Maty
JF-Expert Member
- Aug 24, 2010
- 2,167
- 723
Jamani hapa JF watu tunakuja kupunguza stress, tumekerwa na wenzi wetu, tumekerwa na mabosi na mengine mengi. Kwa upande wangu huwa baada ya kero kama hizo naingia JF mara moja kupunguza hizo stress na nikitoka humu nimefarijika vya kutosha. Sasa kinachonishangaza utakuta watu wanaleta mastress waliyotoka nayo huko na kuyaingiza humu JF inafikia mpaka watu wanagombana humu haipendezi hata kidogo kama umeona thread na hujaipenda halafu una mahasira yako(ucjeniambia kwamba unakuwa hujijui kwamba cku hiyo umeamka vibaya) ipotezee tu nenda nyingine ambayo utaona unaipenda na sio unaanza kuudhi watu. Kuna hawa watu wawili ingawa wapo wengine wengi hawa nimeamua kuwatolea mfano tu Aspirin na Dark City hawa watu wana hekima sana hata kama kuna kitu kimewakera huwa wanajibu kwa ustaarabu sana huwa wanatumia maneno ambayo hayakeri na msg inakupata sawia mi naomba tuige mfano wa watu kama hawa ili JF iwe kweli ni home ya magreat thinkers sio mtu unatoka huko hata ufikirii unaanza kuporomosha maneno ya kukera wenzio. Nawasilisha