Hatari Kubwa Kuongozwa na Watu Wenye Akili Ndogo

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Kwa kawaida binadamu hupambana na changamoto zinazomkabili kwa kutumia kile alicho nacho.

Kiongozi mwenye akili ndogo, hata siku moja hawezi kutumia akili kupambana na hoja za wapinzani wake. Kwa vile atakuwa na nguvu za mamlaka, atatumia nguvu za dola.

Ukiona utawala unatumia sana nguvu za dola kwenye ngazi mbalimbali, ujue kuwa utawala huo umejaza watu wenye akili ndogo. DC, RC, RPC, Waziri, mwenye akili ndogo, mara nyingi atapenda kutumia polisi hata kwa matukio yasiyohitaji polisi.

Kwenye ngazi ya Taifa, kiongozi akiwa na akili kidogo, atajitahidi kutumia polisi, TIS, magereza, mahakama, na hata kuwabambikia kesi wote wenye kumpa changamoto ili kuzima hoja zao, ambazo anashindwa kuzikabili kwa hoja na weledi.

Ukiona matumizi ya vyombo vya dola yanakuwa kwa kiwango cha hali ya juu katika kukabili hoja, ujue kuwa nafasi nyingi za maamuzi zimeshikwa na watu wenye akili ndogo.

WITO: Tunapochagua viongozi, tuhakikishe tunachagua watu wenye akili kubwa. Hao watajibu hoja kwa hoja maana kuijibu au kuishinda hoja kunahitaji akili na siyo nguvu. Mwenye akili ndogo hawezi kutumia asichokuwa nacho, atatumia nguvu kwa sababu ana mamlaka na vyombo vya mabavu, kama vile polisi.

Unapomchagua mtu mwenye akili ndogo, ujue unakaribisha maafa kwa Taifa. Tuwapige vita viongozi wote wenye akili kidogo, na uthibitisho kuwa kiongozi ana akili kidogo, angalia huyo kiongozi anapenda kwa kiwango gani kutumia vyombo vya mabavu.

Ni rahisi sana kiongozi mwenye akili kidogo kutoa amri ya kuua au mtu fulani afungwe hata kama hana hatia, kuliko kwa kiongozi ambaye ni super intelligent.
 
Shida yetu kama taifa, ujanja ujanja, ulioambatana na uvivu wa kutumia, akili, weledi na wakati mwingine nguvu za asili za mwili na sii Dola au nguvu nyinginezo, taifa limelemaa na matokeo yake linatamani mambo yafanyike kupitia miujiza na njia nyingine za mkato bila kujali no wapi na ninini hakiko sawa na kinahitaji marekebisho Gani.
 
Ujinga tu ,Urais ni taasisi ,hakosei yeye binafsi bali taasisi nzima ndio inakuwa mbovu
Ifahamike kuwa taasisi nzima inaweza kuundwa na low minds. Low minds watamshauri Rais kutumia zaidi vyombo vya mabavu maana ndivyo wanaona walivyo navyo, kuliko akili ambayo kwao inakuwa ni kitu adimu.

Mfano mdogo, ebu fikiria, eneo lilitengwa kwaajili ya barabara ni mita 65. Mnaamua kujenga barabara ya njia mbili, mnatumia mita 30 mnajenga katikati, mnaacha kila upande mita 17.5. Halafu baadaye mnaamua kujenga barabara ya njia 4, mnaifumua ile ya mwanzo ambayo ipo katikati ili mmege sehemu mojawapo mpate mita 30 kila upande na mita 5 katikati za kutenganisha!

Kwa nini toka mwanzo msingekuwa mjenga upande mmoja, mnapotaka kuipanua iwe ya njia 4, mnaruka tu mita 5 katikati, na kisha kujenga njia mbili za nyongeza upande wa pili?

Hivi hiyo inahitaji akili ya kusomea? Ukiona tu mambo kama hayo, unajua ni brains za namna gani zipo huko kwenye ngazi za maamuzi.
 
Kabla ya kuendelea na mjadala Tafsiri kwanza maana ya Akili.
Hapa akili imetumika kumaanisha kiwango cha intelligence au IQ. Intelligence ndiyo inakupa uwezo wa kufundishika kiurahisi, kuchota maarifa, na ukishayapata maarifa, inakusaidia kuweza kutambua namna bora ya kuyatumia hayo maarifa kwa njia sahihi katika kupambana na yote yanayokuzunguka.
 
Hapa akili imetumika kumaanisha kiwango cha intelligence au IQ. Intelligence ndiyo inakupa uwezo wa kufundishika kiurahisi, kuchota maarifa, na ukishayapata maarifa, inakusaidia kuweza kutambua namna bora ya kuyatumia hayo maarifa kwa njia sahihi katika kupambana na yote yanayokuzunguka.
Kama nimekuelewa unasema viongozi kabla ya kupewa nafasi lazima wapate IQ test?.
 
Kwa kawaida binadamu hupambana na changamoto zinazomkabili kwa kutumia kile alicho nacho.

Kiongozi mwenye akili ndogo, hata siku moja hawezi kutumia akili kupambana na hoja za wapinzani wake. Kwa vile atakuwa na nguvu za mamlaka, atatumia nguvu za dola...
Na wapinzani wake kam wamechanganyikiwa na na kukosa hoja bali wanataka kuafanya fujo atumie nini kuadhibiti hao wenye misongo ya mawazo.

Apigane nao au atumie dola kuwafundisha adabu?
 
Na wapinzani wake kam wamechanganyikiwa na na kukosa hoja bali wanataka kuafanya fujo atumie nini kuadhibiti hao wenye misongo ya mawazo.
Apigane nao au atumie dola kuwafundisha adabu?
Kama ni fujo za maneno au ni fujo za kisiasa, zinakabiliwa kwa hoja za kisiasa.

Siku zote nguvu ya kiongozi na nguvu ya chama, ni hoja zenye ushawishi. Kama kuna aliye na msongo wa kimawazo, na hoja zake ni za kimsongo wa mawazo, atakosa ushawishi kwa umma, atakufa mwenyewe kisiasa.

Lakini kwa sasa wenye msongo wa kimawazo utawatambua wanatumia nini kujibu hoja, wanatumia hoja au nguvu. Ukiona wanatumia nguvu, utambue kuwa hao ndio viongozi wenye akili kibaba, na hao hawatufai, ni hatari kwa Taifa letu.
 
Kama nimekuelewa unasema viongozi kabla ya kupewa nafasi lazima wapate IQ test?.
Tuwe na taasisi huru ya kututhibitishia kuwa mgombea wa nafasi ya uongozi amethibitika kuwa na intelligence inayoruhusiwa kuwa kiongozi.

Wenzetu kule US, kulipokuwa na mashaka juu ya afya ya akili ya Trump, alipelekwa kupimwa, akathibitika yu mzima.

Hapa kwetu ambapo inaonekana wazi kuwa low minds wengi wanautaka uongozi, basi muhimu kuwe na chombo kinachotoa uthibitisho kuwa anayeutaka uongozi ana IQ above average.
 
Back
Top Bottom