Hebu soma halafu niambie ni sahihi au sio sahihi?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,731
21,133
Amani kwako.

Huko kwa wakoloni ikiwepo Marekani huwezi kumtuma mwanamke akulete maji ya kunywa au kumwagiza mtu na wewe umekaa tena ume-relax, maana yake kila kitu anajihudumia mwenyewe hakuna utumwa wa kuamrishana.

Wala Marekani huwezi kumkaripia mwanamke faini yake ni inafikia laki 600,000 za Kitanzania.

Wala huwezi kutema mate chini faini yake utatoa 260,000 za Kitanzania.

Wale wenye subwoofer ukifungulia mziki wako na sauti kutoka nje ya dirisha kama huko uswahili, Kwa Mrombo, Kijenge au Manzese na Mbagala kesi yake itakuchukua mwezi kuimaliza na faini juu pamoja na kuhamishwa katika eneo hilo kwa nguvu.

Haya kina Mwamposa na wachungaji wengine, ukipitilizisha masaa 2-3 ya ibada kanisani au mskitini kufanya hivyo unaweza kubaki mwenyewe na ibada yako au kuwalipa waumini muda uliowapotezea kushinda kanisani.

Wazee wa michepuko, huwezi kuomba simu ya mkeo ili uichunguze ni kosa kubwa sana la kuingia faragha ya mtu unaweza kumlipa kabisa.

Haya wabongo, unadhani ni sheria gani ije itumike hapa Tanzania?
 
Hizo sheria za ndoa zikija BONGO basi wanawake hawataolewa kabisa.
Nimeipenda hii hapa aseee 👇:

Ukipitilizisha masaa 2-3 ya ibada kanisani au mskitini kufanya hivyo unaweza kubaki mwenyewe na ibada yako au kuwalipa waumini muda uliowapotezea kushinda kanisani.
 
Privacy na uhuru wa mtu mmoja mmoja ni jambo kubwa la kujifunza kutoka kwa wenzetu., mengi uliyozungumza mleta uzi yana ukweli hasa kwa nchi ulaya na marekani.
 
Hivi ndivyo mnavyodanganywa ili muone sheria zenu kandamizi zina afadhali.
Mkuu huko ughaibuni na hasa uingereza na marekani sheria zao zikoje hasa kwenye hayo yaliyoainishwa na mleta mada?
 
Back
Top Bottom