Hebu tukumbushane kidogo basi!

Maengo

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
280
29
Hivi unakumbuka kipindi kile ukiwa bado mtoto siku za sikukuu kama vile Eid, Xmas na Pasaka ukishakula pilau yako na kuvaa nguo mpya mchana ulikuwa unaenda kutembea wapi? Wale waliokulia dar wengi wao walikuwa wanaenda MANZESE DARAJANI kupiga picha kama sio kushangaa tu! Na kama sio manzese basi walikuwa wanaenda UWANJA WA NDEGE! wewe je?

Dah kweli we umezaliwa zamani sana, kumbe kuna vijeba wengi sana humu

Enzi za kutembea mmeshikana mikono ili musiwaache wadogo na kupoteana na wenzenu,wakubwa walivaa ten pasenti suruali inafungiwa tumboni alafu chini kanjiwa...wengine tulivaa mashati ya ujiuji (mtepeto)

All right, chini ndala kwa jina "bata", suruali ya kukwepa umande na juu flana kaba shingo. Jioni kule kijijini kwetu jumba la maendeleo kuona sinema! Wapi mwita25?

teh teh teh! Duh, ndo iko wapi hiyo?

Ipo Msasani karibu na nyumbani kwa hayati Mwl. Nyerere. Kwa sasa unaweza kufika kupitia Chama au pembezoni mwa ofisi za Tanesco Kinondoni kaskazini Old Bagamoyo Road. Bado Beach Mavi ipo, na iliitwa hivyo kutokana na wingi wa mitaro na mifereji ya maji machafu kumwaga maji ktk eneo hilo.

Michango ilikuwa inapitishwa kama mwezi mmoja hivi kabla ya siku yenyewe ya tukio, siku hiyo ikifika watoto waliochngiwa wanajumuika
T.T.I-Club Kidatu huko, tunakula pilau letu then tunashushia na Pepsi ya Enzi zile au koka Kola ambazo zilikuwa ni shilingi 20, baada ya hapo mashindano ya kucheza Disko.. Hapo ni watu kuvunja viungo mwanangu, ni mabreka kwa kwenda mbele. mshindi akipatikana anapewa shilingi 200 na creti la pepsi! Jioni ni disko la wakubwa ole wako sasa uende afu ukutane na mwalimu Chacha kesho kiama kitakushikia shuleni na utajuta kwenda disko la wakubwa!!!

kweli A.M?

Hehehe...unava shati la uji uji na suruali ya mchele mchele afu chini una viatu vya moka (saa nane utanikoma)...mnapanda uda enzi hizo watoto bure mnaenda posta kushangaa shangaa yale ma meli mabovu...hahaha

Nakumbuka moro kuna babu mmoja alikuwa anaitwa bab gereji katuibia sana na maonyesho aliyoita fetefete yani bembea, pipi za filimbi,maputo na mashindano ya kurusha visahani yani dah

Wa kule moshi kulikuwa kuna mhindi anaiza bagia,chauro,tambi weee boda hata uibe hela home kuliko kukosa kwenda kwa "jani" alikusanya hela yule duuuh

nakumbuka tulikuwa tunaenda ndugumbi(magomeni kondoa)kulikuwa na michezo kibao,sarakasi,mieleka,mabembea,korokoro,koni za kumwaga,..tulivyokuakua kidogo tukawa tunaenda dege beach tukipeperusha bendera za marekani na UK..i remember those days...

Dah kweli we umezaliwa zamani sana, kumbe kuna vijeba wengi sana humu
vijeba gani?daraja la manzese limejengwa mwaka 1993 au 94,ina maana ulikuwa haujazaliwa huo mwaka?si useme ukweli tu kuwa ulikuwa kwenu huko nyanchenche

inimegonga mawani yana kimdori, nimevaa shati la mchele mchele na suruali ya dukani imeandikwa canada chini nimepiga chchacha nimenyoa kisaani utanitaka nina shilingi 20 ya noti ya mtumizi acha mchezo usinikumbushe

Sharobaro meeeeeen

Back
Top Bottom