Hebu chukuwa kalukuleta yako tufanye hesabu kwa pamoja..!!

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,326
92,503
a48971f5e9d0100bef664ac7a51199aa.jpg

HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE HESABU..!!
Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu.

Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini).

Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=).

Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako, Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. Tuache hayo. Najua utaniuliza, maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo, mbegu na mengine.

Tafadhali hayo maswali tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu). Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini, niletee nikupelekee Comoro na Madagascar. Kama umeungana na waliokariri kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe laivu!

Nimemaliza!
 
Hesabu za kufikirika kama nchi ya mwendokasi, hivi umeshajiuliza mvua za vuli zilivyonyesha chini kwa 35% ya kiasi kilichozoeleka! Basi tuwekee na gharama za kumwagilia hiyo heka moja na uchukulie unaishi Isuna au Hedaru.
 
Hii ni theory Wakuu,
Na always kunako theories basi "other things/factors kept constant". Laiti kama hizo factors zingine kama vile Mvua, Stable Market, Magonjwa, Uchaguzi wa aina bora za Mbegu, Hali ya Hewa, Usimamizi Mzuri, etc zisingekua constant basi hii theory kukamilika au kutimia ingekua vigumu sana.

So as a theory wacha tuikubali tu, ila in reality basi other factors should be considered also.
 
a48971f5e9d0100bef664ac7a51199aa.jpg

HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE HESABU..!!
Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu.

Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini).

Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=).

Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako, Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. Tuache hayo. Najua utaniuliza, maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo, mbegu na mengine.

Tafadhali hayo maswali tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu). Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini, niletee nikupelekee Comoro na Madagascar. Kama umeungana na waliokariri kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe laivu!

Nimemaliza!
Waza tena usijeingiaa hasaraa mkuu,, sikukatishii tamaaa
 
Ndio kwenye biashara lazima risk taking,lakini estimation zisizo na reality hatuwezi kuziterm kama ni risk taking,kwenye Kilimo 2m itengeneze 40m ndani ya miez tisa? Unalima uranium!?

Jaribu uanguke na sio kupiga mayowe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom