Jamani nimejaribu kupitia kwenye mitandao kutafuta mipango ya maendeleo ya makazi kwa hii miji miwili Kigali na Dar es salaam.
Nini kimenisukuma kwanza ni kutokana na maneno ninayoyasikia mtaani kuwa kigali rwanda ni kuzuli ni kuzuli.
Nikaingia kwenye youtube nikajaribu kutafuta kigali kwa bahati nzuri nikakutana "kigali master plan 2040" ki msingi nilijisikia kushikwa na wivu sana.
Kwa kifupi mimi katika katika kabila langu wanyarwanda walikuwa wanadhaurika sana tena sana. Hii kudhaurika ni kutokana na maisha yao waliyokuwa nayo huko nyuma ya vita na kuishia kuwa wakimbizi kule kwetu.
Watu hawa walikuwa wakifanya kazi za vibarua na kutuhumiwa kufanya matukio ya uhalifu kwenye jamii yetu hivyo walionekana watu wa chini sana.
Kwenye jamii yetu mtu akiambiwa mnyarwanda ilikuwa tusi kubwa sana. katika jamii yetu hii kuoa mnyarwanda ilikuwa ni kitendo cha kashifa ambacho ilikuwa ni kufanya kituko cha aibu.
Hivyo nilitafuta kutazama kigali nikiwa na mentality ya dharau hiyo kichwani lakini nimestaajabu kuona mipango ya jinsi kigali itakavyokuwa mwaka 2040 sio ya bara hili la afrika labda ulaya au amerika sawa.
Nikataharuki kwa maana waswahili wanasema "ukiona mtu kapiga hatua za kimaendeleo ukaona kawaida bila kusikia taharuki ya wivu ya kujiuliza hivi sisi tunafanya kitu gani? jua wewe upoupo tu.
Nikajaribu kutafuta "Dar es Salaam master plan"
Nilichokutana nacho kimeandikwa kama Dar es Salaam master plan kwenye youtube ni kituko. Nimekutana na porojo za watanzania wamerekodiwa mara wakilalamika majengo ya kihistoria yasibomolewe na porojo tu na picha za mji. Nilijisikia kunyongonyea nikajiuliza hivi natakiwa kudharau wanyarwanda au kujidharau kwa kuwa mtz.
Kama mpaka sasa hatuna master plan ya miji yetu kuona jamani mpango wa maendeleo wa makazi yetu tunaojaribu kuutekeleza ni huu, kuwa labda ikifika mwaka 2040 tunataka kuwa tumefikia hapa. Kila mmoja anatekeleza yake kichwani. Huyu akiamka anasema jangwa tunaweka hiki huyu kile, huyu anajenga hapa yule akija anabomoa.
Jamani wenye dhaman katika jambo hili mnatuangusha, jaribuni kutafuta hiyo kigali "2040 ilivyo mjaribu kuzisukuma miji yetu yote itengeneze dira kama hizo za maendeleo. Mkisha kuwa na hizo dira wekeni kanuni za kutuwezesha kufika huko.
Watu binafsi wajue kufika 2040 makazi yake kulingana na eneo alilopo linatakiwa liweje, manispaa zijue maeneo ambayo yako chini yao yanatakiwa yaweje, n.k.
Tukiwa na mipango tutafika lakini tukifanya bila mipango hatuwezi kufika popote. Maendeleo ni sawa na ujenzi wa nyumba ukijenga nyumba bila ramani leo unajenga chumba kimoja kesho unabomoa hapa unaongeza chumba pale utakuwa na nyumba kubwa mwishoni lakini isiyoeleweka na hivi ndivyo tunavyojenga miji yetu.
hii ndio kazi ya msingi ya wale wenye dhamana ya ardhi na maendeleo ya makazi kwa mijini.