Hekaya za Abunwasi....zinakutufunza nini wa-TZ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hekaya za Abunwasi....zinakutufunza nini wa-TZ?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mpasuajipu, Feb 21, 2011.

 1. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Katika mwaka mmoja, Abunuwasi aliamua kuwa mfugaji mbuzi. Alinunua mbuzi na akanza kufuga na huku akiwa na tamaa ya kumuongezea kipato chake pindi tu mbuzi huyo atapoanza kuzaa watoto, naye atawafuga hadi wawe wengi na kuwa tajiri mji mzima kwa mbuzi wake hao.
  Siku moja Abunuasi akipokuwa anampeleka malishoni mbuzi wake njiani alikikuta kiatu kimoja kizuri sana kati kati ya njia. Alisimama na akakingalia na kilimpendeza na alisema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu" alitafuta kiatu chengine pembezoni mwa ile njia hakukiona. Akaona hakina maana kukichukua kwani hawezi kuvaa kiatu kimoja.
  Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na akakiwacha kile kiatu pale pale. Aliposonga mbele kidogo akakikuta kiatu chengine kama kile ambacho kilikuwa ni cha mguu mwengine wa kile cha mwanzo. Abunuasi alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo na kwa sasa vingelikuwa tayari vishatimia pea moja. Ndipo alipoamua kumfunga mbuzi wake pembeni ya njia na akakiweka kiatu kile pale pale alipomfunga mbuzi ili arudi akakichukuwe kiatu kile cha mwanzo.
  Aliporudi pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukikuta tena kiatu kile, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akaona kuwa ametokea mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake. Nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Ikawa amemkosa mbuzi na pia viatu hakuvikuta, Abunuasi ndoto zake zote za utajiri ziliruka na akabaki na umasikini wake kwa ubaya wa tamaa zake.

  Hapo nilipiga mstari: Mafisadi inabidi tuwadhibiti sasa, la sivyo tukisema tutawarudia baadaye tutakosa kila kitu!
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hivi vitabu vizuri sana!
   
 3. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  "Zinakutufunza" ndo kitu gani? Au ni moja Kati ya misamiati mipya iliyoundwa karibuni pamoja na mkukuta, mkurabita, umitashumta, nk?
   
 4. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  i like it
   
 5. ZeMangi

  ZeMangi JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi abunuwasi alikuwa raia wa wapi?
   
 6. f

  filonos JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  ABUNUWASI alikua RAIA wa MESEPOTANIA...ambayo vijana waleo hawataijua kamwe kwani sasa inajulika kama IRAQ Kwa zamani kabla ya BC..dunia ilikua ina ma bara ma tatu 3..tu ndio yalikua yanajulikana nayo ni UYUNANI ..greec...UAJEMI...iran..na METHEPOTANIA ...IRAQ
   
 7. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  kama unanyingine mwaga kaka...
   
 8. ngulinho

  ngulinho JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah! hii kali
   
 9. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mi sikumbuki nchi yake ila najua alizaliwa maeneo ya Msoga pale Chalinze.
   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  huu uzi umejirudia!

   
Loading...