Hebu tutazame timu iliyomzunguka Spika Job Ndugai

businesslink

Senior Member
Mar 20, 2019
129
113
Kuna msemo unaosema kawa ukitaka kumjua kiongozi tazama watu wake wakaribu waliomzunguka

Naamini kuwa Spika Job Ndugai lazima atakuwa kazungukwa na team nzito sana ya wasomi wa hali ya juu ambao wana uwezo, ujuzi na weledi uliotukuka.

Je team speaker ni akina nani? Elimu zao ni zipi? wamefanikiwa au wamefanikisha mambo yepi kwenye maisha yao ya public and Private? Na je waona mbali? Je wamefanyiwa extended vetting? Je wana ni watu ambao wameweka maslahi ya taifa mbele?

Je kwa haya yanayoendelea wana role zipi? Na hata kama maamuzi na matamshi ya spika kwenye hili sakata lake na CAG si ya spika moja kwa moja je hii team yake wamempa ushauri wenye maslahi kwa taifa?

Je hii ni team ya YES SPEAKER au ni watu embao wako independent minded with conviction? Je wako principled?
 
Usomi ni tofauti sana na weledi. Tunayo yaona huko bungeni yanatia shaka weledi wa hao wanao mzunguka huyo mtu pamoja na yeye mwenyewe.
Bunge dhaifu hujengwa juu ya udhaifu wa anaeliongoza.
Ndugai yuko busy anawatisha wabunge kwa madeni waliyonayo. Wasiseme.
Badala ya kujenga hoja za kudhihirisha uwepo wa heshima na uimara wa bunge ni VITISHO mpaka kwa waandishi wa habari kama walivyofanya Makaburu, Iddi Amin, Sadam Hussein etc hasa walipokaribia miisho yao.
Tatizo kubwa zaidi lililopo Tz ni unafiki wa hasa Wasomi wetu.
"... Wanachuja mbu wanameza ngamia....."
Katiba na sheria za nchi zinavunjwa, amri za mahakama zinagomewa, bunge linakuwa kichekesho cha karne, vyombo vya dola vya tumika kama mwiko jikoni, wao wako busy kulinda mazingira ya kuteuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilidhani utatoa majibu ya maswali unayoyauliza kumbe ni porojo tu zenye nia ya kuwafanya watu waone speaker amezungukwa na watu wa ovyo.
 
Wote ni ndiyo mzee kuanzia juu hadi mashinani

In God we trust
 
Wanaweza wakawa wazuri sana ila na wao wanaogopa kuitwa mbele ya kamati mahakama ya maadili na haki za bunge.
Ila ukweli uko palepale watanzania hatufai kuwepo duniani, tunaijaza dunia bila manufaa, Algeria hiyoo, Kenya hiyoo na Sudani hiyooo sisi tulotupo!
 
Kibajaji, Mlinga na Musukuma ndiyo watu wa karibu sana na Spika Ndugai.

You need not extrapolate at all. Kwa HEKIMA alionayo kama kiongozi basi inatosha kubaini yukoje. Sasa hekima inafundishwa wapi? Kwa wanaomzunguka? Nakumbuka usemi wa ki-slavik .... ako nyi stava, nyi stava! .... hana basi hakuna!
 
Spika mwenyewe dhaifu,unategemea waliomzunguka watakuwaje.

Si unaona kila kitu wao wanagonga meza kushangilia,ndiyo udhaifu wenyewe huo.
 
Safari hii Bunge kwa Mara ya kwanza limekutana Na Chuma Cha Pua ambacho kipo tayari kupoteza cheo Kuliko kunajisi Taaluma yake!

Taaluma yake inamtaka aseme Bunge Ni dhaifu wakati Siasa inamtaka asithubutu kusema Bunge dhaifu

Kasimama Na Taaluma Na Imani yake kutamka anachokiamini sahihi

Team Maslahi tungesimama upande wa Ugali
 
Back
Top Bottom