Hebu tuangalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais Magufuli Maabara kuu ya Taifa

Na iliyokutwa negative nayo ilikuwa contaminated na vitu gani hadi hicho kipimo kikatoa jibu negative??
Hiyo negative ina maana hakiko contaminated. It it is true negative. Samples zenye matatizo ni zile ambazo ni false negative au false positive.
 
Hiyo negative ina maana hakiko contaminated. It it is true negative. Samples zenye matatizo ni zile ambazo ni false negative au false positive.
Kwanini kipimo kitoe majibu negative wakati hiyo sample sio sahihi kwa kipimo husika kwanini haikukataa kuwa hiyo sample ni unknown?
 
Kwahiyo kwasasa tunatumia hizo zilizokuwepo hapa nchini au tunatumia hizo tulizoletewa??
Siwezi kujibu hayo kwa kuwa sifanyi kazi huko. Ila nilichokuwa nasema ni kuwa technology inayotumika siyo ngeni. REAL TIME PCR zipo TZ na zinaweza kufanya analysis ya Covid 19.Naamini watachokuwa wamepewa ni procedure Labda na training possibly online.
 
Hawa Wataalamu hawana hatia mnataka kuwaonea tu! Wao wanakuwa GUIDED na vipimo kwa kupata swap sahihi toka kwa Binadamu under suspect ya Covid-19!

Sasa Kama mtu anakufanyia HILA anakuletea OIL, PAPAI, FENESI, KWALE etc, expect a very COMPLICATED RESULTS Kama tulivosikia: INDERTEMINATE, NEGATIVE na POSITIVE altogether!!
Soma tena mada labda utaelewa Kisha uje tena tujadili mkuu.
 
Kwanini kipimo kitoe majibu negative wakati hiyo sample sio sahihi kwa kipimo husika kwanini haikukataa kuwa hiyo sample ni unknown?
Wanaporeport negative ina maana kuwa specific nucleiic acid was not detected. Kwa hiyo unaposema negative it means not detected or not present.
 
Ndio nakuuliza kama hizo sample ziko contaminated kwenye process yote hiyo na mtu aliye chukuliwa hiyo sample akapewa majibu ya positive Inamaana tuna wagonjwa ambao ni positive kwa makosa na sio kwamba wanaumwa Corona kama walivyo ambiwa??

Unasema madaktari wangegundua, wangegundua lini wakati tunaona hapa hadi Rais ndio anakuja kuwafumbua macho mkuu?.
Sijasema kuwa madaktari wangegundua. Nimesoma kama kulikuwa na contamination kwenye maabala matechnicians au scientists wangegundua.
 
Siwezi kujibu hayo kwa kuwa sifanyi kazi huko. Ila nilichokuwa nasema ni kuwa technology inayotumika siyo ngeni. REAL TIME PCR zipo TZ na zinaweza kufanya analysis ya Covid 19.Naamini watachokuwa wamepewa ni procedure Labda na training possibly online.
Rais amesema vifaa hivyo vimeletwa hapa nchini maalumu kwaajili ya corona na si hivyo ulivyovisema wewe, na baadhi ya wataalam wamesema vipimo hivyo ni kwaajili ya kupima Covid-19 tu na si vinginevyo, Inamaana ukipima kitu tofauti lazima kitaleta majibu Unknown.
 
Wanaporeport negative ina maana kuwa specific nucleiic acid was not detected. Kwa hiyo unaposema negative it means not detected or not present.
Mkuu mbona tunachoshana bure, not present or not detected kwanini wakati sample sio sahihi au hili swali huliewi mkuu?? Sample sio sahihi kwenye kipimo sasa jibu kama hilo limekujaje??
 
Ni jambo la kushangaza na kutia shaka kuona wataalam na wanasayansi wa Tanzania wanavyopinga uchunguzi wa Rais kwa hoja dhaifu.

Hii inatia shaka juu ya uwezo wa wataalam tulio nao hapa nchini.

Hebu tungalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais kwa jinsi wataalam wetu walivyozitolea maelezo.

1 vipimo ni Specific kwaajili ya kupima virus ama bacteria, hivyo huwezi kupima sample tofauti DNA/RNA hivyo basi hakiwezi kupima papai, lazima kitaleta majibu tofauti.!!

Hoja hii haina mashoka kama ni hivo kwa nini vipimo hivi vimetoa majibu ya positive na negative wakati sample sio sahihi??

Je wataalam wetu walijaribu kuvifanyia uchunguzi wowote hivi vifaa pindi vilipokaja kabla hawajaanza kuvitumia??
Kama hawakufanya kwanini waliviamini moja kwa moja, taaluma yao iko wapi hapi??

2 wataalam wengine wakaja na hoja kuwa majibu yanaweza kuwa positive kwasababu sample zinaweza kuwa zinamaambukizi (Contaminated) ama wakati wa kuchukua sample ama wakati wa upimaji hivyo kipimo kitatoa majibu Positive.!!

Okay.
Sasa kama ni hivi hamuoni hapo kuna uwezekano kuna watu ambao ni negative hawana maambukizi Ila kwasababu ya uzembe/ makosa wakati wa kuchukua sample ama uzembe wakati wa upimaji wakaiambukiza hiyo sample na kumpa mtu majibu ya positive kumbe Hana maambukizi?? Mtu unapewa ugonjwa ilihali huumwi.

Alafu hivi kama hiyo sample sio sahihi na imetoa positive kwasababu ipo Contaminated mbona sample za nanasi na kondoo zimetoa majibu negative??
Kwanini iwe negative wakati sample sio sahihi na haipo contaminated??

Hili limekaaje sasa wataalam? Inamaana kama inangekuwa haipo contaminated si ingetoa majibu kuwa haitambuliki (sample sio sahihi) kwanini Sasa ikatoa negative??

Halafu Inamaana team ya watafiti wa Rais hawakuwa na uelewa kabisaa kiasi kwamba wakazichukua sample tu ovyo ovyo bila ya umakini wowote na kuzipeleka tu zikapimwe hadi zinapata maambukizi??
Siamini kama ni wajinga kiasi hiki.

3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??

Hamuoni hapa kunatakiwa kufanyaka uchunguzi wa kina kama Rais alivyotilia shaka??

Kumbe sample zinakuwa contaminated hapo hapo maabara na kutupa majibu ya positive kwanini waachwe Sasa??.

Watanzania wenzangu Mimi kwa maoni yangu mh Rais anahoja ya msingi sana tusimpuuze, hawa wataalam wetu ndio wanatudanganya mh Rais yuko sahihi..

Kuna sehemu haiko sawa katika hili.

Kama una majibu ya maswali hayo uje hapa ulete ufafanuzi.
Jibu zuri ni kupeleka hizo sample katika mabara za nje ili kufanya quality assuarance
 
Ni ya kuchukua sampuli katila fenesi ni nini?

Je ni kuonyesha kuwa hatuna co-vid nchini???
 
Sijasema kuwa madaktari wangegundua. Nimesoma kama kulikuwa na contamination kwenye maabala matechnicians au scientists wangegundua.
Unauhakika gani kama hizo contamination hazipo kwenye hiyo maabara.?
Alafu kumbuka hayo mambo ya contamination ni hao wataalam ndio waliyosema sasa iweje wasema vitu ambavyo havipo kwenye hizo maabara.?
 
Back
Top Bottom