Hebu tulinganishe nguvu za kijeshi kati ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523
Rejeleeni somo tajwa hapo juu. Katika pitapita mtandaoni nimeshangaa kuona kwamba kumbe ktk rank za dunia (current) tanzania tunazidiwa hata na Uganda na kenya !!? Lakini kiutaalamu sijaelewa vigezo, karibuni tulinganue
 
kuna mambo binadamu anakua na ushawishi wa kujua lakini kamwa hayamsaidii kitu ktk maisha yake ya kila siku. na huyo yapo mengi ya msingi hana habari nayo. km ukijua uwiano wa nguvu za kijeshi east africa itakusaidia nini?
 
Tathimini kubwa hufanywa kwa kuangalia bajeti ya jeshi kwa wakati huo.

Sasa kwa sababu Kenya iko kwenye vita kule Somalia imefanya manunuzi makubwa sana hivi karibuni, hilo limeifanya kuwa moja ya majeshi yenye bajeti kubwa.

Nchi kama Uganda kuna waasi kule wanasumbua upande wa Kaskazini, kwa hiyo ni lazima manunuzi ya silaha yawe makubwa pia.

Kwa Tanzania kwa kuwa hatuna matishio ya vita, matumizi yetu kifedha ni madogo sana kwa hiyo kigezo cha bajeti kinachotumiwa sana kuyapima majeshi na uimara wake kinatufanya tuonekane tuko chini sana.

Ila bana, hapana chezeya muziki wa JWTZ, ile ni habari nyingine, kama unabisha nenda ukaishi mipakani mwa nchi zenye mapigano kama Burundi na Congo uwaulize wale wanaopigana kwa nini wakitibuana huwa wanabanana humo humo wakiuana, hawathubutu kuvuka mpaka kuja huku bongo kujificha.
 
KENYA DRINKING FORCE(kdf) hawa hawa wanasumbuliwa na alshabaab kila mara mbona hawayazimi hayo mashambulizi?
 
Back
Top Bottom