Healthy food: Watanzania tujali afya zetu

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu habari zenu?

Kuna kitabu kimoja nime bahatika kukisoma kinaitwa healthy food kimeandikwa na George D.Pamplona-Roger,M.D ,nilichokisoma humo ndio nikaamua nije niwaambie na nyinyi wakuu .maana naamini “We are what we eat”

IMG_4912.jpg


1.Daily intake

IMG_4913.jpg






2.Food compostion(muundo wa chakula)

IMG_4921.jpg


3.prepare and use


IMG_4926.jpg



4.Magojwa.

IMG_4923.jpg


IMG_4924.jpg




5.Chakula kwa ajiri ya nini?
IMG_4925.jpg









Watu wananiambia nacomplicate Maisha aisee.

Mimi sio daktari lakini swala afya yako sio mpaka daktari akuambie anza kula vyakula vya aina hii.

Nilichokiona ni kuwa watu wengi tunaugua sana na mwisho kufa kabisa kutoka na vyakula tunavyo kula na vyakula tusivyokula.

Kwenye hicho kitabu nilichikiona ni kwamba kuna kiwango unachotakiwa ule kwa kila virutubisho kwa mfano protini, Vitamin A, Vitamin B au calcium kuna kiwango chake kulingana na umri wako na jinsia yako sio

Tunasemaga karanga ina protini lakini ina protini kiasi gani maana karanga ina protini 25.8g, na wakati daily intake yako ya protini kulingana na umri wako wa kuanzia miaka 25-50 ni 63 kwa mume na 50 kwa mke, kuwa hiyo unakuwa umekula protini lakini sio kiwako kinacho takiwa kulingana na umri wako, maana hiyo ulitakiwa ule karanga, uongeze na na wali maharage ndio hiyo protini ifikie kiwango unachotakiwa ule kwa siku.

Nimekuwa nikitumia kitabu hiki kuangalia kila chakula kina muundo((composition) wa nini ndani yake yaani kina virutubisho gani kwenye hicho chakula mfano karoti ina madini ya calcium kiasi gani? Ina vitamin B,ina nguvu(energy) ,sodium,magnesium,sodium,potassium kaisi gani?hiyo inakuwa kwa kiwango cha namba maana kumbuka hapo juu nimekuonesha kiwango unachotakiwa kula kwa siku kulingana na umri wako.



Kwa hiyo ukijua unatakiwa ule kiwango gani unaenda kuangalia kwenye composition(muundo) wa chakula hicho utaona inakiasi gani?

Mfano natakiwa nile potassium 2000mg kwa mtu mzima na kwa siku mimi nimekula ndizi peke yake ambayo ina potassium 396mg, bado nadaiwa hapo potassium 1604mg nyingine ambayo nikiongezea kutoka kwenye korosho nakuwa naikamilisha.na kuwa siitaji kula tena chakula chenye potassium kwa siku hiyo.

Baada ya kuona daily intake na muundo wa chakula kuna kitu kingine hapa namna ya kuandaa chakula na kula.



Mfano namna ya kuandaa karanga na kula karanga kiafya wanashauri ziliwe mbichi au kukaanga lakini zisiwekwe chumvi.

Nimeweka picha hapo chini ya maelezo kutoka kwenye kitabu.

IMG_4926.jpg


Mfano mwingine ni katika upishi wa kabichi(cabbage) wanasema usizipike sana maana kuna sulfurous phytochemicals inakuwa inaondoka kutoka kwenye kabichi hiyo,

Mfano mwingine ni kitunguu kisikaangwe Zaidi ya dakika 1.



IMG_4928.jpg



IMG_4927.jpg





Kwa upande mwingine wa magojwa wamesema kwa ungojwa huu usile vyakula hivi na uongeze ulaji wa vyakula hivi.

Mfano wale nguvu za kiume wamezuiwa kula vya kula vyenye CHOLESTEROL,ALCHOLIC BEVERAGES… na waongeze kula vyakula vyenye antioxindant,ZINC…, nimeweka picha hapo chini.

IMG_4930.jpg




Na kingine ni kwa ujumla chakula hivi kinasaidia nini? Mfano cucumber(matango) chakula hiki kinasaidia nini ? kwa matango yanasaidia Ngozi,



Nimeweka picha hapo chini.

IMG_4934.jpg




Ni kazi sana kwa watanzania kufata muundo wa chakula na daily intake yake kwa siku lakini pia tunaweza kufuata ile kwa ujumla kwamba chakula hiki kina saidia nini?

Nilisha wahi kujiuliza hivi hii imekaaje hii unakuta mnaenda kula jamaa anasema mimi sipendi mafuta mengi maana haya mafuta sio mazuri haya,sisi wengine tunakula kila siku na hatupati matatizo yoyote wala nini.

Mimi nikaelewa hivi mfano na kula vyakula vya kuniletea koestro na halafu naenda kula kinga yake ambayo ni pera (guava), hapo koestro nitaisikia kwenye bomba tu.na hapo ni kwenye kila vitu Nimeweka picha ya pera hapo chini.
IMG_4937.jpg





Nilipofikia sasa kila chakula nachokula najua kinanisaidia nini mwilini na namna ya kukiandaa na kukila mfano nazi (madafu) wakati nakuwa nilikuwa nasikia yanaleta mabusha, kwenye kitabu hapo wamesema kwenye upande wa preparation and use nazi unaweza kula kama dafu na maji yake ukanywa , au ukatafuna pia, tunasikiaga kwa watu kuwa jamaa ameishiwa mafuta kwenye magoti yule, sasa nazi inasaidia kuongeza mafuta hayo kwenye magoti nikiwa nakula nazi nawaza yasije yakanikuta nanunua nazi nakula kwa muda wa siku hata siku tatu ,haiwi kwa siku moja tu.
IMG_4938.jpg



Mara nyingi nikiwa nasafiri wanakuwa wananishaanga ,kuna kipindi nilikuwa Mbeya kwa Rafiki yangu ananishaangaa kila nikirudi home nina machungwa anashaangaa mbona unakula sana machungwa ila mimi najua machungwa yanasaidia kukuimalisha kwenye magonjwa yakuambukiza(machungwa ni food for infection) kama mafua kwenye kitabu wanashauri machungwa ule kuanzia 4, nimeweka picha hapo chini.unakuta hapo kwenye machungwa nimejipa hapo kinga kwenye magojwa hayo ila pia ukiangalia kwenye nguvu za kiume kule wanasema uongeze vyakula vyenye antioxidant, na machungwa yana antioxindant na navyo kula inakuwa ni kwa muda wa siku kadhaa inakuwa kama vile dawa iliyo yaani kama dozi sio siku moja, nafanya hivyo ili nijipe kinga ya mwili wangu mafua nayasikia kwa watu yaani hakuna kuumwa.


IMG_4939.jpg

IMG_4940.jpg



Una kuta unasikia huyu anasma huyu, mara ya kwanza kusikia nikajiuliza hivi ni nini? Nikaambiwa anashindwa kupumua vizuri, sasa maswala ya kupumua vizuri yanasaiziwa na vitunguu , vitunguu ni food for respiratory system, ndio maana nikiwa nakula chakula lazima kitunguu nikile kabisa najua kabisa najizuia na ugojwa wa asyma, nikipika lazima mboga au kachumbali lazima vitunguu vionekane sio ili mradi , nakula kitu ili kiende kuimalisha mwili wangu (hekalu la mungu).

IMG_4942.jpg






Kuna muda una shangaa hivi nimekula nini mbona tumbo mbona kama haliko sawa hapo lazima nije kwenye food for the stomach, mimi hapo nachagua nanasi tumbo hapo lazima litulie hapo hapo narudia tena lazima litulie hapo hapo.

Kuna jamaa siku nimekuja na nanasi nikampa amekula mimi hapo nikaanza story nanasi linasaidia kuweka tumbo sawa kama lina shida , akaniambia kweli aisee naona hapa nimekula nanasi lako hapa najisikia vizuri sasa hivi maana tumbo lilikuwa linanisumbua sana aisee.

IMG_4943.jpg




Nyigine hii hapa unakuta mtu ana vidonda vya tumbo haelewi chochote, kwenye kitabu hapo wamesema cabbage(kabichi) inatibu vidonda vya tumbo ,kabichi bei rahisi tu mara moja moja weekend ijumaa,jumamosi na jumapili unakuwa umekula dozi ya dawa yaai kama ilitaka kukuanza lazima ikimbie, nimeweka picha hapo chini bila kusahau preparation and use maana ukiipika sana hiyo virutubisho vya sulfurous phytochemicals vinaondoka.

IMG_4927.jpg

IMG_4944.jpg






Katika kukuwa kwangu tulikuwa tuna bishanaga sana eti ugali na wali upi una nguvu sana .

Sasa nilivyokuwa na kitabu iki tukaangalia kwenye muundo yaani kwenye composition tuone nani anaenergy sana kati ya rice na mahindi tukaona corn imezidiwa mara nne ya rice(mchele)

Nimeweka picha hapo ya corn na rice angalia energy hapo nani anaenegy nyingi tuache maneno mengi?

RICE ENERGY IN 1508 KJ NA WAKATI CORN MAHINDI NI 358KJ

IMG_4945.jpg

IMG_4947.jpg




Kuna kipindi wife alikuwa ameenda kliniki akaniambia amepimwa ameambiwa ana damu 8 alipaniki balaa. mara nyingi mambo ya vyakula haya huwa hanisikilizi kabisa lakini alivyoambiwa hivyo akanisikiliza , nikachukua kitabu nikaenda sokoni mwenyewe.baada ya siku nne akapima nilimuongeza damu ndani ya siku nne damu ikawa 12 kutoka kwenye 8, wakasema haiwezekani labda agha khani walipima vibaya lakini mimi najua nilifanyanini na nilifanya kisomi Zaidi sio kimazoea.



Hii sasa ikanishangaza maana tulikuwa tunaambiwa limao linakausha damu kwenye kitabu nimekuja kukutana hii eti ina zalisha nakushafisha damu, picha hipo hapo chini

IMG_4958.jpg




Spinach na carrot zinasaidia kwenye macho mtu kuona vizuri angalia kwenye macho kuona unaitaji kuwa na vitaminiA ukiangalia kwenye muundo wa hicho chakula utaona kuna vitamini A vingi sana kushinda vyakula vingine.

Nyingine hii hapa Kipindi cha covid19 vidonge vya Vitamini C viliadimika madukani , kuna mwamba yeye anakuja ofisini na mapera mzee anakula mapera, nikarudi kwenye kitabu kumbe pera ndio tunda lenye Vitamini C vingi kushinda tunda lolote lile, nimekagua kwenye kitabu chote hakuna chakula kilichozidi pera(guava) kwa kuwa na vitamini C vingi pere lina vitamini C 184mg.bila kusahau kula papai au nanasi ili upate choo laini. picha iko chini hapa

IMG_4937.jpg


Kuna nyingine hii hapa watu wanasema jamaa ana anemia yaani anaupunngufu wa seli nyekundu za damu yaani huyo anatakiwa ale parachichi picha iko chini hapa.

IMG_4960.jpg


Kuna vyakula kwa ajili ya figo kuimalisha figo yako figo imefail wewe vyakula vya kuimalisha figo hauli unakunywa tu pombe,



IMG_4961.jpg

IMG_4962.jpg

IMG_4962.jpg






Kuna hii ya tezi dume nyanya zinasaidia usipate tezi dume maana yake umekosa madini yanayopatikana kwenye nyanya ndio maana tezi dume umepata, Nyanya zinazuia usipate tezi dume. Kwa upande wa nyanya hapa ile tomato source wanasema tatizo kunakuwa na chumvi kwenye tomato source, picha iko chini hapa bila kusahu preparation and use.

,na kingine hapa ishu ya kunywa red wine wanashauri unatakiwa unywe 200ml kwa siku kuzuia heart attack,sasa wine 200ml hiyo mbona utani huo wine ilivyokuwa tamu vile,na wamependekeza ni red wine .
Ni hayo tu wakuu picha ambazo hazija onekana vizuri nitakuwa nazituma tena kama utataka kusoma Zaidi.
 

Attachments

  • IMG_4913.jpg
    IMG_4913.jpg
    54.6 KB · Views: 10
  • IMG_4927.jpg
    IMG_4927.jpg
    49.3 KB · Views: 11
Asante kwa kutujali na kujali afya zetu

Ila ukitaka kuwakatisha tamaa wabongo wadokeze hicho kitabu kinauzwa sh ngapi?
 
Mkuu Asante..
Ila limao na pera kipi kinavitameni c nyingi

IMG_4937.jpg

Angalia hapo kwenye composition (muundo)pera ina vitamin C kwa kiwango hicho hapo 184 mg ,matunda mengine hayaja fikia hicho kiasi
Mengine yanaishiA tu kwenye kiasi cha 5mg

Limao linA kiwango cha 53mg cha vitamin C.
View attachment 2401701


Pera Lina kiwango Kikubwa
 
UKitaka kufa mapema komaa na izi guidelines.
Kula na kunywa kila kitu moderately mengine mwachie Mungu.
KUna mahala article ya DR kabisa ankataza maziwa maji vegetables na anatoa sababu kabisa nkachoka.
 
UKitaka kufa mapema komaa na izi guidelines.
Kula na kunywa kila kitu moderately mengine mwachie Mungu.
KUna mahala article ya DR kabisa ankataza maziwa maji vegetables na anatoa sababu kabisa nkachoka.

Sema kama tunaona kama tunanyimwa uhuru,tumeshazoea maisha yetu ya kula junk food.

Sasa hao inategemea unaumwa nini?

Unaweza kufuata baadhi tu taratibu taratibu baada ya hapo utazoea
 
Sema kama tunaona kama tunanyimwa uhuru,tumeshazoea maisha yetu ya kula junk food.

Sasa hao inategemea unaumwa nini?

Unaweza kufuata baadhi tu taratibu taratibu baada ya hapo utazoea
Uzuri Mungu kanipa akili ya kupembua zuri na baya na pia access ya articles mbali mbali za afya najua namna ya kubalance baada ya apo
 
Back
Top Bottom