Hebu tuchambue matumizi ya haya magari ya viongozi wetu yanazolalamikiwa

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
14,907
2,000
Wakuu kuna huu mjadala wa matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wetu haya ma V8

Tangu napata akili huu mjadala nimeukuta ukijadiliwa.

Sasa hebu wanaojua tujadili gharama zake hasa manunuzi na matumizi yake ya mafuta mfano V8 moja linatumia kiasi gani cha mafuta kwa kilometa 1 n.k

Lengo tujue ni jinsi gani tunapoteza kwa ajili ya magari tu. Na ikiwezekana tutoe na pendekezo la gari gani zinafaa kwa viongozi wetu zenye gharama nafuu lakini zina usalama kwa viongozi wetu.

Asubuhi njema wakuu.
 

am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
445
1,000
"No research no right to speak"

Natafuta wasaa nifanye utafiti then nitarudi ku comment.
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
14,907
2,000
Tangu mtu anye huko Geita, naona saizi mavi yanarushwa kila mtaa...
Mkuu huu mjadala haujaanza baada ya msukuma kusema.

Nakumbuka kina Lema walimbana Pinda hadi anataka kulia kule bungeni sababu ya haya magari.
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,454
2,000
Kuna taasisi moja ya serikali, boss wa taasisi alikuwa anatumia Suzuki Maruti nyeupe mpaka kastaafu, kwa sasa ni marehemu. Na alikuwa Brigedia wa jeshi miaka hiyo ya awamu ya pili. Maruti hiyo ilitumika pia kwa kiongozi wa awamu iliyofuata na ikapumzishwa awamu ya Mkwere mwishoni. Taasisi hii ilikuwa inazalisha pesa.

Hard top kushuka chini ndo uwezo wa serikali inayotegemea wahisani kujiendesha.

Ma VX V8 ni anasa kwa sasa, yanazurula tu mjini hapa, kutumwa kwa michepuko tu na kutufanyia fujo road.
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Kama yule kule Geita kawekwa pembeni, hao wanapewa nafasi yakujieleza ili iweje.

Hapo watasema mabaraza ya madiwani yamepitisha.

Wapumzishwe kwenye nafasi hizo wapewe wengine kama wameshindwa kua waadilifu
 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,836
2,000
Hesabu yake sio mchezo mkuu! Fikiria kitaani tuu gari ina cc 2500 na inauzwa 25m wafanyabiashara wenye kipato kizuri tu wanazikimbia kisa, Spare ghali.

Ulaji wa mafuta ,....sasa hayo ya 400m na cc 4500 unafikiria je
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
2,765
2,000
Serikali inabidi itumie ma-V8 japokuwa yana gharama kubwa kwa sababu barabara ni mbovu
IMG_20201218_085434.jpg
 

komrade

Senior Member
Sep 26, 2019
138
250
Upepo wa kisiasa, unavuma kisiasa.

Kwa Serikali kununua magari ya Japan, ni kubana matumizi tosha. Sijui hali ingekuwaje kama magari ya aina hiyo yangenunuliwa toka Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italy...
 

Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,127
2,000
Wakuu kuna huu mjadala wa matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi wetu haya ma V8

Tangu napata akili huu mjadala nimeukuta ukijadiliwa.

Sasa hebu wanaojua tujadili gharama zake hasa manunuzi na matumizi yake ya mafuta mfano V8 moja linatumia kiasi gani cha mafuta kwa kilometa 1 n.k

Lengo tujue ni jinsi gani tunapoteza kwa ajili ya magari tu. Na ikiwezekana tutoe na pendekezo la gari gani zinafaa kwa viongozi wetu zenye gharama nafuu lakini zina usalama kwa viongozi wetu.

Asubuhi njema wakuu.
Vx V8 inaenda 4-5 km/l
Hayo magari yanastarehe bwana acha kabisa.
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,580
2,000
Kiuhalisia hayo magari yanakula kodi za watanzania si mchezo.

Msafara wa JPM unaweza kuwa na hizo gari almost 50.

Kila moja inakula 5km/l.

Hizo gari hazizimwi mwanzo mpaka mwisho wa safari, zipo silencer msafara ukisimama.

JPM akitoka Dom kwenda Dar kwa barabara, gharama yake inafika almost 500M kwa posho, mafuta, services na misc.

Nashauri viongozi wakuu na mawaziri pekee ndo watumie hizo VX V8. Hao wengine watumie magari yao ila serikali iwawekee full tank kila jumatatu. Wataokoa hela nyingi sana.

Kama kila mtu serikalini atataka kuendeshwa na hizo gari, hela nyingi sana inapotelea huko.
 

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
466
500
Vx V8 inaenda 4-5 km/l
Hayo magari yanastarehe bwana acha kabisa.

Mkuu sio kweli hata kidogo 1ltr/7km na itategemea na upya au uchakavu wa gari, kuna hizi Prado New Model TXL 2019/2020 nimetoka nayo Dar to Arusha nimetumia half tank tu mkuu.

Kwa hiyo 1ltr/4km sio sahihi kiongozi. Thanks.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom