Hebu WANAUME tukae kitako tujadili haya . . . .!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu WANAUME tukae kitako tujadili haya . . . .!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Sep 7, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Najua jukumu la mwanaume ni kuleta mambo chanya kwa familia yake na jamii inayomzunguka.Yameshasemwa mengi sana,lakini bado yatasemwa.MWANAUME anajulikana ndie KIONGOZI wa jamii katika hali zozote,hili halina ubishi,sasa kama kiongozi anakuwa wa hovyo hata kile anachokiongoza nacho kitakua hivyo hivyo.Ni ukweli ulio wazi jamii yetu leo ni ya hovyo,kama ni ya hovyo ni lazima kiongozi ndo ameruhusu hayo na kwa upande mwingine nae ni wa hovyo.Kuna mambo kama ukahaba,watoto wa mitaani na kukosekana uaminifu kwenye ndoa/mahusiano,ninaamini kama wanaume tungekua dhabiti,hata kungekua hakuna huu ujinga wa kudai haki sawa.Naita ujinga kwa sababu wanaume kwanza tangu mwanzo,mwanaume ndo alikua anahudumia familia alipochemka mwanamke ikabidi aende nae front line,mwanaume alipowaka tamaa alianza kumshawishi mwanamke kumpa mwili wake kwa malipo ndipo ukaibuka ukahaba,still mwanaume akashindwa kuridhika na mkewe akaenda kuanzisha nyumba ndogo(kuna wajinga wanasapoti hili)matokeo yake wanatelekeza familia maisha yanakua magumu watoto nao wanaingia mtaani tunapata watoto wa mtaani.Haya ni makosa makubwa yaliyofanywa na yanafanywa nasi leo,yapo mengi lakini hebu tuyajadili hayo leo.Najilaumu mimi kama sehemu ya wanaume na nawalaumu wenginepia kwa sababu inafahamika mwanaume pekee ndie alikua mtafuta riziki so ndie alikua anatoka nyumbani na kumuacha mwanamke,na mwanaume ndie alikua mtoa maamuzi kuanzia familia,mtaa hadi taifa,sasa tutakwepaje lawama?Sisi ndo tulioanzisha upuuzi mwingi kwa kuwa ndo tulikua na mamlaka.Wateja wa makahaba ni wanaume,wanaoanzisha nyumba ndogo ni wanaume,wanaowapa ujauzito wanafunzi ni wanaume,mambo ya hovyo tunayofanya ni mengi halafu tunayatetea,this is a shame.Unadhani unapoonesha mambo ya hovyo na tabia za hovyo,unadhani unaemuongoza atakuheshimu?Sidhani,ndo maana wanawake kudai haki sawa naita ujinga kwa kuwa kumetokana na udhaifu wetu wanaume.Hebu leo tusemezane tulikosea wapi ili tuparekebishe ili turudishe heshima yetu jamani!
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  definition yako ya haki sawa ni ipi?

  ukishanijibu nitakaa hapa pembeni huku nikipata:coffee: taratiiiiiiiiiiiiiiiiiibu nakutizama :fencing:unavyoendelea....
   
 3. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ukahaba, small house na mimba yote hayo ni matatizo ya wanawake sio mwanaume. hapa duniani mwanamke lazima atatogozwa tuu na yeye ndio mwenye msimamo wa mwisho kama hataki kumegwa hamegeki.
  mimba biologically ni mwanamke ana determine kama anapata au lah...kama demu hataki mimba basi mwanawane utatwanga K mpaka mwisho na hamna kitu.
  ukahaba well thats just kukosa maadili on their part.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Nina mengi ya kusapoti na kubisha.
  Ngoja kwanza mjadala uchanganye na hii komoni yangu kichwani itulie
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ngoja, nitarudi ....
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hapo sikubaliani na wewe.
   
 7. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una kila dalili ya kuwa mwanamke hivi karibuni.
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  Eiyer mdogo wangu wa ukweli mbona hata wale tu;io waamini humu jamvini kama HorsePower nae anakimbia?

  mimi naanzisha mjadala kwamba mwanaume kiini cha mabadiliko.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  nakusihi ukae pembeni kidogo ili tujadili kwanza ila swala la matusi hapa si mahala pake. jiheshimu mkuu manake unaheshimiwa na wengine.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  naomba nikuulize swali je waweza kuuza bidhaa dukani mwako kama haina mteja?

  na kama bidhaaa haina mteja inamaana gani?
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  gfsonwin sijakimbia, nimeahidi kurudi, naomba nisieleweke vinginevyo ...!:redface:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nimetamani kugonga LIKE mara mbili, lol! Kwa mara ya pili nimeona neno la busara toka kwa mwanaume.
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mume wangu hayupo huku kwenye haya mambo Eiyer
   
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kweli akili nayo inamwishoooo.una miaka mingapi ndugu yangu?????????????,unaishi wapi,?kama ulishapita pita dsm utaiweka hiyo sentensi virse versa its so personal
   
 15. data

  data JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,776
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  Kwa vile neno hovyo limetokea sana..namsubiri hovyohovyo aje tia neno nami ntaendelea
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mi mwenyewe hapa natafuata doble like siiioni!wawe wanziweka bana kwa mambo ya msingi kama haya .hapa najipanga kuja kumsapoti hivo!
   
 17. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari za kukatazana nyumba ndogo nitumie mwakani. Yaani nimteme Sara! Hiyo haipo wewe sema. Kwaheri...
   
 18. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mi naunga hoja mkono kwa asilimia mia moja. Kuna mambo mengi ambayo wanaume wa sasa hatufanyi na hivyo kuonekana MEN=WOMEN. Zama za mababu zetu kama generation 2 tu zilizopita MEN were MEN na WOMEN were WOMEN. Clear distinction ilikuwepo interms of roles and responsibilities. Kizazi hiki tulicho haswa sisi wababa wenye umri kati ya 25 hadi 65 asilimia kubwa tumepoteza kabisa ile tabia ya uanaume. Eti wanaume wa sasa utasikia kapigwa kibao na mkewe; hii ni kufuru kubwa kwa wanaume wa zamani na lilikuwa ni kosa la kuondolewa kwenye ile familia for good au kuchapwa viboko hadharani au ulipe faini ya mbuzi, ngombe na hiyo italipwa na kaka za mke.

  Imefika mahala vijana wetu wa kiume eti wanataka kuolewa na akina Sugar Mummy watumiwe just kama playboy wa kula kulaa bila kuingiza hata senti moja. tunakokwenda ni kubaya zaidi na inabidi tuwalee watoto wetu wa kiume katika mtazamo wa kuwa family and community leader na si viwanaume vya kuzabwa kelbu na wake zao huku majukumu ya msingi katika familia yakiwashinda .

  Mwanaume unatakiwa ktk nyumba uonyeshe njia na uonekane reliable na dependable, kazi za kiume kama kulipa ada, kujenga nyumba, kununua vitu muhimu vya familia ununue na kuvisimamia na si kukwepa majukumu na kumwachia mkeo. Kama huna uwezo wa kufanya majukumu ya kibaba ni bora usioe kwani hata ukioa mke atakudharau na hutashirikishwa katika maamuzi mengi ya familia na hata watoto hawataona umuhimu wako zaidi ya kukuona just as a any other family member. Na hapa ndipo heshima inapokuwa haipo na matokeo mtoto wa kiume anakuwa akijua mama ndiye kiongozi
   
 19. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Acha ya kupigwa kibao na mke, unamkuta mwanaume kajiachia anachekacheka ovyo tu hadi anaachia ushu.i tena mbele ya watoto haaa!Wanaume badilikeni bwana kwani mmesahau baba zenu walivyokuwa? Sie baba yetu alikuwa baba kweli, akirudi kila mtu anashika adabu, hadi mama tulikuwa tunamuona anavyongwaya mzee! Siku hizi wanaume wetu akirudi toka kazini watoto wanamrukia kila kona ya mwili hadi sometimes wanagusa nanihii za baba yao, looh! BADILIKENI WANAUME, NYIE NDIO CHACHU YA MABADILIKO KAIKA JAMII
   
 20. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hiyo ni hofu sio heshima. mwanaume wa leo needs empathy, a caring heart na aweze kucheza na wanawe; the rough guy from yester-year is gone. Move on au tafuta mwanaume wa kijijini.
   
Loading...