Hebu tuwe wakweli, hivi Wabunge wanataka kumpongeza jpm kwa mafanikio yapi?

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,069
18,347
Jana ndugai amesema wanaandaa utaratibu wa kumpongeza jpm ambao utaratibu utatolewa leo!
Hebu tuwe wakweli raisi anapongezwa kwa lipi lililofanikiwa?
Kwasababu kama tume zilianza kuundwa toka enzi za mkapa!

Halafu hatujasikia hao acacia nao wanarespond vipi!
Je, ni kweli wamekubali kulipa hizo trillion 100+?

Mimi nafikiri bado mapema mno kuanza kupongezana kwanini tusiwe na subra katika hili! Tuone mafanikio yapoje?

Binafsi nisiwe mnafiki nitampongeza mheshimiwa raisi mwishoni baada ya kuona mafanikio yanayoshikika kabisa sio haya ya kuunda tume!
 
Rais ajaye naye atataka afukue mikataba ya kuuza za serikali pamoja na kivuko cha MV Dar es Salaam, watalaumiwa Makatibu wa Idara na Manaibu waziri wa vipindi hivyo, kisha tunawaacha wahusika wakuu.

Mwizi ametubia Trilion 100, ni tahira pekee ndie atakayeamini hizi pesa zote zilalipwa, na ni mjinga pekee ndie ataona vyena kuwa Rais anapaswa kukaa chini na haohao wezi Acacia ili kuja kuwekeza tena. Huu ni unafki Mkubwa sana Rais ameuonesha, utakaaje tena na mwizi ambae amekuibia Trilion 100 halafu uongee nae aje tena kuwekeza kwako?
 
MKUU ANAPONGEZWA KWA UTHUBUTU WAKE KATIKA KUPAMBANA NA WAHUJUMU UCHUMI NA NIA YAKE THABITI KWA AJILI YA MANUFAA YA NCHI HII
Mkuu nia yake thabiti tunaiona vipi? Mbona tume za kuchunguza zimeundwa sana enzi za kikwete!
 
sawa!
Mzima wewe?
Mie ni mzima Ngushi,
Unajuwa wabunge wale wanajitahidi kujipendekeza kwa mkuu. Wanafanya kama sie wanawake tunavyojua kujipendekeza kwenu wanaume, hata ukijamba utasikia anakwambia "POLE BABY, HUJAUMIA" na hali anajua kabisa kuwa kujamba hakuumizi.
hapo ni mwendo wa kujikomba ili wapate mikate yao ya kila siku
 
Ha haaaa haaaaaaa aisee! Nimemshangaa sana ndugai
 
Rais ajaye naye atataka afukue mikataba ya kuuza za serikali pamoja na kivuko cha MV Dar es Salaam, watalaumiwa Makatibu wa Idara na Manaibu waziri wa vipindi hivyo, kisha tunawaacha wahusika wakuu.

Mwizi ametubia Trilion 100, ni tahira pekee ndie atakayeamini hizi pesa zote zilalipwa, na ni mjinga pekee ndie ataona vyena kuwa Rais anapaswa kukaa chini na haohao wezi Acacia ili kuja kuwekeza tena. Huu ni unafki Mkubwa sana Rais ameuonesha, utakaaje tena na mwizi ambae amekuibia Trilion 100 halafu uongee nae aje tena kuwekeza kwako?
ACACIA "wameidharau" ripoti ya Profesa Osoro kwamba kuwaaminisha watu kuwa wao wanachuma mapesa yote hayo "it doesn't make sense". Wamesema hata li kampuni kubwa la madini duniani BHP, halina utajiri huo licha ya kuwa na migodi katika nchi 10 duniani.
 
ACACIA "wameidharau" ripoti ya Profesa Osoro kwamba kuwaaminisha watu kuwa wao wanachuma mapesa yote hayo "it doesn't make any sense". Wamesema hata li kampuni kubwa la madini duniani BHP, halina utajiri huo licha ya kuwa na migodi katika nchi 10 duniani.
Aisee ndio maana Mimi naona Wabunge wawe na subra katika hili!
Kwani kuna ubaya gani baada ya kufanikiwa waje kumpongeza!
Hivi itakuwaje siku acacia nao wakijibu hoja za prof osoro ikaonekana nao wanahaki?
Maana mpaka sasa tunashangilia kwa goli la kuongoza ila game haijafika mwisho
 
Rais ajaye naye atataka afukue mikataba ya kuuza za serikali pamoja na kivuko cha MV Dar es Salaam, watalaumiwa Makatibu wa Idara na Manaibu waziri wa vipindi hivyo, kisha tunawaacha wahusika wakuu.

Mwizi ametubia Trilion 100, ni tahira pekee ndie atakayeamini hizi pesa zote zilalipwa, na ni mjinga pekee ndie ataona vyena kuwa Rais anapaswa kukaa chini na haohao wezi Acacia ili kuja kuwekeza tena. Huu ni unafki Mkubwa sana Rais ameuonesha, utakaaje tena na mwizi ambae amekuibia Trilion 100 halafu uongee nae aje tena kuwekeza kwako?

Hata mimi nakubaliana na wewe ila nahisi kama angesema hataki majadiliano yoyote na hawa wawekezaji bado tungesema anajishtukia kwakuwa hataki kusikiliza upande wa pili, wengine tungemuita dikteta na mtu asiyekubali kushaurika. All in all hata kama mtu amekufanyia unyama kiasi gani kumpa nafasi kumsikiliza ni fair play before you make any further movement, na wakati huohuo unapata nafasi ya kumdadisi mwelekeo wa harakati zake

Hata mimi binafsi nasubiri sana nione mwisho wa hii vita ila aisee Watz mna hasira kali
 
Aisee ndio maana Mimi naona Wabunge wawe na subra katika hili!
Kwani kuna ubaya gani baada ya kufanikiwa waje kumpongeza!
Hivi itakuwaje siku acacia nao wakijibu hoja za prof osoro ikaonekana nao wanahaki?
Maana mpaka sasa tunashangilia kwa goli la kuongoza ila game haijafika mwisho
Uzuri wa wabunge wetu wana uthubutu wa kupongeza na kushangilia magoli yote, yawe ya kufunga au kufungwa. Kwa hiyo hilo lisikutishe mzee. Wacha wale posho ya kupongeza.
 
ndio kwanza mechi hii hata half time bdo tayar hawa wabunge wetu wa LA saba B wanakurupuka,, hebu tulizeni hiyo mishono yenu mpk dkk 90 ziishe ili tujuwe tumeshinda kihalali ndio tupongezane
 
Hata mimi nakubaliana na wewe ila nahisi kama angesema hataki majadiliano yoyote na hawa wawekezaji bado tungesema anajishtukia kwakuwa hataki kusikiliza upande wa pili, wengine tungemuita dikteta na mtu asiyekubali kushaurika. All in all hata kama mtu amekufanyia unyama kiasi gani kumpa nafasi kumsikiliza ni fair play before you make any further movement, na wakati huohuo unapata nafasi ya kumdadisi mwelekeo wa harakati zake

Hata mimi binafsi nasubiri sana nione mwisho wa hii vita ila aisee Watz mna hasira kali
Nahisi hukumsikiliza Magufuli, yaani yeye kasema akae nao ili kama kuwekeza wawekeze tena. Sasa huu sio ujinga? Kulikuwa na haja gani kuisoma ile habari public na kutuaminisha kuwa tunaibiwa wakati alikuwa na uweze wa kuwaita na kuongea nao?
 
Mimi binafsi nampongeza kwa hatua alizochukua za kuzuia mchanga usisafirishwe mpaka hapo mgogoro huu utakapotatuliwa. kiukweli ktk viongozi waliopita walifanya tafiti na report ziliandikwa lkn hakuna aliyethubutu hata tu kupokea report hizo hadharani Magu atakua kiongozi wa kwanza kufanya alichokifanya baada ya Nyerere kuondoka madarakani. either way he still deserves credits for that
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom