Hebu tujuane tuliokumbwa na homa kali ilioambatana ni kikohozi na hata kushindwa kupumua katika mwezi 1 uliopita na tuelezane tulifanyaje

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,059
2,000
Wiki 2 zilizopita yalinikuta hayo, nilipata homa kali sana iliambatana na kikohozi na koo kuuma.

Pia kushindwa kupumua vizuri ikiambatana na kuchoka! Kwa mara ya kwanza katika miaka zaidi ya 15 nililala kitandani siku mbili, pumu si pumu, mafua si mafua, joto mpaka wife alikuwa ananipoza kwa taulo lilolowanishwa maji! Piga antibiotic, hola, piga anti-malaria hola. Piga za pumu hola (ingawa huwa sina pumu).

Ikabidi niendeleze tu na panadol na dawa za kikohozi mpaka, na asali mbichi yenye tangawizi, nikaweza inuka na ninaendelea kudunda!

Siku mbili baadaye na wife naye akateteleka kidogo, naye akanywa dawa hizo hizo na siku ya pili akaendelea vizuri siku ya 3 yake akawa vizuri pia.

Mtoto wangu wa kiume naye akaonyesha dalili hizohizo na tukampa dawa akapona yeye haraka sana wala hakulala kitandani!

Yaani kama hii ingetokea kati ya jana na leo hakika ningejua ni Covid-19 imeshabisha hodi!

Naomba na weww kama yalikukuta kama haya hebu jimwage ukitujuza ulitibiwaje!

Nawakilisha!
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,627
2,000
Mkuu kweli una kumbukumbu hiyo mada ililetwa hapa jamvin lkn Wizara haikueleza lolote. Sasa hivi hata ukiugua kikohozi ipo hatari ukasukumwa Karantin ya Corona.

Nashukuru WHO wametoa dukuduku lao kwamba Afrika hatuko makini kwenye Vipimo maana kuna Nchi mgonjwa aliyekufa kwa Kisukari ametajwa kama amekufa kwa Corona.
 
Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,059
2,000
Mkuu kweli una kumbukumbu hiyo mada ililetwa hapa jamvin lkn Wizara haikueleza lolote. Sasa hivi hata ukiugua kikohozi ipo hatari ukasukumwa Karantin ya Corona. Nashukuru WHO wametoa dukuduku lao kwamba Afrika hatuko makini kwenye Vipimo maaana kuna Nchi mgonjwa aliyekufa kwa Kisukari ametajwa kama amekufa kwa Corona.
Yaani sasa hivi kuna watu watapewa Covid-19 kama njugu wasipokuwa makini pamoja na kutengwa!
 
DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
23,034
2,000
Mkuu kweli una kumbukumbu hiyo mada ililetwa hapa jamvin lkn Wizara haikueleza lolote. Sasa hivi hata ukiugua kikohozi ipo hatari ukasukumwa Karantin ya Corona. Nashukuru WHO wametoa dukuduku lao kwamba Afrika hatuko makini kwenye Vipimo maaana kuna Nchi mgonjwa aliyekufa kwa Kisukari ametajwa kama amekufa kwa Corona.
Bila Isabela kujitokeza hadi leo watoto wangekuwa wanakwenda mashuleni
 
naiman64

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
6,141
2,000
Mkuu kweli una kumbukumbu hiyo mada ililetwa hapa jamvin lkn Wizara haikueleza lolote. Sasa hivi hata ukiugua kikohozi ipo hatari ukasukumwa Karantin ya Corona.

Nashukuru WHO wametoa dukuduku lao kwamba Afrika hatuko makini kwenye Vipimo maana kuna Nchi mgonjwa aliyekufa kwa Kisukari ametajwa kama amekufa kwa Corona.
Tuliambiwa tunywe maji mengi sana, wenyewe walikuwa hawakuji hadi Mkwasa Mrs. alipowazindua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom