Hebu tuwaze namna Utumishi wanaweza wakawapunguzia gharama za usaili wanaotafuta ajira

HS CODE

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
1,579
3,573
Ndugu zangu kuna maelfu ya watafuta ajira wenye vigezo ila wanashindwa kuhudhuria saili kwa kutomudu gharama zinazohitajika. Binafsi naamini ziko njia nyingi zinazoweza kupunguza sana ukubwa wa tatizo.

Njia ya kwanza
Kwa mfano, kama imewezekana watu kupangiwa ajira kutokana na kanzi data inayotunza taarifa za walioshindwa kupata kazi kwa sababu ya uhaba wa nafasi husika ila walifaulu usaili wa kuongea, kwa nini na waliofika kiwango rasmi kilichowekwa kama cha kuanzia ufaulu (ufaulu wa 50 kwenda juu), kwenye usaili wa kuandika na wao wasiwe na vigezo vya kuitwa moja kwa moja kwenye saili nyingine za kuongea zinazofanana na nafasi waliyoomba kabla kama wamekidhi mahitaji ya ushindani?

Ni hivi msailiwa ameomba uhasibu taasisi A, hajafika Oral kwa sababu alama ya mwisho kuchukuliwa ni 80 na yeye ana 70, endapo ameomba uhasibu taasisi B yenye vigezo sawa na A, kwanini asiingizwe kwenye ushindani na wapya watakaofanya usaili taasisi B, na kama ufaulu unamruhusu aitwe moja kwa moja kwenye oral kuliko kuanza upya written?

Njia ya pili
1. Wote wanaofikisha ufaulu wa 50 kwenda juu waitwe Oral, kisha wakapambanie huko.

Hata kama wakikosa, sio shida kama wamefaulu ila nafasi zikawa ni chache wawekwe kwenye kanzi data zikipatikana waitwe.

2. Yafanyike maboresho makubwa kwenye kanzi data, uongezwe uwazi, utaratibu udhibiti mianya ya upendeleo na watu watakaouhujumu mfumo tushuhudie wakiwajibishwa vikali.

Tuanze kulijadili hili, na tupendekeze njia nyingine zinazoweza kuepusha gharama zisizo za lazima au kupunguza zile za lazima.

Hii nenda rudi kwenye usaili tusiichukulie poa.
 
wizy

JF-Expert Member
Sep 23, 2016
4,069
9,880
Ndugu zangu kuna maelfu ya watafuta ajira wenye vigezo ila wanashindwa kuhudhuria saili kwa kutomudu gharama zinazohitajika. Binafsi naamini ziko njia nyingi zisizougharimu upande wowote kati ya msaili na msailiwa na bado zinaweza kupunguza ukubwa wa tatizo.

Kwa mfano, kama imewezekana watu kupangiwa ajira kutokana na kanzi data inayotunza taarifa za walioshindwa kupata kazi kwa sababu ya uhaba wa nafasi husika ila walifaulu usaili wa kuongea, kwa nini na waliofika kiwango rasmi kilichowekwa kama cha kuanzia ufaulu (ufaulu wa 50 kwenda juu), kwenye usaili wa kuandika na wao wasiwe na vigezo vya kuitwa moja kwa moja kwenye saili nyingine za kuongea zinazofanana na nafasi waliyoomba kabla kama wamekidhi mahitaji ya ushindani?

Ni hivi msailiwa ameomba uhasibu taasisi A, hajafika Oral kwa sababu alama ya mwisho kuchukuliwa ni 80 na yeye ana 70, endapo ameomba uhasibu taasisi B yenye vigezo sawa na A, kwanini asiingizwe kwenye ushindani na wapya watakaofanya usaili taasisi B, na kama ufaulu unamruhusu aitwe moja kwa moja kwenye oral kuliko kuanza upya written?

Hii nenda rudi kwenye usaili tusiichukulie poa.

Tuanze kulijadili hili, na tutoe mengine yanayoepusha gharama zisizo za lazima au kupunguza zile za lazima.
Hizi route za dodoma zinakula sana hela
 
HS CODE

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
1,579
3,573
Hizi route za dodoma zinakula sana hela

Acha kabisa Mkuu, ni vile hakuna pakusemea watu wakasikika. Ila naamini wapo wengi wanaishia kuziangalia nafasi mpya huku hawana jinsi inabidi waziache kwa sababu ya kutokuwa na pesa za kujikimu.

Ila ukiangalia historia zao, unagundua kuna saili huko nyuma waliwahi kupasua, japo kwa uchache wa nafasi ikabidi waachwe.
 
wizy

JF-Expert Member
Sep 23, 2016
4,069
9,880
Acha kabisa Mkuu, ni vile hakuna pakusemea watu wakasikika. Ila naamini wapo wengi wanaishia kuziangalia nafasi mpya huku hawana jinsi inabidi waziache kwa sababu ya kutokuwa na pesa za kujikimu.

Ila ukiangalia historia zao, unagundua kuna saili huko nyuma waliwahi kupasua, japo kwa uchache wa nafasi ikabidi waachwe.
Ndo hivyo maana nauli ,hela ya kula na sehemu yakulala kwa siku kama tatu hivi sio mchezo
 
BAHARI J

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
766
886
Daaah nime Kumbuka rout moja toka kijin kwetu ad shinyanga kufanya usairi....
Nauli ya kwenda nika kopa..... Kula nika unga unga.... Kulala gest siku ya kwanza tuka unga na jamaa tuka share room.
Siku ya jumamos tuka fanya usairi fresh majibu yalikuwa saa nane mchana.... Tuka shinda tuna kunywa maji huku tukianza kutafuta nauli kama tukipita tubaki ad juma tatu kwaajiri ya oral...
Saa nane hii hapa Mungu alikuwa upande wetu tukapita sasa oral juma tatu...
Unga unga juma tatu ila fika piga usairi daah mazingira ya nje kujiandaa yalikuwa duni sana Huna uwakika wa kula unawaza kufaulu upate kazi
All in all Mungu mwema sana tuendeleee kupambana
 
Duh! Mkuu, inasikitisha sana hebu malizia ilikuwaje, mlifanikiwa kupata kazi kupitia huo usaili? Na kama hamkupata kazi, ulifanikiwa kulipa deni la watu?
 
meck pro

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
1,322
2,752
Shida ni moja tu kwa mawazo hayo Kuna watu watakua wanapachikwa kwenda oral kwa kisingizio cha walifaulu interview iliyopita wakakosa nafasi kifupi saili na formula ya Sasa inavyoendeshwa ipo fair kwa asilimia kama 80 hizo ishrini zilizopaki ni zinapotea linapokuja swala la database kwa namna yeyote najua Kuna watu wanaitwa kazini na wasema walikua database ila kiuhalisia ni kupachikana tu ndugu na Wenye connection so unavyosema watu wakifaulu wawe wanawekwa database kwa ajiri ya interview nyingine waingie oral moja kwa moja mie nauhakika Kuna siku utaenda fanya interview written hatachaguliwa hata mmoja mtaambiwa Kuna watu walifaulu kwa Makisi za juu Zaid yenu wapo Sita so hao ndo wataenda oral nyie wengine mrudi home so kifupi nasema hivi USIAMINI DATABASE MKUUU

ila na support kwenye swala la gharama kwa kweli kwa jobless tunapigika sana kwenda dodoma
 
Yani database siku zote kuna chenga ya mwili tunapigwa pale lakini wangefanya interview zifanyike kimikoa ingepunguza gharama sema na hii yakimikoa pia ina risk mnapofika kwenye oral unaweza kukuta panelist wa mkoa X wako fair kuliko panelist wa mkoa Y , hapo napo unakuwa shida ila kwa mfumo wa sasa upo fair sana wote mnakandwa sehemu moja kama kufokewa na panelist mnafokewa pamoja
 
Ni kweli mkuu usaili upo fair Kiasi now(japo connection huenda zipo) shinda gharama tu mkuu labda usaili ukifanyika kikanda gharama zitapungua kidogo
 
meck pro

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
1,322
2,752
Connection hazikosi lakini ukifanyika kikanda ndo connection itaongezeka mkuu Yani bora asaivi
Kweli mie hata kikanda huwa sifagilii sana ndo maana huwa sichangii mada hiyo kukataa kuhofia wadau kunishambulia Bure so napiga kimya ila najua hapo watu watalia vibaya kama zoezi la sensa Kila mtu analalamika na mkoa wake hawapo fair ndo maana hata ukisoma comment yangu juu ni meweka Neno labda nikijua tu hapo hakuna kitu
 
wizy

JF-Expert Member
Sep 23, 2016
4,069
9,880
Kweli mie hata kikanda huwa sifagilii sana ndo maana huwa sichangii mada hiyo kukataa kuhofia wadau kunishambulia Bure so napiga kimya ila najua hapo watu watalia vibaya kama zoezi la sensa Kila mtu analalamika na mkoa wake hawapo fair ndo maana hata ukisoma comment yangu juu ni meweka Neno labda nikijua tu hapo hakuna kitu
Kabisa yani hizi interview zikianza kufanyika kikanda hatutatoboa aseeh
Ingawa ni gharama kwenda dodoma lakini inapunguza mambo ya connection kama mtu ameshawahi kufanya interview zinazosimamiwa na taasisi yenyewe bila utumishi atakuwa anaelewa hii shida ni heri mambo yabaki huko dodoma
 
JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,568
2,183
Namna bora ni utumishi kujumuisha idadi yote ya post za kila kada kwa nchi nzima kuanzia halmashauri hadi serikali kuu kisha kuzitangaza zote kwa pamoja kwa fani husika bila kutaja idara . Hii ya kutangaza leo nafasi moja taasisi fulani, kesho nafasi mbili wizara x, inaumiza sana waombaji ajira.
 
herikipaji

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
1,137
1,128
Shida ni moja tu kwa mawazo hayo Kuna watu watakua wanapachikwa kwenda oral kwa kisingizio cha walifaulu interview iliyopita wakakosa nafasi kifupi saili na formula ya Sasa inavyoendeshwa ipo fair kwa asilimia kama 80 hizo ishrini zilizopaki ni zinapotea linapokuja swala la database kwa namna yeyote najua Kuna watu wanaitwa kazini na wasema walikua database ila kiuhalisia ni kupachikana tu ndugu na Wenye connection so unavyosema watu wakifaulu wawe wanawekwa database kwa ajiri ya interview nyingine waingie oral moja kwa moja mie nauhakika Kuna siku utaenda fanya interview written hatachaguliwa hata mmoja mtaambiwa Kuna watu walifaulu kwa Makisi za juu Zaid yenu wapo Sita so hao ndo wataenda oral nyie wengine mrudi home so kifupi nasema hivi USIAMINI DATABASE MKUUU

ila na support kwenye swala la gharama kwa kweli kwa jobless tunapigika sana kwenda dodoma
Hata mie natafakari hivi ile kanzidata watu wanauhakika gani kuwa wale candidate walifaulu adi kuekwa katika kanzidata na kupewa kazi? Hiyo kanzidata nani anaifanyia verification kuthibitisha?
Nani anacheki na kukagua taratibu za utumishi katika kuajiri? Maana malalamiko yamekua mengi kwa muda mrefu sasa.

Mie naona utaratibu ubaki kama ulivyo lakini kuwe na uhakiki na ukaguzi kuhakikisha utumishi wanafanya kazi kwa maadili na haki. Mfumo na kanzidata ukaguliwe kama idara nyingine zinavyokaguliwa na CAG. Tunaweza kuongeza majukumu ya CAG aingie na utumishi kukagua utaratibu mzima wa kuajiri kama unafanyika inavyotakiwa.
 
8 Reactions
Reply
Top Bottom