Hebu geukeni mabubu nchi itawalike kirahisi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
Hebu geukeni mabubu nchi itawalike kirahisi

Christopher Nyenyembe
Tanzania Daima

KAMA ilivyo ada, mara nyingi napenda sana kuifikiria hadithi ya Mfalme wa Mauritius (Muris) jinsi alivyofanikiwa kurithiwa na watoto watatu waliotoka kwenye familia masikini, lakini walikuwa na uwezo wa ajabu.

Hadithi hiyo inajaribu kumwonyesha wazi mfalme huyo kuwa himaya ya kifalme na watu anaowatawala alifanikiwa kukalia kiti hicho si kwa matakwa ya mfalme baba yake aliyemrithi wala watu wa nchi hiyo.

Kikubwa kilichojitokeza kwenye hadithi hiyo ni siri kubwa aliyokuwa nayo mama mzazi wa mfalme wa Mauritius, siri ambayo hakuweza hata siku moja kumweleza mwanawe kuwa ndani ya jumba la kifalme kuna walakini, kuna kasoro kubwa.

Mama huyo hata siku moja hakudiriki kumweleza mwanawe kuwa ufalme wake una walakini na umezongwa na kila aina ya ujanja na uficho kwa wananchi wa nchi hiyo ili wasiweze kufahamu kuwa mtawala wao ana walakini.

Siri hiyo iliendelea kujikita ndani ya moyo wa mama huku mwanawe akifikiria upya kuandaa mrithi wake kutoka miongoni mwa watoto wake watatu wa kiume na alipata wakati mgumu wa kumpata mtoto mwema na mwadilifu kwa kuwa watoto hao wote wa mfalme walikuwa wamejikita kwenye vitendo vya ufisadi.

Watoto hao watatu wa mfalme waliweza kutumia vibaya mali za nchi hiyo na hawakuweza kuwajali masikini, walijineemesha jinsi wanavyotaka huku wakitawanya vito vya thamani kwa makahaba na marafiki zao, ili wapendwe zaidi, lakini waliinyong’onyeza himaya ya baba yao.

Walisababisha watu waliokuwa wakimpenda mfalme huyo na kumheshimu kwa kila kauli aliyokuwa akiitoa, walianza kumsema vibaya na kila alipokuwa akipita na kuwapungia wananchi wake mikono walimwitikia, lakini hawakupenda tena kumuangalia usoni kwa kuwa anawalinda watoto wake mafisadi.

Himaya ya mfalme huyo ilizidi kukumbwa na mikasa mingi na kusababisha wananchi waanze kupaza sauti zao juu wakimtaka mfalme huyo awatendee haki kama alivyokuwa akifanya marehemu babu yao huku wakilalamika kuwa wanateseka na mwenye uwezo wa kuwakomboa ni mfalme mwenyewe na sio watoto wake waliogubikwa na kashfa.

Mfalme wa Mauritius alipoona anasakamwa sana na wananchi wake na himaya ya kifalme ikiendelea kupoteza heshima yake, ndipo alipoanza kutumia nguvu ya majeshi na vyombo vingine vya dola ili kuweza kuwanyamazisha wananchi wanaolalamikia watoto wake.

Aliwataka wafunge midomo na kuomba kila mwenye shida aonane na wasaidizi wake watakaotoa majibu ya malalamiko ya wananchi, hatua hiyo iliitikiwa na watu wengi na kila siku nje ya jumba la kifalme kulijaa watu wenye shida na vilio vilitawala, kila mmoja aliyepewa nafasi ya kueleza shida yake alilalamikia ufisadi wa watoto wa mfalme.

Kazi ya kupokea malalamiko ya watu ilikuwa ngumu, ulifika wakati wasaidizi wa mfalme huyo wakachoka na kumshauri awaeleze ukweli wananchi juu ya vitendo vya ubadhirifu wa mali za nchi vinavyofanywa na watoto hao na awachukulie hatua kali, vinginevyo wananchi wakiendelea kulalamika watajichukulia sheria mikononi na kuiteka himaya ya mfalme.

Wakati mfalme akiwaza hilo ndipo walipojitokeza watoto watatu kutoka katika familia ya kimasikini na kuomba waingie kwenye jumba la kifalme kwa madai kuwa safari ndefu ya siku 70 waliyotembea kwa miguu siku, walikuwa wanakwenda kwa mfalme huyo kwa nia ya kumrithi na ndivyo walivyoweza kuwaeleza wasaidizi wa wafalme huyo.

Taarifa za mfalme huyo kutaka kurithiwa na vijana hao watatu masikini zilimshtua kwa kiasi kikubwa na ili wasiweze kutimiza lengo lao aliamuru wakamatwe kisha wahojiwe sababu za kutaka kurithi huku wakijua wazi kuwa hawajatoka kwenye familia ya kifalme.

Mfalme huyo alisahau kuwa alikwishatoa amri ya kuwataka watu wake wasiseme lolote kuhusu ufisadi wa watoto wake na alipojaribu kupokea maoni kupitia kwa wasaidizi wake malalamiko na lawama zote bado zililenga kuitumbukiza himaya yote kwenye dhuluma na ufisadi uliopindukia.

Ndipo alipoona umuhimu wa kuwasikiliza vijana hao watatu masikini ambao kwa pamoja waliweza kumwambia mfalme kuwa ufalme wake una walakini, wali anaokula mfalme una walakini na mbuzi aliyechinjwa kwa kitoweo naye pipa ana walakini, hivyo wameona ni vyema wamrithi.

Kauli za vijana hao zilimshtua mfalme huyo ndipo alipomwita mama yake mzazi akimtaka aeleze kwa nini kaambiwa kuwa ufalme wake una walakini hatua iliyomfanya mama yake akiri na kudai kuwa wakati anaolewa aliingia kwenye jumba la kifalme akiwa na mimba ya mwanaume mwingine, hivyo ufalme alionao ni batili.

Akahoji kuhusu wali kuwa na walakini ndipo alipoelezwa kuwa wali anaokula mpunga wake alipandwa bondeni eneo la makaburini ambako hakujawahi kulimwa ndiyo maana punje zake ni nene na kukiri kuwa walikosea kumlisha mfalme mpunga uliolimwa makaburini.

Kuhusu walakini wa mbuzi aliyechinjwa kwa ajili ya mfalme walikiri kuwa mbuzi huyo alipozaliwa siku hiyo hiyo mama mbuzi alikufa ndipo walipoamua kuendelea kumnywesha maziwa ya punda na kunona kwake kulisababishwa na maziwa hayo kama alivyoweza kuelezwa ukweli na vijana hao wenye akili na maarifa na mwisho walifanikiwa kumrithi mfalme wa Mauritius.

Hadithi hii inaonyesha chimbuko la utawala na nafasi za watawala katika nchi pale wanaposhindwa kuwaridhisha wananchi wao kwa jambo ambalo wanaamini kabisa kuwa linahitaji majibu mazuri na ya haraka ili kuweza kuwaondolea wananchi kitu ambacho wanaamini kabisa sauti ya mwisho kwa kila jambo lenye utata lazima itolewe na kiongozi wa nchi.

Tanzania hivi sasa imekumbwa na jinamizi kubwa la wanasiasa wanaotupiana tuhuma nzito za ufisadi na rushwa zinazodaiwa kufanywa na watendaji wa serikali hali iliyowaweka wananchi njia panda, wengi wakitaka kufahamu ukweli wa tuhuma hizo na msimamo wa serikali kuhusu watendaji wanaotuhumiwa.

Ni vigumu hivi sasa wananchi kugeuka mabubu na viziwi ili wakubali mjadala huo ulioibuliwa ili ufungwe kimya kimya bila wahusika kuchukuliwa hatua zozote, nikimaanisha kuwa umefika wakati ambao serikali haipaswi kufananishwa na watoto wa mfalme wa Mauritius.

Umefika wakati Rais Jakaya Kikwete anaopaswa atumie nguvu zake binafsi kutambua kuwa ufisadi unaodaiwa kuwapo kwa baadhi ya watendaji wake unapaswa kuwekwa bayana ili kuondoa matamanio ya watoto wa masikini wenye nia ya kumrithi mfalme.

Sumu ya ufisadi imekwishawaingia wananchi. Kamwe haiwaelekezi wanasiasa walioisambaza sumu hiyo wafunge midomo yao na wageuke mabubu kwa kuogopa kuwaambia wananchi madhara ya umasikini wanaoupata kutokana na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Wananchi wanataka kumsikia mtawala wao akiwaambia ukweli juu ya tuhuma hizo na kuunda tume huru, kama Rais alivyoweza kufanya wakati wa vifo vya wafanyabiashara wa Kilombero waliouawa jijini Dar es Salaam na viongozi wa Jeshi la Polisi waliohusika na mauaji yao hadi leo wengine wapo mahabusu.

Tuhuma za rushwa na ufisadi haziwezi kutofautishwa sana na muuaji kwa kuwa mtu anayehujumu uchumi wa nchi anasababisha athari kubwa ndani ya jamii, pale watu wanapokosa huduma bora za afya, usafiri wa uhakika, maji safi na pembejeo za kilimo.

Ufisadi unaongeza umasikini kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wa kawaida na ndio hao wanaoilalamikia serikali kwa kushindwa kuwawekea misingi imara ya kuinua maisha bora wanayotarajia kuyapata, kutokana na mfumo mzuri na mipango ya serikali wanayotarajia kuwa ndiyo waandaaji wakuu wa sera na watekelezaji ni wananchi.

Rais Kikwete ana kila sababu ya kuwatoa kwenye giza nene na kuweka uwazi wa mambo mazito yanayotajwa na wapinzani kwa kuwa wananchi wanatambua kazi ya mahakama, wanatambua kazi ya polisi na wanatambua umuhimu wa kuwapo kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, kazi iliyopo mbele ya serikali ya awamu ya nne ni kuondoa makovu ya ufisadi.

Watu hawawezi kugeuka mabubu wala viziwi kama bado wanasikia na kuambiwa kuwa serikali ina makovu ya ufisadi. Wapo wanaotajwa kwani wanaotajwa si baraza lote la mawaziri wala watendaji wote wa serikali. Ni kundi ndogo linalotajwa, sasa uchunguzi utafanyikaje wakati watuhumiwa wanaendelea kuula?

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu; 0754 302 864 au baruapepe: cnyenyembe@yahoo.com
 
Yawezekana Mfalme wa Nchi ya kusadikika anawalakini Mama yake aliolewa akiwa na Mtoto mkubwa wa miaka mitano,je kweli mtoto huyuni wa nchi ya kusadikika?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom