Hebu soma ufunguke - mji huu unatisha sasa

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Jamani,
Hii inatisha sana. Inabidi tuogopane sana!

Habari ya kweli iliyotokea wiki iliyopita

Kuna dada mmoja anasoma chuo buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule. Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa lugaro hospitali na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli. Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu vizuri.

Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita, kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.

Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada, ikabidi awahishwe mwananyamala hospitali, ikaoneka itumika sumu kufanya awe hivyo! lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo regency hosp. hivyo akawahishwa regency na kupata matibabu.

Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa,tigo pesa na bank ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.

Na bank walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha. Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.

Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu, akimwambia ‘’kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye.
Chukua taadhari...........................
 
Mmmh huyu kama wa pili nasikia kuna mwingine nae alikuja humu na kusema kuwa hao watu walimtokea pale quality center wakadai wanataka ongea nae yaani wanasgida na kampuni yao, yule mdada alikuwa a gari ya kampuni baana wakapanga wakutane peacock wakaenda dada kajikuta quality kachoka atm card zimeenda zote na password aliwapa mwenyewe.
Hii dar si salama watu wanakula kwa kuangalia hakuna kuamini mtu hapa
 
mmmh huyu kama wa pili nasikia kuna mwingine nae alikuja humu na kusema kuwa hao watu walimtokea pale quality center wakadai wanataka ongea nae yaani wanasgida na kampuni yao, yule mdada alikuwa a gari ya kampuni baana wakapanga wakutane peacock wakaenda dada kajikuta quality kachoka atm card zimeenda zote na password aliwapa mwenyewe.
Hii dar si salama watu wanakula kwa kuangalia hakuna kuamini mtu hapa

tuomba mungu na kuwa waangalifu!!!
 
... sasa inabidi tufunguke kweli, kama mtu ataanza kuona dalili zozote kama zilizotwa, ni bora kuchukua hatua mapema kabisa...
 
......hao watu wanapata taarifa za mtu kupitia mtu wa karibu nae.....na polisi kwa nini hawachukui hatua? Wanapewa cha juu??...........
 
Nimeshuhudia jamaa zangu wawili wametapeliwa laki sitasita hivi hivi, huu utapeli upo sana mjini hapa
 
Dah! Mjini shule
Watu wanajichukilia tu pesa bila jasho
 
Ila huyo dada hakuwa na sababu yoyote ya kukutana na huyo jamaa. Kama alifika hadi hapo chuo, whatever he couldnt ask her on the phone si angeenda mapokezi huko. Huyo dada yuko na wenzie, anaenda kukutana na jamaa alone ili aulizwe kuhusu chuo? Yeye ni shareholder hapo chuoni?

huu ujeuri wangu namshukuru Maulana manake unaniweka safe siku zote. Pole yake. Afadhali wamemuibia kuliko wangembaka.
 
Tatizo na nyinyi wapolipoli mnaingia kwakasi sana mjini hapa mpaka hajulikani nani mzawa nani mchunga mbuzi bakini makwenu jama daa ime jaa
 
Ndio maana ya kuitwa bongo! Watu wanakula kwa kutumia ubongo sasa ww ukitumia tope badala ya akili utaliwa hata ningekuwa mm. Alafu kaeni mkijua kuwa kila mtu bongo ni mwizi ni kwakuwa hatujapata nafasi au vitengo na wengine arobaini zao hazijafika. Ashukuru mungu hajafa. So take care guys.
 
Ila polisi wetu wanafahamu fika hao watu!!! Cha kusikitisha wale wanaokaba watu pale Gymkana polisi wa Salender wanawafahamu fika na hawawakamati!!! Mtandao mkubwa huo na unalindwa!!
 
Ila polisi wetu wanafahamu fika hao watu!!! Cha kusikitisha wale wanaokaba watu pale Gymkana polisi wa Salender wanawafahamu fika na hawawakamati!!! Mtandao mkubwa huo na unalindwa!!

ili la polisi kuwafahamu ni kweli, kuna jamaa alikabwa akawatishia bastora wakakimbilia kwenye maji
 
Mjini hapa sitakagi eti nimekuta miscal ah ah utaishia kukutusi tu niko makini aise wacha we sitaki hata salamu ya mtu.
 
Lakini pia kwa nini mtu utembee na kadi zako zote za benk, kama unazo mbili au zaidi tembea na moja zingine acha nyumbani. Yaani kuna watu wallet zao zimejaa kadi na vitambulisho vyote alivyonavyo duniani hapa; e.g kadi zote za benki, cha ajira, bima ya afya, leseni ya gari( mpya na ya zamani), kadi ya kupigia kura, cha shule/chuo hata kama alishamalisha chuo, ma- business cards kibao, mwisho kabisa unakuta ana eflu mbili mia saba kwenye hilo wallet.
 
Back
Top Bottom