Cathy Diwani
Senior Member
- Feb 13, 2016
- 119
- 182
Nilipata tatizo la panick attacks na anxiety disorder kiasi cha miaka mitatu iliyopita hali iliyopelekea kuwa na mapigo ya moyo kwenda kasi, kuruka na moyo kupiga kwa nguvu kwa baadhi ya nyakati. Nilifanya vipimo vya moyo (ultra sound, ECO, na AKG lakini moyo ulikuwa normal kabisa, sikuonekana na tatizo.
Nikaambiwa shida ni stress hivyo nikapewa dawa za Propranolol na amytriptiline, shida ikaisha. Lakini nilipata tatizo likanifikirisha kiasi, tatizo linarudi, moyo kwenda mbio, kuruka mapigo na kupiga kwa nguvu kiasi naskia mpaka masikioni kishindo cha mapigo ya moyo.
Nimerudi hospitali, nimepewa dawa zile zile lakini hazinisaidii. Naona tatizo limekuwa kama ni mara mbili zaidi.
Kwa Sasa moyo unaruka mapigo mfululizo mpaka nahisi kama akili zinahama(feeling nervous)
Naombeni msaada kuwa wapi naweza kupata huduma ya tatizo hili. Nimepita pita mitandaoni angalau nimeweza kudhibiti panick attack, nimebaki na anxiety disorder maana kuwa wakati naogopa kitu ambacho sikijui mpaka najishangaa. Lakini pia nimekosa kujiamini, kuna muda najihisi kama sijakamilika.
Nisaidieni. Nimepitia changamoto flani za mahusiano ambapo nimeshazikubali kuwa ni sehemu ya maisha yangu.
Nisaidieni hapa kwenye mapigo ya moyo maana kuna muda nahisi kama moyo utasimama ghafla.
Asanteni