Hebu tuujadili huu wizi ambao HESLB wanataka kutufanyia

Mwemary

JF-Expert Member
May 25, 2016
304
500
Jamani wanajamvi kwanza naomba maadimin wasiuunganishe huu uzi na uzi mwingine lengo nikuelezea bayana wizi ambao bodi ya mikopo inataka kuwafanyia wananchi maskini. Kwanza ikimbukwe waliiomba mikopo jumla yao ni wanafunzi 88650 na waliopata ni wanafunzi 20000 kwahiyo ambao hawajapa ni zaidi ya 66000 ukizidishi mara appeal fee yaani sh 10000 unapata sh 660 millions halafu katika hzo pesa wanasema tumebaini wenye vigezo wanaostahili kulipwa ni 200.kama kila mwanafunzi atapewa sh 3000000 pesa hiyo itatosha na senti nyingine xitabaki. Sasa kwanini nasems wizi sababu ni hii hawa jamaa walisema ni wanafunzi elfu 5 tuu ndio waliosahau kuambatanisha nyaraka muhimu ili wapewe loan sasa siwangeyatoa hayo majina elfu 5 ili waambatanishe hizo nyaraka wanazoziitaji ili waweze kupatiwa mikopo na waswas wangu utakuwa mkubwa zaidi kama iyo elfu 10 itawahusu na wanaoendelea hebu jamani msiharibu mazuri alioyaacha jk mwisho wa siku mtakuja aibika wizi wa wazwaz na uhuni inawezekana ukawa umebarikiwa ndalichako . Sasa serikali hii ilisema matajiri wataishi kama mashetani sasa imekuwa kinyume chake sisi walalahoi tunaendelea kukamuliwa natukiishi kama maibilisi ifikie hatua wananchi tuamue tuuu. Hatuelewi haya maigizi yanatupeleka wapi?
 
Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,250
2,000
Nasapoti Mod wasiunganishe huu Uzi.

Kuna wanafunzi 5000 ambao watapatiwa Mkopo.

Kati yao kuna F6, Equivalent na watakaokata rufaa.

Nitajuaje ulazima wa mimi kukata Rufaa?

Chuo wataniandikisha huku nasubiri rufaa?

Kwa nini Bodi isi update information ili nikiingia nione ulazima wa kukata rufaa?
 
endesha

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
918
1,000
Naunga mkono hoja.Na nakusihi ushikilie shilingi mpaka tupate majibu ya KINA.Huu ni wizi wa mchana kabisa
 
msono

Member
Oct 17, 2016
8
45
tatizo ni kwamba hawa jamaa washajua aina ya wananchi wanaowaongoza kuwa hawa reason tunaleta siasa na mambo ya msingi kama rais akiwa Igunga alisema atakaye mnyima mwanafunzi aliyedahiliwa kujiunga chuo kikuu mkopo na ana sifa katika serikali yake ajiandae kuachia ofisi ivi ni kweli hayaoni haya?acheni kucheza na watu utafikili hizo pesa wanatoa bure kumbe ni mkopo nawatarejesha sitakagi ujinga kwenye mambo ya msingi mda huo watoto wao wanatanua Kwa kodi zetu
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,745
2,000
Hili la wanafunzi na mikopo naona nyota na sarakasi. Yaani ukipita vijijini utaona kwa nini serikali inapaswa kuruhusu na kuwakopesha wanafunzi wengi ili tuongeze idadi ya raia wanaojitambua hata kama ajira watakosa lkn fikra zitakuwa Pana.
 
juju000

Senior Member
Apr 2, 2015
143
225
Very true. .. achana na huo kuna wizi mwingine waliofanyiwa wenye equivalent qualification. Mwanzo kwenye guide book waliweka vigezo kwa equivalent qualification halafu Leo unasema hawajapata mkopo bila kutoa ufafanuzi
 
indian mark 2

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
373
500
mimi nashauli tu wanafunzi wote walitokea diploma na wamekosa mkopo na vigezo wanavyo waungane wote waende bodi tu kujua ni nini kilichosababisha mpaka wao wasipewe mkopo wakati vigezo vya mwanzo waliwaconsider. na kwanin waanzishe vigezo vingine vipya wakati vigezo vya mwanzo vipo na watu waliomba kupitia vigezo hivyo.
 
meloy

Member
Sep 27, 2016
75
125
Jamani wanajamvi kwanza naomba maadimin wasiuunganishe huu uzi na uzi mwingine lengo nikuelezea bayana wizi ambao bodi ya mikopo inataka kuwafanyia wananchi maskini. Kwanza ikimbukwe waliiomba mikopo jumla yao ni wanafunzi 88650 na waliopata ni wanafunzi 20000 kwahiyo ambao hawajapa ni zaidi ya 66000 ukizidishi mara appeal fee yaani sh 10000 unapata sh 660 millions halafu katika hzo pesa wanasema tumebaini wenye vigezo wanaostahili kulipwa ni 200.kama kila mwanafunzi atapewa sh 3000000 pesa hiyo itatosha na senti nyingine xitabaki. Sasa kwanini nasems wizi sababu ni hii hawa jamaa walisema ni wanafunzi elfu 5 tuu ndio waliosahau kuambatanisha nyaraka muhimu ili wapewe loan sasa siwangeyatoa hayo majina elfu 5 ili waambatanishe hizo nyaraka wanazoziitaji ili waweze kupatiwa mikopo na waswas wangu utakuwa mkubwa zaidi kama iyo elfu 10 itawahusu na wanaoendelea hebu jamani msiharibu mazuri alioyaacha jk mwisho wa siku mtakuja aibika wizi wa wazwaz na uhuni inawezekana ukawa umebarikiwa ndalichako . Sasa serikali hii ilisema matajiri wataishi kama mashetani sasa imekuwa kinyume chake sisi walalahoi tunaendelea kukamuliwa natukiishi kama maibilisi ifikie hatua wananchi tuamue tuuu. Hatuelewi haya maigizi yanatupeleka wapi?
ani wamesababisha mbaka watu wameacha kuripoti chuoni kwenyewe, mimi mmoja wapo nimeshaona mizinguo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom