Hebu jikumbushie 'Siku ya Gulio Katerero'

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Shule za Msingi ( UPE )Category:Common Interest - HistoryDescription:
Ushawahi kusoma shule za kukimbia mchakamchaka, kwenda na kidumu cha maji na mfagio mkononi? Kama ndio basi kundi (Group) hili linakufaa.

Hebu jikumbushie haya:

1. Bulicheka na nduguze
2. Mr. & Mrs. Daudi
3. Fikiri na Sadiki
4. Linda amwokoa Kapilima
5. Siku ya gulio katerero
6. Tola anakula gizani
7. Twende tukawinde Ngedere
8. Kibanga ampiga mkoloni
9. Nanzoge anapika.
10. Mafuriko ya mto Rufiji
11. Pazi na jogoo

Waweza ongezea na wewe.

Kama ulisoma academy school, huambulii...
Lazima ujifunze:

1. Sayansi Kimu
2. Uraia
3. Sanaa

Wakati wa mapumziko lazima ucheze,

1. Mpira (Chandimu, one touchi, mputo)
2. Netboli na rede
3. Mdako
4. Bong'oa
5. Kula m'bakishie baba
6. Kubanjua Gololi

Msosi wakati wa mapumziko.

1. Mihogo ya kukaanga na chachandu
2. Aishiklimu
3. Barafu
4. Kashata
5. Bagia (za walimu)
 
Juma na Rosa
Safarri ya Chalinze
Mr. all of you
Cha wote
Sizitaki mbichi hizi
Karudi baba mmoja
Ahadi 10 za MwanaTANU (Std. III)
 
Jogoo aliyesema.
Lindu amwokoa Kapilima.
Kula mno ni hasara.
Kijiji chetu.
Safari yenye mkosi.
palikuwa na watoto 10, wakaenda kutafuta kuni, mmoja kapotea huko wakabaki 9.
Palikuwa na watoto 9,wakenda kuoga mtoni, mmoja akatumbukia,wakabaki 8.
Palikuwa na watoto 8...
...zilikuwa siku njema sana zile!
 
unavaa kaptula 3 kukwepa bakora zisikuingie mwilini tena za jeans au unaweka maboksi na makaratasi kwenye makalio duh!zamani bakola zilikuwa zinatembea sana!
 
Shule za Msingi ( UPE )Category:Common Interest - HistoryDescription:
Ushawahi kusoma shule za kukimbia mchakamchaka, kwenda na kidumu cha maji na mfagio mkononi? Kama ndio basi kundi (Group) hili linakufaa.

Hebu jikumbushie haya:

1. Bulicheka na nduguze
2. Mr. & Mrs. Daudi
3. Fikiri na Sadiki
4. Linda amwokoa Kapilima
5. Siku ya gulio katerero
6. Tola anakula gizani
7. Twende tukawinde Ngedere
8. Kibanga ampiga mkoloni
9. Nanzoge anapika.
10. Mafuriko ya mto Rufiji
11. Pazi na jogoo

Waweza ongezea na wewe.

Kama ulisoma academy school, huambulii...
Lazima ujifunze:

1. Sayansi Kimu
2. Uraia
3. Sanaa

Wakati wa mapumziko lazima ucheze,

1. Mpira (Chandimu, one touchi, mputo)
2. Netboli na rede
3. Mdako
4. Bong'oa
5. Kula m'bakishie baba
6. Kubanjua Gololi

Msosi wakati wa mapumziko.

1. Mihogo ya kukaanga na chachandu
2. Aishiklimu
3. Barafu
4. Kashata
5. Bagia (za walimu)[/QUO

Ubuyu...
Viazi vya kukaanga
 
"Huyu ni Baba. Baba ni mnene. Baba ana ng'ombe. Ng'ombe wake ni mweusi. Baba anasema kimbia ng'ombe, kimbia upesi, kimbia nyumbani, baba ana njaa".
 
they were great and memorable times though. Vitabu vilichuwa vinaelimisha, kuburudisha. Hakika vilibeba ujumbe mzito na vilitukuza utaifa. I wish watoto wa siku hizi wavisome na kuacha vitabu vilivyotungwa na wakenya na waganda just 4 the sake ya kujua kingereza!
 
Hapo kuna kuwahi number asubuhi,ukaguzi siku ya alkhamisi na band ya shule.

I see umenikumbusha mbali sana!

Kwa wale waliofika Nansio, nilikuwa naishi Nakatungulu (karibu na Motel Galu ya UDECO - enzi hizo, sijui kama bado ipo!) na shule nasome Bukongo, kisha kuwahi namba saa 1 asubuhi! Hapo kuamka ni saa 10 afajiri na mwendo ni mchakamchaka.
 
ukiwahi unakimbilia kuchota maji mtoni then kumwagilia mchicha na maua mwalimu anapima kwa kuchomeka fimbo kama kimelowa sasa ole wako aone hakijaloana maji hayajafika chini pia tulikuwa tunaagizwa mbolea ya mavi ya ngombe,kuku na mbuzi pia udongo uliooza na miradi ya shule kuuza mapera ya shule dah!enzi hzo ilikuwa raha sana!
 
Kula mno ni hasara. .....Akapewa nyama akala akamaliza, Akapewa asali akala akamaliza, Akapewa........... akamaliza. mara akasikia ubavu PU. wakachinja ng'ombe wakamfungia ngozi. waikumbuka hiyo? nilikuwa nikifikia kusoma pu naitamka kwa nguvu zote.

Sasari ya kwenda mtwara,
Maadui wa binadamu,
Heri mimi sijasema,
Manenge na Mandawa,
Pia kuna moja jamaa alitobolewa sikio na ndama akawa anajiuliza jinsi gani atamweleza mumewe heading siikumbuki.

Ama kweli vitabu vya zamani vilikuwa burdani kwelikweli.:teeth:
 
I see umenikumbusha mbali sana!

Kwa wale waliofika Nansio, nilikuwa naishi Nakatungulu (karibu na Motel Galu ya UDECO - enzi hizo, sijui kama bado ipo!) na shule nasome Bukongo, kisha kuwahi namba saa 1 asubuhi! Hapo kuamka ni saa 10 afajiri na mwendo ni mchakamchaka.
Bado ipo. Vipi ulikuwa unapitia mtaa wa uhindini kwa kina gandecha, sengula n.k. Anyway yako hiyo ilikuwa fair sana, maana kuna nguli mmoja alikuwa anatoka nakatungulu hadi kagunguli akiwa mido skuu.
 
Wakuu posts zote hapa zimenisisimua sana. Watoto siku hizi hawafaidi. Darasa la sita kama sijasahau kitabu cha Kiswahili kilikuwa na sura "Kutembelea Uwanja wa Ndege." Tulipata nafasi ya kutembelea uwanja wa ndege kutokana na juhudi binafsi za Mwalimu wetu Emmanuel Mbelele. Napenda kuonesha shukrani zangu kwake. Naamini nimekuwa na wakati mzuri sana katika maisha ya utotoni. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ofa hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom