Heeee! kumbe kuuza hela (coins) nalo ni kosa la jinai! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heeee! kumbe kuuza hela (coins) nalo ni kosa la jinai!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by white wizard, Sep 5, 2011.

 1. w

  white wizard JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Leo ktk pitapita yangu mitaa ya posta mpya jijini DSM nimekutana na ki2u, ambacho kidogo kimenishangaza, kuna vijana wawili walikamatwa na polisi kwa kosa la kujishughulisha na uuzaji wa chenchi za sarafu kwa makondakta wa daladala Unatoa 1000, wanakupa 900, maisha yanakwenda.

  Na hii biashara mbona imekuwepo miaka mingi sana, walikuwa hawawaoni? Au kwa vile majuzi nilimsikia afisa mmoja toka BOT, anazungumzia eti hii biashara ya sarafu nayo inaathiri uchumi!. Labda kwa wanauchumi wanaweza ku2usaidia. Wale vijana walipandishwa kwenye defender cjui hatima yao imekuwaje.

  Ila mimi nadhani ni njaa tu zinazosumbua hawa maaskari wetu kuna mambo mangapi ya msingi ya kushughulikia? Uzuri wa nchi hii bwana uhangaike kujitafutia riziki halali una banwa, utumie nguvu ndio balaaa, ukae tu unaonekana mzururaji, abda utaifa wako ndio utakaoweza kukusaidia.

  Mfano pale kariakoo machinga wa kitanzania akiweka bidhaa chini ni balaa kwa mgambo wa city, ila pembeni hapo kuna mchina ameweka bidhaa zake haguswi!

  'TANZANIA NI ZAIDI YA UIJUAVYO"
   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Gavana Ndullu ameshindwa kuthibiti mfumuko wa bei; ametuletea noti zenye quality hafifu na hata ameshindwa kuleta sarafu za kutosha kwenye mzunguko, na matokeo yake wananchi wanapata tabu kupata chenji!! sasa huyu bwana anaweza nini? Anapinga hata kuweka reserve zetu kwenye DHAHABU kitu ambacho kingetusaidia kuimarisha shililingi yetu!! GODDAM give me my GUN!!
   
Loading...