Hebu pata picha ingekuwa wewe unaishi maisha wanayoishi hawa wenzetu wenye uhitaji maalumu

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,723
10,008
Mungu atukuzwe kwa yote aliyoyaumba kwa kuwa hata vilivyo dhaifu huviimarisha kwa namna yake.

Hebu mfano wewe uliye na kila kiungo mwilini vikiwa timilifu katika utendaji kazi; siku moja inatokea kubadilishana uzoefu na walionyimwa labda kuona au kusikia mfano; {mfano si kwa nia mbaya}

- Kipofu " anasikia tu sauti bila kujua sauti inatokea kwenye kitu kinafananaje. Utasikia tu watu wakicheka, wakilia, bila kujua nini wanalilia/chekua/ongelea kinafanana vipi.

- Kiziwi" Unaona tu bila sauti. Ni kama vile unaangalia televisheni ikiwa MUTED. Hivyo hivyo na kwa ulemavu wengine. Maisha yao wanayoishi ni kama wako kwenye ulimwengu wao pekee yao.

Watu wa namna hiyo kwa kweli wanahitaji sana upendo na msaada mkubwa toka kwetu tulio wazima. Wanapitia mengi sana magumu maishani mwao. Hata kidogo tusijilinganishe majaribu yanayotupata sisi na wao. Tusiwe watu wa kujigamba sana na kujiona kwamba sisi ni so special tukutanapo na watu wenye uhitaji maalumu tuwasaidie kwa upendo na sio kwa matusi wala kejeli.

Ninaweza kujikuta sijaeleweka kwa wengi nini ninataka kuelezea lakini nimejitahidi kufikisha ujumbe hata kwa walio wachache walionielewa.

Tupendane na kusaidiana bila kujali jinsia wala muonekano wa mtu kwani kila mtu anajua ni magumu gani anayapitia maishani mwake ambayo kwa mtu mwingine ni ngumu kuyabeba.

Nipende kuwatakia maandalizi mema ya kufunga na kufungua mwaka mpya 2021. Heri nyingi kwenu nyote mwenyezi Mungu atujalie kuushuhudia mwaka ujao.
 
“Tupendane na kusaidiana bila kujali jinsia wala muonekano wa mtu kwani kila mtu anajua ni magumu gani anayapitia maishani mwake ambayo kwa mtu mwingine ni ngumu kuyabeba”.
 
Back
Top Bottom