HS CODE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 1,779
- 4,310
Ndugu zangu kuna maelfu ya watafuta ajira wenye vigezo ila wanashindwa kuhudhuria saili kwa kutomudu gharama zinazohitajika. Binafsi naamini ziko njia nyingi zinazoweza kupunguza sana ukubwa wa tatizo.
Njia ya kwanza
Kwa mfano, kama imewezekana watu kupangiwa ajira kutokana na kanzi data inayotunza taarifa za walioshindwa kupata kazi kwa sababu ya uhaba wa nafasi husika ila walifaulu usaili wa kuongea, kwa nini na waliofika kiwango rasmi kilichowekwa kama cha kuanzia ufaulu (ufaulu wa 50 kwenda juu), kwenye usaili wa kuandika na wao wasiwe na vigezo vya kuitwa moja kwa moja kwenye saili nyingine za kuongea zinazofanana na nafasi waliyoomba kabla kama wamekidhi mahitaji ya ushindani?
Ni hivi msailiwa ameomba uhasibu taasisi A, hajafika Oral kwa sababu alama ya mwisho kuchukuliwa ni 80 na yeye ana 70, endapo ameomba uhasibu taasisi B yenye vigezo sawa na A, kwanini asiingizwe kwenye ushindani na wapya watakaofanya usaili taasisi B, na kama ufaulu unamruhusu aitwe moja kwa moja kwenye oral kuliko kuanza upya written?
Njia ya pili
1. Wote wanaofikisha ufaulu wa 50 kwenda juu waitwe Oral, kisha wakapambanie huko.
Hata kama wakikosa, sio shida kama wamefaulu ila nafasi zikawa ni chache wawekwe kwenye kanzi data zikipatikana waitwe.
2. Yafanyike maboresho makubwa kwenye kanzi data, uongezwe uwazi, utaratibu udhibiti mianya ya upendeleo na watu watakaouhujumu mfumo tushuhudie wakiwajibishwa vikali.
Tuanze kulijadili hili, na tupendekeze njia nyingine zinazoweza kuepusha gharama zisizo za lazima au kupunguza zile za lazima.
Hii nenda rudi kwenye usaili tusiichukulie poa.