Hebu nijulisheni uwiano gani umetumika kwa Chadema iliyoambulia mbunge mmoja iweze kupata viti maalum 19 na CCM iliyojizolea viti 262 kupata viti 94?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Hesabu hii imenipiga chenga kujua NEC imetumia uwiano gani katika utoaji wa wabunge wa viti maalum kwa Chadema kupewa "offer" ya kupeleka wabunge Wa viti maalum 19 wakati CCM iliyojizolea viti 262, karibia ya viti vyote vya ubunge nchini, iweze kupata viti maalum 94?

Kuuliza siyo ujinga, naomba tu nieleweshwe ni "ratio" gani imetumika ya kukokotoa kupata idadi hiyo ya wabunge?
 
Kwa kadri ya ufahamu wangu, wabunge wa vitu maalum hupatikana kutokana na idadi ya kura za wabunge kilizopata chama cha siasa.

Hawatokani na idadi ya wabunge mlioshinda, sasa kwa hesabu ya Mahera wabunge wa upinzani waliokuwa wanapigiwa kura nyingi baada ya CCM ni wagombea wa Chadema, hapo ndipo walipoambulia hivyo viti maalum (niko tayari kusahihishwa)
 
Nashukuru kwa kunipa ufafanuzi.

Mimi nilidhani hiyo "ratio" wameilazimisha baada ya kuona kuwa zile Kamati za Bunge, ambazo zimewekewa masharti kuwa ni lazima ziongozwe na wapinzani, ndiyo ikawafanya hao NEC waje na kikotoo hicho
 
Kanuni ni hii.
Chukua idadi ya kura za wabunge wa vyama vilivyopata zaidi ya asilimia tano kisha ujumlishe upate jumla.Kisha chukua idadi ya viti maalum vinavyotakiwa tuseme labda 20 na hatimaye fanya kanuni hii
(X/(X+Y))×20
X ni idadi ya kura za wabunge wa Chadema.
Y ni idadi ya kura za wabunge wa CCM.
20 ni namba ya kufikirika yaani idadi ya viti maalum zinazogombaniwa.
Z ingeweza kuwepo endapo kuna chama kingepata kura asilimia tano na kuendelea
 
Kanuni ni hii.
Chukua idadi ya kura za wabunge wa vyama vilivyopata zaidi ya asilimia tano kisha ujumlishe upate jumla.Kisha chukua idadi ya viti maalum vinavyotakiwa tuseme labda 20 na hatimaye fanya kanuni hii
(X/(X+Y))×20
X ni idadi ya kura za wabunge wa chadema.
Y ni idadi ya kura za wabunge wa CCM.
20 ni namba ya kufikirika yaani idadi ya viti maalum zinazogombaniwa.
Z ingeweza kuwepo endapo kuna chama kingepata kura asilimia tano na kuendelea
Nashukuru kwa ufafanuzi wako

Hata hivyo inaonekana namna gani walivyofanya huo wizi wao Wa kura "kishamba" kabisa kwa huyo mshindi Wa pili kuambulia kupata kiti kimoja pekee cha ubunge Wa kuchaguliwa, tena kwenye jimbo ambalo wao CCM wameliona siyo tishio kwao
 
Wewe umeleta mada uelimishwe watu wanajitahidi kukuelimisha Sasa umegeuka mjuaji kuliko wanaokuelimisha kwa kutoka nje ya mada !!! Baki na li mada lako
 
Kwa kadri ya ufahamu wangu, wabunge wa vitu maalum hupatikana kutokana na idadi ya kura za wabunge kilizopata chama cha siasa.

Hawatokani na idadi ya wabunge mlioshinda, sasa kwa hesabu ya Mahera wabunge wa upinzani waliokuwa wanapigiwa kura nyingi baada ya CCM ni wagombea wa Chadema, hapo ndipo walipoambulia hivyo viti maalum (niko tayari kusahihishwa)
Na ruzuku hupigwaje kujua chama kipi kitapata shilingi ngapi?
 
Kwa kadri ya ufahamu wangu, wabunge wa vitu maalum hupatikana kutokana na idadi ya kura za wabunge kilizopata chama cha siasa.

Hawatokani na idadi ya wabunge mlioshinda, sasa kwa hesabu ya Mahera wabunge wa upinzani waliokuwa wanapigiwa kura nyingi baada ya CCM ni wagombea wa Chadema, hapo ndipo walipoambulia hivyo viti maalum (niko tayari kusahihishwa)
Kwa sheria ipi
 
Hesabu hii imenipiga chenga kujua NEC imetumia uwiano gani katika utoaji wa wabunge wa viti maalum kwa Chadema kupewa "offer" ya kupeleka wabunge Wa viti maalum 19 wakati CCM iliyojizolea viti 262, karibia ya viti vyote vya ubunge nchini, iweze kupata viti maalum 94?

Kuuliza siyo ujinga, naomba tu nieleweshwe ni "ratio" gani imetumika ya kukokotoa kupata idadi hiyo ya wabunge?
Wametumia hesabu za kugawanya, kwenye orodha ya wagombea urais CCM wapo juu ova Chadema wapo chini, CCM ÷ Chadema = 19.
Probably NEC's principle.
 
Back
Top Bottom