Hebu Tukumbushane Misingi ya Katiba Yetu na Hali Halisi

Vicky-Abelly

Member
May 27, 2016
72
89
Ndugu wana Jamvi, naleta kwenu misingi ya Katiba yetu ili tuijadili na kuona kama kuna haja ya Katiba mpya Tanzania

Misingi ya Katiba yetu inasema hivi:

Kwa Kuwa Sisi Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya UHURU, HAKI, Undugu na Amani:

Na Kwa Kuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye DEMOKRASIA, ambayo Serikali yake husimamiwa na BUNGE lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha WANANCHI, na pia yenye MAHAKAMA HURU zinazotekeleza wajibu wake bila WOGA wala UPENDELEO wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila MTU unatekelezwa kwa UAMINIFU:

KWA HIYO BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUMU LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya DEMOKRASIA, UJAMAA na isiyokuwa na dini.

Je, hayo yanayosemwa na KATIBA yapo na yanafuatwa? Kama jibu ni ndiyo kivipi, na Kama jibu ni hapana kivipi?. Na tunawezaje kusonga mbele kutokea hapo?
 
Back
Top Bottom