Hebu kumbuka tulikotoka, bongo fleva ni mtoto wa jana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu kumbuka tulikotoka, bongo fleva ni mtoto wa jana

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by galagaja mtoto, May 30, 2012.

 1. galagaja mtoto

  galagaja mtoto Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1]TUNDA[/h] Sheria na mila zetu, utokapo utotoni watambulika na watu, waingizwa ukubwani, waitwa mzima mtu, kisa ndevu kidevuni, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kundi kubwa kijijini, wengi wao ni vijana, pinde ziko mkononi, visu tulinoa jana, twaelekea porini, kwenda kusaka amana, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Safari imekolea, mikono watupungia dua wanatuombea wengine watulilia, msitu twauendea, kijiji twakiachia, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Safari hii hakika uvumilivu yataka, inagharimu miaka na miongo kukatika, Huusisha kinakaka , na wadada kadhalika, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Sekunde dakika siku, miezi kufika mwaka, mchana hadi usiku, amana tunaisaka, zunguka huku na huku wengine wameshachoka, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kila tunakopitia, mengi tunajionea, wengine wanabakia vizuri kijibebea, wachache tumebakia safari kuendelea, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Ilifika siku moja nilibakia mwenyewe, zaidi ya mia moja walishaweka vijiwe, nikaona tunda moja lisilo na mfanowe, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Kwa hakika tunda hili limependeza mtini, hajaliona tumbili lisingedumu mtini, napiga hatua mbili nasogelea mtini, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Wenzangu walio nyuma wamejenga na vibanda, kwa bahati ya karima familia wameunda pekee nimesimama, nalitaka lile tunda, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Nachukua mawe yangu nilishushe lile tunda, na mimi dhamira yangu kusimamisha kibanda, kama wlivyo wenzangu , familia kuiunda, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Mojamoja natupia jiwe kwenye tunda lile, na tena nalisifia, tunda lapendeza lile, tena limejiivia nalipenda ili nile, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Mwili wote umechoka tunda ninalililia, ni mitano sasa miaka mawe ninalitupia, nami pia kwa hakika moyoni nimelitia, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Si chungwa wala si embe sio epo sio dafu, nikiufanya uzembe, naweza geuka mfu, lafanana na kiumbe mwenye baba mtukufu, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa. Jamani nakaa chini pekee nimebakia, panatisha msituni, lakini ninayo nia, njia nyiongine nipeni nipate kulitungua, kila nikitupa jiwe tunda hili nalikosa.
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280

  Pole sana ndugu yangu, kwa uchovu ulopata,
  Kweli yatia uchungu, kwa tunda kutolipata
  Yote mkabidhi Mungu, neema ataileta
  Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

  Kwa tunda lilio zuri, shida sana kulipata,
  Walifungia safari, Ubungo hadi Msata,
  Kwani ni tamu na zuri, gharamia hutosita,
  Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

  Ongeza yako juhudi, na tamaa kutokata,
  Itafikia kipindi, hilo tunda utapata,
  Unahitaji ufundi, ili upate livuta
  Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

  Pindi ukirusha jiwe, pia jaribu kuita,
  Lahitaji lisifiwe, kwa maneno yenye nta,
  Na ulimi utumiwe, ili kuweza livuta,
  Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

  Na bado nasisitiza, kwa tama kutokata,
  Lala kesha ukiwaza, mbinu mpya utapata,
  Tabasamu liwe kwanza, hakika utalipata
  Tunda zuri siku zote, linajificha mibani

  =========================================


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...