GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,516
- 108,791
- Thread starter
- #41
Ghadafi alikua mtu wa hovyo tu, yaani kisa umenilipia mahari, umenipa nyumba na umeniwekea pesa kwenye account bila ya kuvifanyia kazi basi niendelee na maisha tu. Yaani kama nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa au mwanasiasa nifute hizo ndoto sababu tu naoa, nakula na kulala kwenye nyumba nzuri!!
Kwa mbongo huyo ndiyo kiongozi
Kama ikitokea nikaambiwa nichague JamiiForums Members Kumi ( 10 ) tu ninaowakubali kwa 100% kuwa wana ' IQ ' kubwa basi Wewe na Bila bila hamtakosekana katika hiyo idadi. Na sikusifii hivi au siwasifieni hivi labda nikimaanisha kuwa huwa mnakubaliana na ' Mabandiko ' yangu hapana kwani kuna ' Mabandiko ' yangu mengine huwa tunapishana ' Kimtizamo ' ila ninachopenda Kwenu nyie ni kwamba mnajua sana Kujenga Hoja na Kuzitumia vyema kabisa ' akili ' zenu katika ' Uwasilishaji ' wa masuala mbalimbali hapa Jamvini.