Heka heka za CHADEMA za ahirisha mbio za Mwenge Mkoani Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heka heka za CHADEMA za ahirisha mbio za Mwenge Mkoani Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SG8, May 13, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Katika hali isiyo tarajiwa zoezi la kuwashwa mwenge lililokuwa lifanyike Mkoani Mbeya tarehe 29.05 limeahirshwa na na kuhamishiwa mkoani Mara hapo Oktoba 14. Sababu zilizotajwa ni kuwa zoezi hilo lifanyike sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa na kuzimwa Desemba 9 siku ambayo Tanzania itaadhimisha miaka 50 ya uhuru. Kwa hali hiii ni wazi kuwa tofauti na ilivyozoeleka, mwaka huu mwenge hautazunguka nchi nzima kwani muda ni mfupi miezi mitatu tu na sehemu kubwa ya nchi kuwa katika hali ya mvua.

  Lakini nyuma ya pazia sababu zinazotajwa kuahirisha zoezi hilo mkoani Mbeya ni hizi hapa
  1. Hali ya sasa kisiasa na kiuchumi: Hapa inatajwa nguvu kubwa ya Chadema mkoani Mbeya na Tanzania kiujumla. Kuna dalili kuwa kama CCM na serikali wangeng'ang'ania kuwashia mwenge jijini Mbeya ni wazi kuwa kingetokea kitu cha ajabu ambacho hakijapata kutokea. hasa ukizingatia anayewasha mwenge ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inaelezwa kuwa ama kingetokea kilichotokea pale Uyole au watu wasingejitokeza. Kwa hiyo kiusalama haikuwa mufaka kuwasha mwenge Jijini Mbeya.
  Kiuchumi ni juzi akiwa huko Vwawa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe alifyatua bomu ambalo limeitikisa sana serikali. Kwamba serikali inakopa hata mishahara ya watumishi. Hilo halina ubishi na kwa kuwa zoezi la kuwasha tu mwenge lingegharimu zaidi ya shilingi Mil 400 na mzunguko wa nchi nzima ungegharimu zaidi ya Bil. 2 ni wazi kwamba serikali isingeweza kumudu gharama hizo.
  2. Mtoa habari wetu toka jikoni ameitaja sababau kubwa kuwa ni ILANI YA CHADEMA KUPINGA MBIO ZA MWENGE. Katika hili amenukuliwa akisema "Unafikiri Chadema wabaya? CCM na serikali sasa wanatekeleza ilani ya Chadema". Alipododoswa zaidi akasema Si unajua Chadema kupitia kwa mgombea wao Dr. W. Slaa walisema mbio za mwenge ni ufujaji wa fedha za umma? Wakasema wao watauweka kwenye jumba la makumbusho? Alipoulizwa utaratibu sas upoje akajibu "ndio imetoka hiyo hakuna kukimbiza mwenge nchi nzima labda itachaguliwa mikoa michache au mkoa mmoja tu.

  Hali halisi ndio hiyo na katika hili binafsi nampongeza JK kwani kila mara amekuwa akitekeleza sera za mbwa wa tajiri (Chadema). Alianza na katiba, amewavua wenzake magamba (na yeye pia ni gamba), akasitisha zoezi la hati ya dharura bungeni kuhusu katiba na hatimaye anaelekea kufuta mbio za mwenge ambazo zilikuwa zinakinufaisha CCM. Bravo CDM
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nguvu ya umma sio mchezo, kwanza huu mwenge nao ni gamba, waurudishi mlima kilimanjaro
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I hate mwenge mwenge

  Hii ni anasa kwa serikali

  haina maana yoyote kwa taifa
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Afadhali maambukizi ya ukimwi yatapungua mwaka huu
   
 5. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,199
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ni kweli. Kumbe mambo mengine yanaweza kuepukwa tu
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Ikumbukwe SUGU ameshawaambia wananchi wa Mbeya wakiwaona mafisadi wawazomee na ikibidi wawapige mawe(naunga mkono).Ni hatari kwa viongozi wa CCM kuenda sehemu ambayo wameshatangaziwa hali ya hatari.
  Hata hivyo kama wanahamia Mara bado nina mashaka na usalama wao.Ningeshauri wakafanyie zoezi hili nchi jirani.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mkuu...vijijini mtoto wa kike wanalindwa mbaya kabisa lakini inapofika siku kama ya mwenge wanajisahau wanawaruhusu kwenda kukesha....ndiyo siku ya kuwapata watoto wakike siku hiyo
   
 8. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Mwenge siupendi kbs nnakumbuka shule ya msingi tulikuwa tukichangishwa sn hela za mwenge,bora wauchome moto kbs kwanza mimi sioni maana yake zaidi ya kuteketeza pesa zetu(Watanzania)walipakodi
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  tarime kwetu wasijaribu na hivi awampendi mbunge wao ambaye amekimbilia dar badala ya kuwa tarime na kuangalia wananchi wanataka nini
   
 10. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Afadhali umepelekwa huko Mara mie ningeuona huku kwetu ningeupiga mawe.
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mwenge ni masuala ya kiimani zaidi
   
 12. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hahaha na bado.. gamba la mwenge linaelekea kuvuliwa.. JK anaogopa kupigwa mawe tena asithubutu kabisa kukanyaga Mbeya atakiona cha mtema kuni full kumzomea... Mbeya, Mwanza,Kilimanjaro, Mara, Shinyanga, Arusha, Iringa, Mpanda, Songea, ni ngome zetu CCM hawana chao... Baada ya operesheni ya sasa tutapata ngome zaidi mikoa ya Rukwa, Kagera,Singida, Tabora, naamini this trend itatupelekea kushika nusu ya nchi mwaka huu... then next move should be Tanga, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, at last Dsm - this will be difficult battle kwani ni ngome muhimu kwa CCM & CCM B
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwenge mzuri jamani. Huwa natajirika sana ukija hapa Sikonge maana uuzaji wa Kondom huwa ni wa hali ya juu sana.

  Pato la siku moja, huwa ni sawa na pato la miaka miwili. Mwenge Oyeeee.....

  Nausubiri SIKONGE. KARIBUNI SANA.
   
 14. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  RED ALERT:
  Sio ngumu mwanaharakati,unapopambana usiangalie kushindwa,angalia zaidi kushinda.Usikate tamaa kabla hujajaribu.
  Mashindano yoyote lazima kuna kushnda na kushindwa,CHADEMA mpaka sasa hivi ukiona hivi imekaribia kushinda.
   
 15. Mpiga Nyoka

  Mpiga Nyoka JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  waende kwa m7 au vipi mzee ?
   
 16. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mlima Kilimanjaro walishaukataa kitambo. Kumbuka vuguvugu la mageuzi lilikoanzia!
   
 17. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ,,,,,Shame on them,tena juzi wamekuja kwangu na KUGONGA ati kila nyumba itoe MCHANGO kwa ajili mafuta ya taa,,,,,hii mijitu hii bana daaah!!!!
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  wameogopa kupigwa mawe mbeya... sijui cdm tutangulie musoma?
   
 19. D

  Dwork1 Member

  #19
  May 13, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  na bora hawaja washia mby kwasababu wiki iliyo pita walianza kuwa nyanyasa wafanya biashara kisa hela ya mwenge na kwa upande wangu sija wahijua manufaa ya mwenge zaidi ya ku chochea maambukizi ya ukimwi katika mikesha ya mwenge
   
 20. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kudadadeeki cdm inawapotezea kiundavaundava
   
Loading...