Jamani wanajamvi kwanza naomba maadimin wasiuunganishe huu uzi na uzi mwingine lengo nikuelezea bayana wizi ambao bodi ya mikopo inataka kuwafanyia wananchi maskini. Kwanza ikimbukwe waliiomba mikopo jumla yao ni wanafunzi 88650 na waliopata ni wanafunzi 20000 kwahiyo ambao hawajapa ni zaidi ya 66000 ukizidishi mara appeal fee yaani sh 10000 unapata sh 660 millions halafu katika hzo pesa wanasema tumebaini wenye vigezo wanaostahili kulipwa ni 200.kama kila mwanafunzi atapewa sh 3000000 pesa hiyo itatosha na senti nyingine xitabaki. Sasa kwanini nasems wizi sababu ni hii hawa jamaa walisema ni wanafunzi elfu 5 tuu ndio waliosahau kuambatanisha nyaraka muhimu ili wapewe loan sasa siwangeyatoa hayo majina elfu 5 ili waambatanishe hizo nyaraka wanazoziitaji ili waweze kupatiwa mikopo na waswas wangu utakuwa mkubwa zaidi kama iyo elfu 10 itawahusu na wanaoendelea hebu jamani msiharibu mazuri alioyaacha jk mwisho wa siku mtakuja aibika wizi wa wazwaz na uhuni inawezekana ukawa umebarikiwa ndalichako . Sasa serikali hii ilisema matajiri wataishi kama mashetani sasa imekuwa kinyume chake sisi walalahoi tunaendelea kukamuliwa natukiishi kama maibilisi ifikie hatua wananchi tuamue tuuu. Hatuelewi haya maigizi yanatupeleka wapi?