Hee!!!MGONJA KULIA X-MASS KEKO!!YALAAH!!

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
*Mwingine aongezwa katika orodha ya ufisadi wa EPA

Na Nora Damian


Mahakama ya Kisutu Jumatatu yalikuwa eneo la pilikapilika kwa mara nyingine baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja kupandishwa kizimbani akituhumiwa kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh11 bilioni, huku mfanyabiashara Jonathan Munisi pia akipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuiba fedha kwenye Akaunti ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA).


Munisi, ambaye alikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu (BoT) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuiba Sh2.6 bilioni kutoka kwenye akaunti hiyo iliyokuwa kwenye benki hiyo na kufanya idadi ya watuhumiwa waliopandishwa kizimbani hadi sasa kufikia 21.


Lakini macho ya wengi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu yalikuwa kwa katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Mgonja ambaye alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi yake na kuisababishia serikali hasara hiyo.


Mtendaji huyo mkuu wa serikali alilazimika kwenda kulala mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti yote ya dhamana, likiwemo la kuwasilisha fedha taslimu au mali zenye thamani ya Sh5.9, ikiwa ni nusu ya fedha anazodaiwa kuisababishia serikali hasa.


Mgonja, akionekana kufedheheka, alifikishwa mahakamani hapo saa 7:00 mchana akiwa kwenye gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba T 123ATW huku akiwa amevalia shati la rangi nyeupe na suruali ya rangi ya bluu. Alipelekwa chumba cha mahabusu hadi saa 8.28 mchana alipopandishwa kizimbani.


Wakati akiwa mahakamani hapo Mgonja alionekana kujishika tama mara kwa mara na wakati mwingine kuinama chini.


Wakili wa serikali, Fredrick Manyanda alimsomea mashtaka nane mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja. Mgonja alikana mashitaka yote.


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Desemba 18 mwaka 2003 na Novemba 15

mwaka 2005, akiwa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha, alitoa taarifa za serikali (government notice) ambayo iliipa msamaha wa kodi kampuni ya M/S Alex Stewart kinyume na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato

(TRA).


Mgonja anadaiwa kuwa Oktoba 18 na 19 mwaka 2003 alitoa taarifa ya serikali namba 423, Desemba 19 mwaka 2003 taarifa ya serikali namba 424, Oktoba 15 mwaka 2004 taarifa ya serikali namba 497, Oktoba 14 na 15 mwaka 2004 taarifa ya serikali namba 498, Novemba 15 mwaka mwaka 2005 taarifa ya serikali namba 377 na Novemba 15 mwaka 2005 taarifa ya serikali namba 378.


Mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kuwa kati ya mwaka 2003 na 2007, kwa makusudi na

kwa kutokuwa makini, alisaini taarifa hizo ambazo ziliipa unafuu kampuni hiyo kulipa kodi, kitendo ambacho inadaiwa kiliisababishia serikali hasara ya Sh11,752,350,140.


Hata hiyo, wakili huyo wa serikali alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.


Baada ya hoja za upande wa mashitaka, kiongozi wa jopo la mawakili watano wanaomtetea Mgonja, likiongozwa na Profesa Leonard Shaidi alidai kuwa mashitaka na kiwango cha pesa kilichotajwa yanafanana na ya mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona na kwamba wanashangaa kwanini hawakufikishwa mahakamani pamoja.


Akijibu hoja hizo, Wakili Manyanda wa serikali alidai kuwa upelelezi ulikuwa bado haujakamilika na kwamba wanaweza wakawaunganishwa.


Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mwankenja aliahirisha kesi hiyo kwa dakika 15 hadi saa 9.30 mchana wakati alipotoa masharti ya dhamana.


Mwankenja alitoa masharti manne ya dhamana kwa mshitakiwa huyo akimtaka kuwasilisha fedha taslimu au hati za mali zenye thamani ya Sh5.9bilioni.


Pia mshitakiwa huyo ametakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria, asitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali maalum cha mahakama, na awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh 5.9 bilioni.


Mshitakiwa huyo alitimiza sharti moja tu la kuwa na wadhamini wawili ambao walikuwa wafanyakazi wenzake, Ramadhan Mlinga na Delfina Mlaki, lakini akashindwa kutimiza masharti mengine yaliyowekwa na mahakama na hivyo Mgonja kulazimika kupelekwa rumande mpaka atakapotimiza masharti hayo.


Kesi hiyo imehairishwa Desemba 29 mwaka huu kwajili ya kutajwa tena.


Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, ulinzi uliimarishwa. Zaidi ya polisi 10 waliwasili mahakamani saa 2:00 asubuhi, wakiwa na mbwa wawili. Walitumia gari la polisi lenye namba PT 0948.


Mara baada ya kesi hiyo kumalizika mtuhumiwa huyo alisindikizwa kuelekea rumande na mbwa hao pamoja na gari ya polisi iliyokuwa imetanguliaa mbele.


Kufikishwa mahakamani kwa katibu huyo mahakamani kunafanya idiadi ya vigogo waliofikishwa mahakamni hapo kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara, kufikia watatu.


Tayari mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi na kuisababishia serikali hasara. Wapo nje kwa dhamana.


Katika anga za EPA, Munisi anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 25 mwaka 2006 mkoani Arusha.


Wakili wa serikali Boniface Stanslaus alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ady Lyamuya kuwa mtuhumiwa alijipatia fedha hizo kupitia kampuni ya Njeki Enterprises akidanganya kwamba amenunua deni kutoka kampuni ya E. Itoh ya nchini Japan.


Hata hivyo mshtakiwa alikana kosa na kutakiwa kutoa fedha taslimu Sh1.3bilioni na kuwa na wadhamini wawili kwa ajili ya dhamana yake, lakini masharti hayo yalionekana kuwa magumu kwa mtuhumiwa huyo na alipelekwa kwenda kulala mahabusu hadi Desemba 30 mwaka huu.


Watuhumiwa wa wizi kwenye akaunti ya EPA walianza kufikishwa mahamakani Oktoba mwaka huu na mfanyabiashara maarufu nchini Jeetu Patel ndiye aliyekuwa mtuhumiwa wa kwanza kupanda kuzimbani.


Jeetu na wenzake walikaa rumande kwa majuma kadhaa kabla ya kutolewa kwa dhamana ya mamilioni ya fedha ambayo awali iionekana kuwa ngumu kuipata
 
Jamani si angemlaza tu mpaka january 2..aone mwaka mpya unakuwaje akiwa keko!!!!!mhhhhhhhhhhhhhhh sijui nani atalia newyr keko!!!
Keko keko weeeeeeeeee keko mbona unatupenda hivyo hata ubagui jamani
nimeamini
kweli jela haina mwenyewe
 
Back
Top Bottom