Hebu tukumbushane uongo ambao Watanzania tuliwahi kudanganywa

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,039
Kuna uongo mwingi tuliwahi kuongopewa na watanzania weangi wakauamini hadi watu wakubwa na tuliodhani wanajua mambonao wakaukumbatia. Mimi ninaanza na huu.

1. Kipindi cha Jakaya Mrisho Kikwete akiwa rais, nakumbuka magazeti kadhaa na redio kadhaa ziliwahi ripoti kuwa kuna mapacha wawili ni watanzania ila wamesoma Marekani mmoja ni daktari bingwa na mwingine ni mfanyakazi wa NASA.

Eti kwamba walikuwa amerudi Tanzania, kwa likizo fupi ambapo huyo daktari bingwa alikuwa kafanya operesheni wagonjwa takribani 8 na wote wanaendela vizuri hapa Tanzania, wakati huyo mwanaanga wa NASA ni kati ya wanaanga wa kwanza kutembelea sayari ya Mars. Habari hiyo nakumbuka ilishikiliwa bango PJ na Gerald Hando wakati wote wako Clouds. Wakadai hawataki hojiwa na vyombo vya habari mpaka wakutane na rais.

Mimi nilianza kuwa na shaka na hao mapacha baada ya kusikia tu kuwa eti mmoja wao kashafika Mars, wkati mpaka muda huo na mpaka leo hakuna binadamu ambaye kakanyaga sayari ya Mars zaidi ya vyombo kama Rovers. Na nadhani Kikwete alikuwa mjanja hakuwahi kuwaalika ikulu.

2. Project Kubwa ya kujenga Kigamboni. Nakumbuka kuanzia mwaka 2009 mpaka 2014 nadhani, kulikuwa na video zinazoonyesha jinsi Kigamboni itakavyojengwa na wamarekani, viwanja kigamboni vikawa havishikiki kigamboni ikawa lulu. Zile video zilikuwa zinavutia sana. Jamaa yangu aliuziwa maeneo kule kwa pesa ndefu sana lakini sijajua hii story iliishia wapi, na viwanja vikaanguka thamani hadi alipotaka kuuza hakuweza kuuza hata robo ya pesa aliyotoa.

Nitarudi kuongeza
 
"Bwana fulani" alituaminisha waTz kuwa tanzania yetu eti ni "Dona kantri", tena level za mabeberu kabisa, nikikumbuka huwa machozi yananilenga lenga




Let's meet at the top, cheers
Taratibu blaza.
Screenshot_2019-12-21-09-59-03-1.jpg
 
Baada ya uvumbuzi wa gesi asilia ,mtwara itakuwa kama Dubai na matumizi ya mkaa yatakuwa mwisho.


Katika uongo mkubwa kupita mauongo yote nadhani huu ni mkubwa kupita kiasi, eti gasi ya Mtwara ingeinua uchumi wa bongo "drastically"!!!!🤣🤣.

leo cha ajabu hata Wapinzani wote wapo kimya kama kwamba fikra zao ni "blind folded" juu ya suala la gesi ya Mtwara.

sio Wapinzani wala Chama tawala wote hawazungumzii kabisa juu ya gesi ya Mtwara.

kama Wtz tumelogwa, tumepigwa bumbuwazi,!!!!🤣🤣
 
Back
Top Bottom