Hebu tuwaze ili tujenge nchi yetu Wapendwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu tuwaze ili tujenge nchi yetu Wapendwa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyange, Jul 23, 2011.

 1. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kamishna wa TRA ndg E. Kitilya Ng’oka?

  Tanzania kwa muda mrefu sasa tumejikuta tukishuhudia watendaji wa Serikali wakiwa kwenye nyadhifa kwa muda mrefu bila ufanisi na wala kubadilishwa kwa kushindwa kikamilifu.

  Tumeshuhudia pia kuwa mpango wa kodi ‘’Tax planning and tax base system’ umekuwa hauridhishi kiasi kwamba kila mwaka kodi ni zile zile na kinacho fanyika huongeza asilimia fulani kwenye kodi zilizopo kiasi kwamba hali ya wafanya biashara zina wafanya washindwe kukua na kubadili maisha huku wafanyabiashara wanao jiita wawekezaji wakineemeka kwa misamaha ya kodi, ndege zikitua na kuondoka kwenye migodi na madini ya nchi bila kukaguliwa!

  Ndugu wanaJf, hili limenisumbua sana kuona TRA inazidi kuchangia kutufanya masikini zaidi kwa kuongeza pia ushuru kwenye uagizaji wa magari kutoka nje. Huyu E. Kitilya ni kiumbe gani wakati anafanya watanzania maisha yao yakiwa yanazidi kuwa mabaya huku akikalia ofc kwa muda mrefu, wakati hatuoni utendaji wake kama unaridhisha?

  Yuko kwa maslahi ya nani? mbona huyu bwana hashambuliwi ili abadilike? Hebu tupige kelele kwa huyu bwana ili ang’oke, naye ni kama watu wanao changia kuua taifa letu. Mi naamini Fiscal policy ya Tz ina matatizo makubwa na Bunge linabidi litambue kuwa linahusika kutuumiza. ‘Please JF let us shout’ Mungu aweza kutusikia. ‘They think they are controlling car imports to reduce road traffic. HAPA KINACHO FANYIKA MNAUA WATANZANIA KWA KUWAFANYA MASIKINI ZAIDI.

  Hebu tuwataje wanaoangamiza taifa hili ni
  · Bunge kwa kushindwa kusimamia kikamilifu uchumi kwa kutumia fiscal instruments, badala yake kila mwaka mnajiongezea posho bila kufanya kazi yao kwa uadilifu.
  · Ukiacha Wizara ya Nishati na Madini, Ardhi kwa kuacha nchi ikiwa kwenye ujenzi wa hovyo, Ujenzi kwa kujenga barabara bila kiwango, Usalama wa taifa + Tume ya Taifa ya uchaguzi, kwa kutuchagulia viongozi dhaifu badala ya wananchi kujichagulia viongozi makini.
  · Watendaji wa serikali hasa upande wa Wizara ya fedha-Tax planning kwa kuongeza wigo wa kodi na kuhakikisha kodi inakusanywa bila kuumiza watanzania na kuwapandishia kodi. Huku mkilipwa kwa ajili ya kazi hiyo.
  · Viongozi wa Serikali kutumia muda mwingi kujisafisha bila kuweka juhudi ktk kuweka nguvu za kuinua uchumi.
  · Taasisi za umma zinazotumia raslimali za nchi kulinda viongozi kama Vile TAKUKULU, Jeshi la polisi, Mahakama, tuonee huruma muda si mrefu mambo hayako sawa hapa TZ.
  · ……….
  Vyama vya upinzani mko wapi nani awambie nchi iko pabaya?? Yaani, watanzania pole sana na samahani kwa kuandika mambo mengi na kuyachanganya.
  You still have another 4 yrs in dark, and in economic crises. We can not wait GOD to intervene this! Let us share Tufanyeje?
   
 2. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sina haja ya kuongeza, umesema vyote...
   
 3. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Tuwaze nn kama, "Mzee ruksa miaka 10 hakuyamalza, mzee Nkapa miaka 10 hakuyamalza, mie miaka 5 hayajaisha nmeongeza 5 mingne hayatakwsha" Jk
   
Loading...