Hebu tuangalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais Magufuli Maabara kuu ya Taifa

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,099
2,000
Ni jambo la kushangaza na kutia shaka kuona wataalam na wanasayansi wa Tanzania wanavyopinga uchunguzi wa Rais kwa hoja dhaifu.

Hii inatia shaka juu ya uwezo wa wataalam tulio nao hapa nchini.

Hebu tungalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais kwa jinsi wataalam wetu walivyozitolea maelezo.

1 vipimo ni Specific kwaajili ya kupima virus ama bacteria, hivyo huwezi kupima sample tofauti DNA/RNA hivyo basi hakiwezi kupima papai, lazima kitaleta majibu tofauti.!!

Hoja hii haina mashoka kama ni hivo kwa nini vipimo hivi vimetoa majibu ya positive na negative wakati sample sio sahihi??

Je wataalam wetu walijaribu kuvifanyia uchunguzi wowote hivi vifaa pindi vilipokaja kabla hawajaanza kuvitumia??
Kama hawakufanya kwanini waliviamini moja kwa moja, taaluma yao iko wapi hapi??

2 wataalam wengine wakaja na hoja kuwa majibu yanaweza kuwa positive kwasababu sample zinaweza kuwa zinamaambukizi (Contaminated) ama wakati wa kuchukua sample ama wakati wa upimaji hivyo kipimo kitatoa majibu Positive.!!

Okay.
Sasa kama ni hivi hamuoni hapo kuna uwezekano kuna watu ambao ni negative hawana maambukizi Ila kwasababu ya uzembe/ makosa wakati wa kuchukua sample ama uzembe wakati wa upimaji wakaiambukiza hiyo sample na kumpa mtu majibu ya positive kumbe Hana maambukizi?? Mtu unapewa ugonjwa ilihali huumwi.

Alafu hivi kama hiyo sample sio sahihi na imetoa positive kwasababu ipo Contaminated mbona sample za nanasi na kondoo zimetoa majibu negative??
Kwanini iwe negative wakati sample sio sahihi na haipo contaminated??

Hili limekaaje sasa wataalam? Inamaana kama inangekuwa haipo contaminated si ingetoa majibu kuwa haitambuliki (sample sio sahihi) kwanini Sasa ikatoa negative??

Halafu Inamaana team ya watafiti wa Rais hawakuwa na uelewa kabisaa kiasi kwamba wakazichukua sample tu ovyo ovyo bila ya umakini wowote na kuzipeleka tu zikapimwe hadi zinapata maambukizi??
Siamini kama ni wajinga kiasi hiki.

3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??

Hamuoni hapa kunatakiwa kufanyaka uchunguzi wa kina kama Rais alivyotilia shaka??

Kumbe sample zinakuwa contaminated hapo hapo maabara na kutupa majibu ya positive kwanini waachwe Sasa??.

Watanzania wenzangu Mimi kwa maoni yangu mh Rais anahoja ya msingi sana tusimpuuze, hawa wataalam wetu ndio wanatudanganya mh Rais yuko sahihi..

Kuna sehemu haiko sawa katika hili.

Kama una majibu ya maswali hayo uje hapa ulete ufafanuzi.
 
google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,673
2,000
Mkuu umejiuliza maswali mazuri sana, ni kweli kwa tanzania kila kitu kipo , yaani wataalamu uchwara na orona pia ipo.

Mashaka zaidi ni kwamba kama hao waliopima hizo sample ndio walio bora na wanafanya kazi katika taasisi ya raisi basi mashaka ni makubwa zaidi hata kwa usalama wake.

Hata hivyo ndio maana tunaona viongozi wengi sana wakiondoka nchini na kwenda kutibia nje ya nchi sababu ya hali ya uzembe uzembe kama hii.

Pande zote zina hoja ya msingi kabisa ya kulaumiwa mpaka raisi mwenyewe maana wale ni watendaji wake.
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,587
2,000
We unataka kutuambiaje sasa? Kwamba vipimo ndio tatizo au wanasayansi ndio wenye tatizo?

Vipimo ambavyo vilitumika kupima idadi ile ya watu na kukuta ma maambukizi, halafu jitihada za kimatibabu zilipofanyiwa kwa watu hao mpaka ikapelekea wapone. Unaweza kutuambia vilitumika vifaa gani kuthibitisha kua wagonjwa hao walipona?

Au ni madaktari kutoka nchi gani na vipimo kutoka wapi vilivyo confirm kua wagonjwa hao wame-recover wakati hivyo vipimo hutoa majibu ya positive katika kila test itakayo fanyika?
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,022
2,000
Hao waliochukuwa sample za mapapai hawana utaalam ndiyo sababu tunasema huenda sample zilikuwa contaminated. Sasa unatumiaje hiyo hoja kwa sample zinachukuliwa na wataalam waliosomea kazi yao na wenye uzoefu, ondoa huo utetezi wako
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,587
2,000
Kabla hata ugonjwa haujaja hapa bongo, madaktari kutoka nje walikua wakitoa rai kua mgonjwa wa corona akigusa kitu chochote lazima aache virus.

Sasa kama virus anaweza kukaa kwenye chuma endapo mgonjwa wa corona akishika unafikiri ni ngumu virus kukaa kwwnye liquid ya papai wakati ndio mazingira rafiki kutokana na ile liquid?

Kama wao walikua wanajua kisayansi haiwezekani virus wakawepo katika mapapai, walianzaje kupeleka sampuli hizo lab?
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,117
2,000
Umeambiwa wanapima DNA?Yaani unataka sampuki ije waanze kuhangaika kupima DNA ili wajue kama ni sampuli ya binadamu au mnyama?Sio sawa!Nadhani ilipaswa timu ya Rais kupeleka sampuli za binadamu!Walipaswa labda kupeleka sampuli za mtu mmoja ila kwa majina 10 tofauti ili kuona katika sampuli hizo kumi za mtu huyo huyo mmoja zitaleta majibu ya namna gani!

Unapochukua sampuli za wanyama na mimea,huwezi ukajua wana virus gani na hureact vipi pindi sampuli zao zinapoingizwa kwenye mashine za kupimia Covid 19!Usahihi nadhani ungekuwepo kama tungepeleka known specimen ya binadamu na kuchanganya vitu!

Pia nimlaumu Rais kwa kukimbilia kutoa shutuma kuwa anahujumiwa na Mabeberu kwa kushirikiana na wataalamu wa maabara ya taifa!Vp kama uchunguzi utakuja na majibu tofauti?

Atatoka hadharani kuomba radhi kama alivyotoka kushutumu?Kwanini asingesubiri awe na uhakika kwanza ndio aongee?
 
RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
666
1,000
Kwamba vipimo ndio tatizo au wanasayansi ndio wenye tatizo?
Wanasayansi ndiyo tatizo mkuu. Hii imetokana na kutokuwa na uzoefu(inexperience) na uelewa juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa sababu wao walikuwa wanafanyia kazi findings ambazo zimefanywa na wanaume wenzao(Wazungu).
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,587
2,000
Hao waliochukuwa sample za mapapai hawana utaalam ndiyo sababu tunasema huenda sample zilikuwa contaminated. Sasa unatumiaje hiyo hoja kwa sample zinachukuliwa na wataalam waliosomea kazi yao na wenye uzoefu, ondoa huo utetezi wako
Hawa kuwa disproove ni rahisi sana

Unamuambia twende mguu kwa mguu shambani kwangu huku camera zikichukua kila tukio halafu nichukue sample kisha nizipime then tuone kama kweli kila papai lina corona
 
Masi Lambo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
533
500
Ni jambo la kushangaza na kutia shaka kuona wataalam na wanasayansi wa Tanzania wanavyopinga uchunguzi wa Rais kwa hoja dhaifu.

Hii inatia shaka juu ya uwezo wa wataalam tulio nao hapa nchini.

Hebu tungalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais kwa jinsi wataalam wetu walivyozitolea maelezo.

1 vipimo ni Specific kwaajili ya kupima virus ama bacteria, hivyo huwezi kupima sample tofauti DNA/RNA hivyo basi hakiwezi kupima papai, lazima kitaleta majibu tofauti.!!

Hoja hii haina mashoka kama ni hivo kwa nini vipimo hivi vimetoa majibu ya positive na negative wakati sample sio sahihi??

Je wataalam wetu walijaribu kuvifanyia uchunguzi wowote hivi vifaa pindi vilipokaja kabla hawajaanza kuvitumia??
Kama hawakufanya kwanini waliviamini moja kwa moja, taaluma yao iko wapi hapi??

2 wataalam wengine wakaja na hoja kuwa majibu yanaweza kuwa positive kwasababu sample zinaweza kuwa zinamaambukizi (Contaminated) ama wakati wa kuchukua sample ama wakati wa upimaji hivyo kipimo kitatoa majibu Positive.!!

Okay.
Sasa kama ni hivi hamuoni hapo kuna uwezekano kuna watu ambao ni negative hawana maambukizi Ila kwasababu ya uzembe/ makosa wakati wa kuchukua sample ama uzembe wakati wa upimaji wakaiambukiza hiyo sample na kumpa mtu majibu ya positive kumbe Hana maambukizi?? Mtu unapewa ugonjwa ilihali huumwi.

Alafu hivi kama hiyo sample sio sahihi na imetoa positive kwasababu ipo Contaminated mbona sample za nanasi na kondoo zimetoa majibu negative??
Kwanini iwe negative wakati sample sio sahihi na haipo contaminated??

Hili limekaaje sasa wataalam? Inamaana kama inangekuwa haipo contaminated si ingetoa majibu kuwa haitambuliki (sample sio sahihi) kwanini Sasa ikatoa negative??

Halafu Inamaana team ya watafiti wa Rais hawakuwa na uelewa kabisaa kiasi kwamba wakazichukua sample tu ovyo ovyo bila ya umakini wowote na kuzipeleka tu zikapimwe hadi zinapata maambukizi??
Siamini kama ni wajinga kiasi hiki.

3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??

Hamuoni hapa kunatakiwa kufanyaka uchunguzi wa kina kama Rais alivyotilia shaka??

Kumbe sample zinakuwa contaminated hapo hapo maabara na kutupa majibu ya positive kwanini waachwe Sasa??.

Watanzania wenzangu Mimi kwa maoni yangu mh Rais anahoja ya msingi sana tusimpuuze, hawa wataalam wetu ndio wanatudanganya mh Rais yuko sahihi..

Kuna sehemu haiko sawa katika hili.

Kama una majibu ya maswali hayo uje hapa ulete ufafanuzi.
Asante sana, ubarikiwe hekima zaidi na zaidi, umesema bang on points with extra.
 
RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
666
1,000
Kabla hata ugonjwa haujaja hapa bongo, madaktari kutoka nje walikua wakitoa rai kua mgonjwa wa corona akigusa kitu chochote lazima aache virus.
Walisema lini? lete tuone hayo maandishi au video walizokuwa wanasema hivyo.

Kwanini wanasayansi wa wetu wasingefanya utafiti kuhusu hilo jambo mpaka wasubiri vidume vifanye na wao ndiyo waegemee humo humo. Wanasayansi wetu ni tatizo kubwa sana. Uelewa wao ni mdogo sana na hauendani na ukubwa wa matokeo yaliyo kwenye mavyeti yao na kwa namna wanavyovimba mtaani.
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,587
2,000
Wanasayansi ndiyo tatizo mkuu. Hii imetokana na kutokuwa na uzoefu(inexperience) na uelewa juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa sababu wao walikuwa wanafanyia kazi findings ambazo zimefanywa na wanaume wenzao(Wazungu).
Kwamba wanasiasa wanauzoefu kitabibu kiasi cha ku-criticize wanasayansi?

Hahaha put a joke a side

Hivi huyo mtabibu aliyepondwa kwa kutoa majibu hayo yaliyotokana na papai akisema anataka kujiridhisha hivyo awekewe camera ambazo zitarekodi kila tukio kisha watoke mguu kwa mguu hadi shambani achukie sample za mapapai kisha azifanyie vipimo.

Hivi unafikiri baada ya kufanyiwa test hilo papai jibu litalopatikana hapo litamdharirisha nani?
 
Ndondobwila

JF-Expert Member
Jun 9, 2015
562
500
Ubobezi wako katika tiss na propaganda usikufanye kuwa na wewe ni mwana sayansi. Mbwa we
Ni jambo la kushangaza na kutia shaka kuona wataalam na wanasayansi wa Tanzania wanavyopinga uchunguzi wa Rais kwa hoja dhaifu.

Hii inatia shaka juu ya uwezo wa wataalam tulio nao hapa nchini.

Hebu tungalie hoja hizi zilizotumika kupinga Uchunguzi wa Rais kwa jinsi wataalam wetu walivyozitolea maelezo.

1 vipimo ni Specific kwaajili ya kupima virus ama bacteria, hivyo huwezi kupima sample tofauti DNA/RNA hivyo basi hakiwezi kupima papai, lazima kitaleta majibu tofauti.!!

Hoja hii haina mashoka kama ni hivo kwa nini vipimo hivi vimetoa majibu ya positive na negative wakati sample sio sahihi??

Je wataalam wetu walijaribu kuvifanyia uchunguzi wowote hivi vifaa pindi vilipokaja kabla hawajaanza kuvitumia??
Kama hawakufanya kwanini waliviamini moja kwa moja, taaluma yao iko wapi hapi??

2 wataalam wengine wakaja na hoja kuwa majibu yanaweza kuwa positive kwasababu sample zinaweza kuwa zinamaambukizi (Contaminated) ama wakati wa kuchukua sample ama wakati wa upimaji hivyo kipimo kitatoa majibu Positive.!!

Okay.
Sasa kama ni hivi hamuoni hapo kuna uwezekano kuna watu ambao ni negative hawana maambukizi Ila kwasababu ya uzembe/ makosa wakati wa kuchukua sample ama uzembe wakati wa upimaji wakaiambukiza hiyo sample na kumpa mtu majibu ya positive kumbe Hana maambukizi?? Mtu unapewa ugonjwa ilihali huumwi.

Alafu hivi kama hiyo sample sio sahihi na imetoa positive kwasababu ipo Contaminated mbona sample za nanasi na kondoo zimetoa majibu negative??
Kwanini iwe negative wakati sample sio sahihi na haipo contaminated??

Hili limekaaje sasa wataalam? Inamaana kama inangekuwa haipo contaminated si ingetoa majibu kuwa haitambuliki (sample sio sahihi) kwanini Sasa ikatoa negative??

Halafu Inamaana team ya watafiti wa Rais hawakuwa na uelewa kabisaa kiasi kwamba wakazichukua sample tu ovyo ovyo bila ya umakini wowote na kuzipeleka tu zikapimwe hadi zinapata maambukizi??
Siamini kama ni wajinga kiasi hiki.

3 Wengine wanasema kuwa mh anawadharau wataalam, hana shukurani,anadanganya umma, anataka kuficha wagonjwa n.k.

Hii hoja haina mashiko.

Inakuwaje madaktari na wataalam wabobezi kabisa kwenye utafiti na vipimo unaletewa sample ya papai na fenesi unaambia ni ya binadamu halafu unakubali na kwenda kuipima??

Hii inatoa picha kuwa wataalam wetu wanalipua lipua tu na hawako makini na kazi yao, kama wako makini hili linawezekanaje??

Hamuoni hapa kunatakiwa kufanyaka uchunguzi wa kina kama Rais alivyotilia shaka??

Kumbe sample zinakuwa contaminated hapo hapo maabara na kutupa majibu ya positive kwanini waachwe Sasa??.

Watanzania wenzangu Mimi kwa maoni yangu mh Rais anahoja ya msingi sana tusimpuuze, hawa wataalam wetu ndio wanatudanganya mh Rais yuko sahihi..

Kuna sehemu haiko sawa katika hili.

Kama una majibu ya maswali hayo uje hapa ulete ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
17,587
2,000
Walisema lini? lete tuone hayo maandishi au video walizokuwa wanasema hivyo.

Kwanini wanasayansi wa wetu wasingefanya utafiti kuhusu hilo jambo mpaka wasubiri vidume vifanye na wao ndiyo waegemee humo humo. Wanasayansi wetu ni tatizo kubwa sana. Uelewa wao ni mdogo sana na hauendani na ukubwa wa matokeo yaliyo kwenye mavyeti yao na kwa namna wanavyovimba mtaani.
IMG_20200505_172413_553.JPG

Soma mwenyewe hapo inaonekana vya wazungu unavikubali sana, sa sijui na hawa utawapinga

Halafu kuhusu wansayansi kufanya utafiti, jiulize tu mwenyewe watakua na uhuru huo katika serikali hii? wakati swala la kutoa taarifa za wagonjwa tu limewatoa imani?
 
RAYAN THE DON

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
666
1,000
Kwamba wanasiasa wanauzoefu kitabibu kiasi cha ku-criticize wanasayansi?

Hahaha put a joke a side

Hivi huyo mtabibu aliyepondwa kwa kutoa majibu hayo yaliyotokana na papai akisema anataka kujiridhisha hivyo awekewe camera ambazo zitarekodi kila tukio kisha watole mguu kwa mguu hadi shambani achukie sample za mapapai kisha azifanyie vipimo.

Hivi unafikiri baada ya kufanyiwa test hilo papai jibu litalopatikana hapo litamdharirisha nani?
Hahahahahhh

Mkuu ni aibu, dharau na dhihaka sana kukosolewa na mwanasiasa ambaye hana elimu uliyonayo. Mtu umekaa miaka 7 unasomea taaluma fulani halafu leo hii unadhalalishwa unakaa kimya?

Kama alichofanya mwanasiasa ni uongo basi hao wanasiasa waje na findings zitakazosheheni ukweli mtupu.
 
Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,958
2,000
Mkuu umejiuliza maswali mazuri sana, ni kweli kwa tanzania kila kitu kipo , yaani wataalamu uchwara na orona pia ipo.

Mashaka zaidi ni kwamba kama hao waliopima hizo sample ndio walio bora na wanafanya kazi katika taasisi ya raisi basi mashaka ni makubwa zaidi hata kwa usalama wake.

Hata hivyo ndio maana tunaona viongozi wengi sana wakiondoka nchini na kwenda kutibia nje ya nchi sababu ya hali ya uzembe uzembe kama hii.

pande zote zina hoja ya msingi kabisa ya kulaumiwa mpaka raisi mwenyewe maana wale ni watendaji wake.
Nipo atumishi hewa walondolewa kwa mbwembwe za kutosha,ajira sasa hivi ni chache,ikawaje wawepo watumishi fake?Huu uwajibikaji na uchunguzi unatakiwa upanuliwe na isiwe maabara pekee.Tuanzie State House, TAMISEMI,Wizara ya Afya,Laboratory Personnel, Procurement Departments,msd,Supplier wa Test Kits nk.
Nchi hii likibuma hatukosi mbuzi wa kafara na Praise Team wapi busy to clean mess.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom